Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Kuna watu wanaamini kabisa kuwa Bwawa la Umeme la Rufiji likianza kazi basi suala la Mgao wa umeme litakuwa historia kwenye nchi hii.
Kwa namna ninavyosoma taarifa mbalimbali za kiutafiti zinazohusu masuala ya Mazingira napenda kuwaambia hawa watu wakiwemo viongozi wetu kuwa inawezekana wakawa sahihi kwa muda fulani ila kwa muda mrefu hawatakuwa sahihi
Kwa hali ya mabadiliko ya hali ya hewa ilivyo inasemwa kuwa huko mbeleni suala la ukame litakuwa jambo la kawaida sana duniani na inawezekana hata uzalishaji wa chakula ukapungua sana.
Kwa haya ni sahihi kusema kuwa hata Bwawa la Nyerere inawezekana lisiwe efficient kwa miaka mingi ijayo kutokana na changamoto hizi.
Kwa upande mwingine kuna vyanzo ya umeme vinavyoonekana kuwa vya uhakika zaidi katika miaka mingi ijayo. Vyanzo hivyo ni pamoja na Nyuklia na Jua ambavyo kwa bahati nzuri sana vyote kwa hapa Tanzania tunavyo.
Ushauri wangu.
1. Kuna teknolojia mpya salama zaidi ya kutengeneza plant ndogo za nyuklia. Serikali ialike wataalam kutoka nchi za Ujerumani au Scandinavia wajenge hata plant moja ya namna hiyo kwenye moja ya mikoa yenye bahari/ maziwa hapa Tanzania. Tukipata megawat hata 10,000 au 20,000 sio mbaya. Uzuri madini ya uranium tunayo kinachotakiwa ni teknolojia tu.
2. Kuna mikoa/ sehemu hapa nchini ambayo Jua linawaka kwa uhakika kwa miezi si chini ya 10 au 11. Serikali iwekeze haraka uzalishaji wa Umeme Jua kwenye mikoa hii hata megawat 3000 - 5000
Inawezekana watu wakasema tuna gesi ila kiuhalisia gesi tuliyonayo ni ya matumizi ya miaka 30- 50 kama sikosei hivyo inawezekana huko mbeleni nayo ikaisha.
Naomba kuwasilisha.