Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Habari za jioni wana JF natumaini wote humu ni wazima.
View attachment 885770
Nlipokuwa naipitia uzi huu Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote! - JamiiForums

Mkuu Elungata aliibua hoja kuhusu Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja na nathan ila muanzisha uzi alipotaka ushahidi aliuwekea condition hii.

Baada ya kusoma hii comment nilisikitika sana na nilijiuliza sana kwamba inakuaje kila story ya watu waliotajwa kwenye bible watu wanataka reference kutoka ndani ya Biblia pekee as if Biblia imeandika kila kitu?? Kwanini tunapenda kujifunga akili kiasi hicho?

Baada ya kuona mentality hiyo imeanza kukua humu JF intelligence nikaona nilete mada jinsi Biblia yenyewe imetutuma tukasome vitabu vingine nje ya Biblia ili tuongeze ufahamu kuhusu baadhi ya watu na matukio ambayo Bibila yenyewe haikuandika yote kwa upana wake, hivyo nia ya uzi huu ni kwa wale waliojifunga kwenye kusoma maandiko pekee wabadilike na kuwa na fikra huru na kuruhusu maarifa kutoka kona zote kwa mithiri ya kujifunza zaidi na kupanua uelewa wa mambo.
View attachment 885772
Kwa kuanzia tu labda nitumie nafasi hii kumjibu mkuu wangu maishapopote kuwa hata biblia yenyewe inakiri kuwa maisha yote ya Daudi yameelezewa vizuri zaidi nje ya Biblia hivyo imetutuma tukasome vitabu hivyo mnavyoita vya kipagani ili tujifunze kwa ufanisi zaidi

1 NYAKATI 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.

Vitabu vilivyotajwa hapa ni Book of Gad the seer,Book of Nathan the prophet, Book of Samuel the seer (Sio samuel 1&2) ambavyo kwenye biblia havikuwekwa . Sasa kama Biblia inakiri kuwa sio kila story yake imeongelewa kwa upana wake katika biblia je kwanini siku hizi watu wakijengea hoja kuhusu personality za biblia mnalazimisha reference iwe ndani ya bible pekee??? Ina maana waandishi wa Biblia ni wajinga hadi watutume tukasome hivyo vitabu vingine ambavyo mnaviita vya kipagani??

MAANDIKO
Hapa chini nimeambatanisha vifungu vya Biblia hivyo ningeomba tuisome kwa makini kabla ya kuchangia hoja. Neno Tarehe kwenye maandiko haya kwa kiswahili rahisi inamaanisha Nyaraka/rekodi/kitabu au kwa kizungu book/journal/Annal.
View attachment 885773

1. Kitabu cha Yehu

2 Nyakati 20:34
34 Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

2. Kitabu cha Nabii Gadi muonaji/ Kitabu cha shemaya

2 Nyakati 13:22
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

2 Nyakati 12:15
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

1 Nyakati 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.

3. Kitabu cha mfalme Ahasuero

Nehemiah 12:23
23 Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu

Pia kinatajwa Esther 10:2, 2:23, 6:1

4. Matendo ya Mfalme suleiman

1 wafalme 11:41
41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani (Book of Acts of Solomon)

5. Nyakati za wafalme wa Israel & Yuda

1 wafalme 14:19
19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.(chronichles of the kings of israel/Judah)

6. Kitabu cha Hozai

2 Nyakati 33:19
19 Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.

Hivi ni kwa uchache tu ila kuna vitabu vingine zaidi ya 20 vinatajwa kama reference point kwenye biblia ilihali havipo kwenye Biblia na wala havitambuliki na kanisa lakini leo hii akijengea mtu hoja anaonekana shetani!!
View attachment 885774

HITIMISHO
Baada ya uzi huu nisingetegemea tena kusikia wana JF wakitaka reference kutoka kwenye biblia pekee ilihali Biblia yenyewe inataka tukarefer kwenye vitabu vingine ambavyo vingi ni vya kipagani tu ili tupate uelewa zaidi ya watu muhimu kwenye bible.

However ningependa tujiulize maswali haya ili kupanua fikra zaidi

1. Kwanini vitabu hivi ambavyo Biblia inaturefer tukasome ili kuelewa baadhi ya matukio havikuwekwa kwenye biblia??

2. Na kama havikuwekwa kwa sababu yeyote ile je ina maana ni vya kipagani??

3. Na kama ni vya kipagani ni kwanini vimekuwa referred kwenye bible?

4. Kuna vitabu vingine ambavyo vimenakiliwa hapa ni halali kabisa katika kanisa la kale lakini kwa sasa viko categorized kama vitabu vilivyopotea.... Je nini hatma ya Biblia kama maneno ya Mungu ilihali yanaweza kupotea??

