mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,419
- 17,758
1. Mkuu naposema standard bible namaanisha hii set kama ya Genesisi to Revelation but nachojua vilikuwepo vitabu mbalimbali mfano Torah na vitabu vya manabii wengine wa kiyahudi kwa mamia yake (sio 39 pekee) na wote tunajua kuna baadhi ya vitabu kama ufunuo wa yohana imeandikwa miaka mingi baada ya Yesu kufa hivyo unaposema standard bible ilikuwepo wakati wa Yesu hatuwezi kuwa realistic.
Kuhusu vitabu hivyo vilivyoachwa kuwa vitakatifu ni evident sababu tunaona Yuda na Petro wakifanya direct quotation ya maandiko ya Kitabu cha Henoko.... Hivyo kma sio matakatifu sidhani kama wangeweza kuyaquote na kujengea hoja kama ambavyo waliquote vitabu vya isaya,zaburi n.k
2. Kuhusu compilation
Kwa uelewa wangu kufikia AD 300 kulikuwa na vitabu na nyaraka mamia yanasambaa yakidai ni maneno ya mitume sasa ili kuzima hiyo sintofahamu ikabidi wafanya new testament canonization ili wapate standard bible ya kutumika ulimwengu kote.... Mfano Council of Rome kufikia AD 382 ndipo walipotoa complete list ya vitabu vya Biblia ambavyo ndio halali kabisa na kwa mara ya kwanza kanisa likatambua vitabu 27 ingawa kabla ya hapo vitabu vilikuwa vingi vinazagaa so baada ya mchakato wa kuvikagua ndio wakafikia conclusion kuwa Biblia halali ni hii kwa mara ya kwanzo ilikuwa 382 ikimaanisha kabla ya hapo hakukuwa na standard Biblia hivyo mnaposema kuwa vitabu vilivyoachwa vinakinzana na maneno ya mitume sidhani ni sahihi unless ungesema watu waliocompile Biblia waliamua kugawa vile vinavyokubaliana kutoka kwa vinavyopingana (Collect like terms) ila mnaposema vinakinzana na manabii it's as if Biblia (yaani vitabu 66/72 n.k) ilikuwepo ndipo vikaandikwa hivyo vingine kma cha Enock au Jasher ili viipinge Biblia hicho ndio nachoona sio sahihi.
3. Pia unasema vilivyopo ndio vinakidhi vigezo.... Sasa hivyo ambavyo unasema havikidhi vigezo ni kwanini Biblia inaviquote na kuvirefer tukasome??
Kama vinatosha sasa kivipi kanisa ulimwenguni liliruhusu kuwa na Biblia tofauti mfano catholic wawe na 72, protestant 66 hapo bado martin Luther naye alipunguza baadhi ya vitabu ambavyo protestants wengine wanavitumia (refer luther bible) hapo bado kuna orthodox la tokea enzi na enzi la huko Ethiopia lina vitabu 84!!! Sasa kwa staili hii who is right and who is wrong?? Na kama one is wrong kuongeza au kupunguza vitabu je ni kwanini Mungu ameliruhusu hilo kuwa kanisa lipotoshwe na watu wachache??
Embu tuwekane sawa mkuu maana kupitia maswali haya tunajifunza mengi, ubarikiwe
1: stanard bible ya wqkati wake mkuu sio agano la kale na jibya. Naamini kabisa katika maandishi yote ya wakati wa Yesu yalikuwa hayapewi hadhi sawa. Yalikuwepo maandishi na '' Maandiko matakatifu''. Hata Yesu alitenganisha kati ya "maandiko matakatifu'' na ''Desturi za wazee''.
Ikiwa yalikuwepo, na huko nyuma nimesema kulikuwa na utaratibu wa kuyahifadhi. Naomba ushahidi kuwa hadi kitabu cha enoch kilikuwa sehemu ya hebrew holy inspired writings maana hata Apokrifa havikuwa sehemu ya Bibilia. Hata Jerome alipocompile vulgate alivitenganisha na vingine kuonyesha kuwa havina hadhi sawa.
Na ninachokisisitiza msingi wa utambuzi wa maandiko matakatifu ni resonance ya waandishi hao wasiopingana na hakuna anayefundisha kitu kipya.
Katika reference zote za Yesu na manabii anarefer wa vitabu vinavyofahamika na havipingani na mafundisho ya bibilia.
2:Nadhani kuna sababu nyingi zilizopekelea hivyo vitabu visiwe sehemu ya maandiko nanvingine viwe sehemu ya maandiko.
ambazo zinamashiko na hata mimi nakubaliana nazo ukijumuisha na za martino luther. najifunza zaidi hapo. Ila unapoleta hoja za 300AD unapaswa kuchanganya na hoja za Karne ya pili BC ambapo wasomi wa kiyahudi zaidi ya 70 walipokutanika alexandria nadhani kuandika agano la kale kuyoka kiebrania kwenda kigiriki na hivyo vitabu unavyovitetea mfano Enoch na Jubilee. kumbe utagundua pamoja na mavitabu mengi kuwepo enzi hizo za kale lakini sio yote yalipewa hadi za kuwa maandiko matakatifu. Kitu kingine historia ya wakristo ktk karne ya awali pia kuliibuka watu wengi kama alivyoahidi Paulo pale troa kuwa wataibuka mbwa mwitu wasiwahurumie, waliibuka watu wengi walifundisha mambo mengi yasiyofaa. na pia sidhani kama kila balua ilikuwa intended kuwa sehemu ya maandiko, hata wewe leo ukipata mafunuo kutoka kwa Mungu tutayapokea kwa kuyapima kama yanaumana na wenzakomwa kale waliovuviwa na kuyakubali ila haiayawi bibilia au sehemu ya bibilia bali maagizo tu ya Mungu kwetu yanayotufanya tumuamini zaidi yeye na mitume wake.
