Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,059
Ukizungumza na baadhi ya wataalam wa TANESCO, wanasema mgao wa umeme ni wa kutengenezwa. Sababu za kutengeneza mgao huo zinatajwa ni ubinafsi wa baadhi ya watu, LAKINI nyingine inayotajwa ni maelekezo kwa nia ya kuisadia CCM.
Kati ya mashirika ambayo yametumika sana kuwatajirisha baadhi ya wafanyabiashara na baadhi ya wanasiasa, kwa njia haramu, ni TANESCO. Na hali hiyo imekuwepo wakati wote, na sasa imekomaa.
Kuna wakati uhaba wa umeme ulitengenezwa ili uhaba huo utoe uhalali wa kununua umeme toka majenereta ya makampuni binafsi. Kuna wakati uhaba wa umeme umetengenezwa ili wafanyabiashara wa majenereta wapate soko kubwa la majenereta yao.
Kauli tu moja ya Magufuli kuwa hataki mgao wa umeme au la mkurugenzi na watu wake watafukuzwa kazi, ilitosha mgao kukoma na umeme kuwa wa kutosha.
Hatimaye wafanyabiashara walipofanikiwa kumwingiza mtu wao kuwa Wairi, mgao ulianza. Na ilipoonekana mgao ni mdogo, akaamrisha bwawa lifunguliwe, maji yapungue, akitengeneza sababu kuwa maji yakiwa mengi yatabomoa kingo za bwawa. Wataalam wa TANESCO waliokataa, walihamishwa kitengo, na walioletwa wakafungulia maji yapotee ili mazingira ya mgao yaimarike.
Kwa sasa, sababu za huo mgao wa kutengenezwa, wapo wanaosema ni maslahi binafsi ya wafanyabiashara wakubwa, LAKINI ambayo inasemwa zaidi ni hii ya CCM kutafuta pesa za kampeni kupitia kwa wauzaji wakubwa wa majenereta makubwa ya umeme.
Kama Serikali, CCM, waziri aliyetoa amri maji yafunguliwe ili mabwawa yapungukiwe maji, na baadhi ya watendaji wakuu wa TANESCO hawahusiki na huu upungufu wa umeme wa kutengenezwa, kwa nini isiundwe tume huru ya kuchunguza kuwabaini wahusika halisi wa huu upungufu wa umeme wa kutengenezwa? Kwa sasa, kwa ujumla kuna hasara ya mabilioni ya pesa yanayopotea kutokana na kutokuwepo umeme. Kwa nini Taifa zima liangamie kwaajili tu ya manufaa ya CCM au waziri au maafisa wa juu wa TANESCO?