5. Na kama yamepotea je ina maana biblia haijakamilika sababu sehemu ya stori yake imepotea??

Naomba kuwasilisha

Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu
Nilitarajia kwamba utaweka vitabu hivyo hapa kwenye thread yako tufanye rejea, kumbe unakuja na hoja isiyo mashiko!? Hakuna kipya katika uliyoandika, muhimu kwako, weka hivyo vitabu hapa, pili weka uushahidi wa mapenzi ya jinsia moja ya mfalme Daudi. Kukurupuka kubaya sana.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Soma vizuri mada...... Huyo Nabii Gadi au Nabii Nathan vitabu vyao HAVIPO kwenye Biblia maana kanisa limeviterm vitabu vyao kama Pseudepigrapha/Apocrypha hivyo havitambuliki kwenye Bible na vinahesabika ni vya kipagani tu.

Sasa nikuhoji wwe... Je kwanini basi Biblia inatoa reference kutoka vitabu vya kipagani?? Ila sisi wana JF tukitoa reference kutoka vitabu vya nje ya bible mnakataa hoja zetu??

Tuanzie hapo kwanza
Huna ujualo, hapo juu imewekwa picha ya kitabu, The lost books of Eden, unadhani kwa nini vimeitwa hivyo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nilitarajia kwamba utaweka vitabu hivyo hapa kwenye thread yako tufanye rejea, kumbe unakuja na hoja isiyo mashiko!? Hakuna kipya katika uliyoandika, muhimu kwako, weka hivyo vitabu hapa, pili weka uushahidi wa mapenzi ya jinsia moja ya mfalme Daudi. Kukurupuka kubaya sana.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Tunapoingia kwenye mijadala isiwe kama vita ila kuelimishana kwahiyo hoja ipingwe kwa hoja sio matusi na kejeli

Kwa kuanzia Mzizi wa hoja sio ushoga wa daudi labda uonyeshe ni wapi nimetetea hiyo hoja?? Ila mzizi wa hoja ni referencing external texts for biblical stories and chronology.

Sasa basi hoja inakuja kwanini humu JF ukieleza mfano historia ya Nimrod au Cain kutumia Book of Jasher au Enoch inapingwa kwa misingi kwamba haipo ndani ya Bible...... Ilihali bible hiyo hiyo ina cite Book of Enoch na jasher??

Tuanzie hapa kwanza
 
Huna ujualo, hapo juu imewekwa picha ya kitabu, The lost books of Eden, unadhani kwa nini vimeitwa hivyo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Kweli sifahamu kitu ndio maana nimeleta humu hoja ili wajuzi mnisaidie.

Lost books of Eden kina vitabu kama First book fo Adam and Eve, Apocalypse of Abraham n.k ambavyo vipo categorized kama pseudepigrapha na mainstream christianity kama tu hivyo vingine mfano Book of Gad the seer au Wisdom of solomon ila bado vimekuwa cited na Biblia.

Sasa swali ni je kwanini baadhi ya vitabu vilipotea?? Mfano Paul's letter to Laodicea?. Je nini hatma ya neno la Mungu kama maneno yake yanaweza potezwa na watu??

Na je msimamo wako ni upi watu kucite hzi pseudepigrapha/Apocrypha ili kujengea hoja za Biblia maana hata Bible authors kama Mtume Yuda na Muandishi wa kitabu cha Yoshua wamevinakili??

Natanguliza shukrani
 
Bado namalizia kusoma kitabu cha The Satanic Verses cha Salman Rushdie. Nikimaliza nitakuja kutoa maoni yangu.
Hiyo fiction story ina uhusiano gani na mada?? Tatizo kila mtu anayehoji Biblia mnadhani ni muislam?? Ina maana hatuwezi kuwa na wakristo wanaohoji mambo yanayowatatiza??

You can do better than this
 
Tunapoingia kwenye mijadala isiwe kama vita ila kuelimishana kwahiyo hoja ipingwe kwa hoja sio matusi na kejeli

Kwa kuanzia Mzizi wa hoja sio ushoga wa daudi labda uonyeshe ni wapi nimetetea hiyo hoja?? Ila mzizi wa hoja ni referencing external texts for biblical stories and chronology.