Nitajifunza zaidi na Inshallah mwenyezi Mungu akinipa neema nitapita kutia neno la ziada kwenye hoja mbalimbali.
3:kanisa unamaanisha nini mkuu? kuhusu Luther alikataa baadhi lkn baadae alivielewa akavijumuisha. Kuhusu apokrifa kwa katolīki licha ya kukataa vitabu vingine vingi, ni tamko la kidini la mtaguso wa Trent ndio lililohalalisha hizo apokrifa. Tena kutoa kemeo la kitisho '' anaethma'' kwavatayevipinga, wanaweza kukaa mitaguso mingine hata mtaguso wa '' hong kong'' wakavitoa japo wanasema yale makubaliano ya trent ni ''ex cathedra'' hayapingiki. hata jerome alipoandika vulgate ile kwa mujibu ya wananzuoni(kama nakosea utanirekebisha) alivitenga pembeni maana hata scholars wa kiyahudi hawakuvihesabu kama ni miongoni mwa vitabu vilivyovuviwa ila vinaelezea matukio halisi kihistoria. Hata KJV ilipoandikwa viliwekwa vikatengwa pembeni pia (apokrifa) wenda kwa manufaa hayohayo.
Wengine hasa catholic wanavikubali maana ndiko waliopatia mafundisho yao (Dogma) mengine ni kama nguzo ya kanisa, mfano ibada za wafu na wamakabayo. Hakuna tendo la ibada ya wafu nje ya wamakabayo kwenye vitabu vingine. Waandishi karibu wote wamekubaliana kuwa mtu akifa analala, na ibada za wafu zinaonekana kwa wapagani zaidi. Na sio salama kujenga fundisho kwenye kafungunkaboja ambako jakaungwi mkono na vyanzo vingine.
Binafsi na nawapendekezea wote wasome bibilia 66Books, inakila utetezi na Lengo la Mungu kutupa maneno yake liko uchi kabisa kama sio wazi kabisa.
Huko kwingine kusomwe kama kujiburudisha na kujua mambo ya pembeni ili kutanua ubongo na uelewa wa mambo ya nje ya bibilia ili uiamini zaidi na sio ili uwe muasi, mtukana Mungu, mtu aliyechanganyikiwa na kuishi bila matumaini ya Uzima wa milele kupitia Yesu.
KwA UFUPI
1: Hao wakkristo waliokitana miaka ya 300 AD sio watu wa kwanza kucompile maaandiko. Bali watu wa kwanza tukianza na agano la kale ni Ezra na Nehemia chini ya Uonhozi wa Mungu. Lkn pia Kwa Mujibu wa Muratori flagments za 1740 zilikutwa na almost vitabu vyote vya agano la jipya ambayo aliyevicompile ni mtu anayeitwa Pius askofu wa kanisa la kikristo huko rumi mwaka 150AD miongo karibu 15 kabla ya hao wa 300AD. Peshito Syriac nauo ikataja vitabu vingi tu vya agano jipya tunavyotumia sasa ikiwemo hadi ufunuo wa Yohana miaka mingi kabla ya hao wa 300AD , vimetajwa pia hadi na wakina polycap askofu wa efeso na anasaidikiwa alikuwa mwanafunzi wa yohana pia. ninachpfahamu limitation ya technology nayo ilichangia upatikanaji wa wakati mmoja wa maandishi ya watu zaidi ya 30 walioandika katika range ya miaka 1500, hivyo hata makusanyo lazima iwe process kureflect uhalisia. Na hii ni moja ya sababu ya mimi Kuamini bibilia. Haikushushwa ni maneno ya Mungu yaliyoandikwa na binadamu halisi kwa mazingira na ugumu wao halisi kwa lugha yetu rahisi binadamu kuelewa.
2:Bibilia ni ukuaji, sio dude lililodondoka kutoka mbinguni. Hata Baada ya Kutoka babeli Bibilia au maandiko ya wakati huo yalyokusanywa na Nehemia na Ezra hayakuwa bibilia tulionayo sasa, Vitabu vingine havikuwepo. Hata mwanahistoria Josephus anayaita hayo maandiko matakatifu ya enzi zake '' Against Apion'' na Yesu kayathibitisha pote katika kauli zake. Hakuwahi kuzunhumiza au kuquote cha Apokrifa wala pseudo.... wa'la enoch maana havikuwa sehemu ya maandiko matakatifu ya wayahudi ambayo Yesu alijifunza utotoni na ujanani.
3:Kingine kuhusu enoch na vingine kuwa quoted, nimejifunza uhalali na usahihi wa nani kamkopi nani ni debate kubwa.
Hata mtetezi mkuu wa hivyo vitabu humu jukwaani anaitwa Eiyar ukimbana anakwambia vimefichwa, mara viko sijui etjiopia, mara siwezi kukwambia kama ninacho au la, yaani vimekaa kinjamanjama ambapo vinaonyesha sio vya kuaminika. Hata wewe huwa unaibuka unasema kuna maneno ya Mungu yamefichwa sijui vatican na kuna wengine hudai yamefungiwa Medicci Library huko Florence Binafsi mkuu huwa siamini sana hizo sarakasi na usiti wa maandiko matakatifu. Haya Yaliyopo Yamekamilika,
mkuu nimetoa maoni ya jumlajumla unaweza ukaokota vipande vya dhahamu humo sina shaka.