Sasa basi hoja inakuja kwanini humu JF ukieleza mfano historia ya Nimrod au Cain kutumia Book of Jasher au Enoch inapingwa kwa misingi kwamba haipo ndani ya Bible...... Ilihali bible hiyo hiyo ina cite Book of Enoch na jasher??

Tuanzie hapa kwanza
Kwani unajua sababu yoyote kwa nini vitabu hivyo havikuwe kwenye biblia? Je, nakala zake halisi zipo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Kwani unajua sababu yoyote kwa nini vitabu hivyo havikuwe kwenye biblia? Je, nakala zake halisi zipo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Yes kuanzia compilation ya Alexandria, mpaka council of Jamnia hadi Father Jerome akitafsiri biblia kuwa ya kilatin kutoka Hebrew/Greek vitabu vilitengwa kama pseudepigrapha kwamba havikuvuviwa na Roho mtakatifu.

Sasa cha kushangaza hiyo sababu tuliopewa kwanini Mtume Yuda ali cite Bool Enoch ilihali tunaambiwa hakikua na uvuvio wa Roho?? Ni kwanini Yoshua alinakiri Kitabu cha Yashari ilihali tunaambiwa hakikuvuviwa??

Hizi double standard ni kwa faida ya nani

NB: Inaonekana kauli ya ushoga imekukera sana lakini ni vizuri ufahamu King James Version bible ilitafsiriwa na kusambazwa na kuitwa kwa Jina la mfalme James wa kwanza alikuwa shoga na aliishi na mwanaume.

2. Ni vizuri ufahamu NIV hii ambayo ndio inatumika kuliko biblia yeyote duniani ilikuwa sponsored na Harper collins (Zondervan) wakapewa patent wawe pekee watakaochapisha dunia nzima. Ni muhimu uelewe taasisi hii inasupport ushoga kwahiyo kila unaponunua Biblia ya NIV jua inaenda support gay pride movements duniani.

Ni hayo tu
 
Ufalme was mbiguni hauji kwa kuuchunguza.hata Mussa kabla kuwaongoza wa Israel aliua mtu.kwa habari hi unataka iweje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama uchunguzi utaujuaje??
Ukisoma Zaburi 78:2 na Mathayo 13:11-13 inasema siri za ufalme zimefichwa kwenye mafumbo na kwamba Yesu aliongea kwa mafumbo, hivyo bila uchunguzi hata huo ufalme utauelewa vp.

Mfano Mat 24:15 ni siri ya ufalme wa Mungu je ni wangapi wanaelewa lile fumbo?? Ila ukichunguza maandiko deep na deep ndio utaelewa muktadha wake.

Sasa wakristo kama ww mnafuata upepo tu hata hamuelewi Kwani A ni A na sio B. Hata nikikuuliza kwanini Yesu alikufa msalabani na sio kwa mshale huwezi jibu kabisa.

Wakristo tupende kutafiti ili tuweze kuijua imani yetu tusifuate upepo tu
 
Kuna watu aidha kutokana na kuwa na mioyo midogo ama vipi wanamshambulia mwenye uzi bila mpangilio..
Ingependeza sana watu mjadiliane kwa hoja kistaarabu...naamini kila mmoja ana la kujifunza kwa mwenzie
 
Mkuu huwa napata confusion ya nini maana ya secret society,,kwamba freemason walio kwenye kundi la secret society watu wasio washirika na washirikina wanapata wapi kujua Mambo yao??

Sasa kwa nini kile mnachokiita habari za kutoka kwao tusiseme ni za uwongo mtupu??

Naomba niweke jambo moja sawa..............

Kuhusu hekalu la Suleiman.Blueprint au ramani ya hekalu,,au mwongozo wa namna ya kujenga hekalu lile haukutoka kwenye mawazo ya Suleiman wala sio wazo lililoingia kwenye moyo wa Suleiman,,,ramani ile alipewa Daudi baba yake.

Kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana vita vingi na kumwaga damu nyingi kazi ya kulijenga hekalu akapewa Suleiman.Lakini aliambiwa namna litakavyokuwa.Na alilijenga kulingana na alivyoambiwa na Daudi baba yake.

Kingine ujenzi wa hekalu mpaka kukamilika kwake kumeelezwa kwa kina katika biblia wala haihitaji vitabu vya nadharia na hadithi kuongeza chumvi na uwongo eti majini(uchafu/takataka) zilishiriki ujenzi kitu ambacho ni absurdity na nonsense.

Kuhitimisha,,lile halikuwa hekalu la Suleiman ila lilikuwa hekalu la Mungu muumba wa mbingu na nchi.
Na maelezo yake ya kina yote mwanzo na mwisho wake vipo ndani ya kitabu kimoja chenye muongozo wa kutosha biblia.
Huu ni ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia..... Ukisoma hata Muongozo wa ibada za Scottish rite freemasonry degree ya 6 inahusisha kutafuta missing pieces kwenye hekalu la suleiman. Kwahiyo kuna patterns unatakiwa uzitafute kwenye ramani ya lile hekalu ambapo inahusisha kusafiri kiroho/kiakili hadi wakati ule hekalu linajengwa.

Ni ibada nzito sana na kwenye katiba yao inaongelewa vizuri sana ila ukileta huo mjadala humu unaweza onekana ni ibilisi fulani hivi maana watu wamemsoma kwa upande mmoja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ya James kuwa shoga ni Habari yenye utata,,haikubainika wazi kwamba yeye alikuwa biskuti.
Pia alitoa amri kwa baraza la kanisa kuandika biblia ila hakushiriki kwa namna yoyote kwenye uandishi.
Kwa hio watu walioandika KJV walikuwa watu safi wote hakuna hata mmoja wa kundi la watu wapungufu wa akili(mashoga)

Katika kijarida fake(New International version) waandishi waliokuwa wapumbaf wakubwa na wakadiriki kuondoa maneno mengi ndani ya biblia rasmi,,,miongoni mwao walikuwepo mashoga wawili.Hii ndio sababu ya kila mkristo mwenye hichi kijarida anatakiwa akipeleke vyoo vya vijiji vyenye baridi kali ili visaidie watoto wa shule za awali kuchambia.

Kwa hio haiwezekani kufananisha biblia na jarida fake la watu walioamua kwa makusudi mazima kuwa wapumbaf.
Yes kuanzia compilation ya Alexandria, mpaka council of Jamnia hadi Father Jerome akitafsiri biblia kuwa ya kilatin kutoka Hebrew/Greek vitabu vilitengwa kama pseudepigrapha kwamba havikuvuviwa na Roho mtakatifu.

Sasa cha kushangaza hiyo sababu tuliopewa kwanini Mtume Yuda ali cite Bool Enoch ilihali tunaambiwa hakikua na uvuvio wa Roho?? Ni kwanini Yoshua alinakiri Kitabu cha Yashari ilihali tunaambiwa hakikuvuviwa??

Hizi double standard ni kwa faida ya nani

NB: Inaonekana kauli ya ushoga imekukera sana lakini ni vizuri ufahamu King James Version bible ilitafsiriwa na kusambazwa na kuitwa kwa Jina la mfalme James wa kwanza alikuwa shoga na aliishi na mwanaume.

2. Ni vizuri ufahamu NIV hii ambayo ndio inatumika kuliko biblia yeyote duniani ilikuwa sponsored na Harper collins (Zondervan) wakapewa patent wawe pekee watakaochapisha dunia nzima. Ni muhimu uelewe taasisi hii inasupport ushoga kwahiyo kila unaponunua Biblia ya NIV jua inaenda support gay pride movements duniani.

Ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huu uzi ulianzisha? Nitag tafadhali
Dah mkuu umenigusa sana..... Umeshasoma gospel of judas iskariot?? Imenifungua kichwa sana itabidi nianzishie uzi wake kabisa maana inaelezea chanzo halisi cha Yuda kumsaliti Yesu na "injili" ya kweli ambayo Yuda pekee ndio alipewa na mengine mengi yenye uhalisia ila ndio hivyo kimetolewa nacho..... Anyway nasubiri mkuu utueleze kidogo hapo kuhusiana na sababu kwanini baadhi ya vitabu imebidi vifichwe

Ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitegemei mtu mwenye akili timamu akasema Daudi Alikuwa basha!! Wazungu wanaita ridiculous au pia total crap au pia utter nonsense.
Tafuta ukweli usiweke hisia na imani mbele bila kutafuta ilipo kweli.
Kama aliweza kutamani mke wa askari wake na kumpeleka vitani auwawe kisha amtwae mke wa marehemu, anashindwa nini kufanya jambo lingine lolote la kibinadamu kama ubasha ilihali yeye ni binadamu wa kawaida?
 
Kwa kukusaidia vilivyoandikwa kwenye Bible ni vile tu vilivyokuwa tested na kuthibitika kweli, yale yasiyo na uhakika japo yaweza kuwa kweli yakatupwa nje.
Nani aliyejipa mamlaka hayo ya kimungu kuchagua kukataa baadhi ya injili na kukubali zingine?
 
Mkuu huwa napata confusion ya nini maana ya secret society,,kwamba freemason walio kwenye kundi la secret society watu wasio washirika na washirikina wanapata wapi kujua Mambo yao??

Sasa kwa nini kile mnachokiita habari za kutoka kwao tusiseme ni za uwongo mtupu??

Naomba niweke jambo moja sawa..............

Kuhusu hekalu la Suleiman.Blueprint au ramani ya hekalu,,au mwongozo wa namna ya kujenga hekalu lile haukutoka kwenye mawazo ya Suleiman wala sio wazo lililoingia kwenye moyo wa Suleiman,,,ramani ile alipewa Daudi baba yake.

Kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana vita vingi na kumwaga damu nyingi kazi ya kulijenga hekalu akapewa Suleiman.Lakini aliambiwa namna litakavyokuwa.Na alilijenga kulingana na alivyoambiwa na Daudi baba yake.

Kingine ujenzi wa hekalu mpaka kukamilika kwake kumeelezwa kwa kina katika biblia wala haihitaji vitabu vya nadharia na hadithi kuongeza chumvi na uwongo eti majini(uchafu/takataka) zilishiriki ujenzi kitu ambacho ni absurdity na nonsense.

Kuhitimisha,,lile halikuwa hekalu la Suleiman ila lilikuwa hekalu la Mungu muumba wa mbingu na nchi.
Na maelezo yake ya kina yote mwanzo na mwisho wake vipo ndani ya kitabu kimoja chenye muongozo wa kutosha biblia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tatizo umeassume kuwa characters wa Biblia wote ni malaika mfano hapa unampamba suleiman kuwa mtu wa MUNGU haswaa asiye na kasoro hadi kuhusianishwa na ibada ya giza.

Naomba ukasome wafalme 11:11 uone jinsi Mfalme Suleiman unayempamba humu alivuohusika kujenga Mahekali ya miungu wa kibabylon wanaotumiwa na secret societies nyingi duniani kuanzia Baphomet mpaka Molek!!

Kwahiyo si kweli alijenga hekalu la Mungu pekee bali mahekali zaidi ya 1000 ya miungu mingine mingi na matambiko mazito yalikua yakifanyika ila propaganda za wazungu zinatuaminisha ndio mtu aliyekua na hekima kuliko wote ilihali ndio aliyeharibu kabisa ufalme wa Israel ukafutwa mpaka leo hii

Mkuu amka
1 KINGS 11 soma yote uje na feedback
 
Mkuu huu uzi ulianzisha? Nitag tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu nina muda kidogo niliacha kupost mada za kiimani maana humu watu wakisikia jambo jipya ni mapovu tu hamna watu walio tayari kujifunza kitu kipya wao walishaamua A ni A hawataki kuambiwa kuna B.

Kibaya zaidi hawabishi kwa hoja bali vitisho na kejeli mwisho wa siku uzi unageuka uwanja wa vita za kidini na kupoteza maana.
 
Dah, tunaopenda elimu na vitu vipya kichwani tunakosa madini mazuri basi tu, mkuu uko deep sana ila nikwambie ni wachache sana ndio wanazingua, ila wengi sana tunavutiwa na kujifunza sana kupitia posts zako.. tufikirie mkuu
Hapana mkuu nina muda kidogo niliacha kupost mada za kiimani maana humu watu wakisikia jambo jipya ni mapovu tu hamna watu walio tayari kujifunza kitu kipya wao walishaamua A ni A hawataki kuambiwa kuna B.

Kibaya zaidi hawabishi kwa hoja bali vitisho na kejeli mwisho wa siku uzi unageuka uwanja wa vita za kidini na kupoteza maana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama habari ya kumchafua Nabii Daudi ilitoka kitabu kingine kisicho biblia inatakiwa tujiulize kama kina faida ya kukisoma na kukijadili.

Back
Top Bottom