Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Basi tusaidie kwanini kitabu cha Nabii Gadi hakipo kwenye biblia??? Kwanini kitabu cha Jasher na Enoko havipo katika Biblia??
Ni vema utambue kuwa Biblia tuliyonayo ni mkusanyiko wa Vitabu mbalimbali vya kiimani.

Pili, ni Vitabu vile ambavyo vilivyopatikana wakati wakiiandaa Biblia ndivyo vilivyounda Biblia, Vitabu vingine havikupatika na hivyo havikujumuishwa kwenye Biblia.

Tatu, kuna Vitabu vinasadikika kuwa vya kiimani vilivyodaiwa kuwa viingizwe kwenye Biblia lkn havikukidhi canonical rules kuijumuishwa kwenye Biblia maana vinaonekana viko tafauti kabisa na vinapingana vitabu vinginevyo. Mfano ni kinachodaiwa kuwa ni Injili ya Barnaba.

Vv
 
Biblia imequote kitabu cha Henoko na kitabu cha yashari sasa Yashari anasema misri ilipigwa na mapigo 15 sio 10 kama Biblia inavyosema

Pia inasema musa alikimbilia ethiopia na kuwa mfalme na sio huko midian kama biblia inavyodai

Pia inadai pharaoh hakufa kwenye bahari ila aliendelea kuishi ilihali zaburi kwenye biblia inasema pharaoh na jeshi lake waliteketea wote kwenye bahari

Sasa nikuhoji ww je kitabu hiki kukinzana na Biblia nikikiita cha kipagani nakosea?? Na kama sio cha kipagani je unakubaliana nacho ilihali kinaipinga Biblia wakati wote tunajua Mungu hawezi kujipinga mwenyewe

Karibu tueleweshane
Natumai unaongelea hicho kitabu, sio vyote!
 
Mkuu ww ulikataa vitabu nje ya Biblia sio vya kipagani ndio nmekuonyesha mifano ya hivyo viwili jinsi vilivyo kinzana so nataka kwanza ukubali je ni vya kipagani au lah?? Na kama umekubali unazungumziaje kitabu kitakatifu kuchukua reference ya vitabu vya kipagani?? Huu ndio mzizi wa hoja
 
Ni vema utambue kuwa Biblia tuliyonayo ni mkusanyiko wa Vitabu mbalimbali vya kiimani.

Pili, ni Vitabu vile ambavyo vilivyopatikana wakati wakiiandaa Biblia ndivyo vilivyounda Biblia, Vitabu vingine havikupatika na hivyo havikujumuishwa kwenye Biblia.

Tatu, kuna Vitabu vinasadikika kuwa vya kiimani vilivyodaiwa kuwa viingizwe kwenye Biblia lkn havikukidhi canonical rules kuijumuishwa kwenye Biblia maana vinaonekana viko tafauti kabisa na vinapingana vitabu vinginevyo. Mfano ni kinachodaiwa kuwa ni Injili ya Barnaba.

Vv
1. Vitabu vingapi?? Alikusanya nani?? Mbona kila kanisa lina vitabu vyake?? Nani yuko sahihi?? Kma namba zinakinzana iweje uviite vya kiimani ilihali tunajua Mungu hajipingi mwenyewe

2. Una maanisha Biblia haijakamilika? maana unadai kuna vitabu vya kiimani vilivyopotea? Je una maana neno la Mungu linaweza kupotea kama gazeti la uwazi tu??

3. Canonical rules ni zipi?? Kama zilikuwepo hizo rules kwanini namba ya vitabu inatofautiana?? To be specific unaongelea Biblia gani maana kila Biblia ina canonical rules zake!! hivyo kitabu A kinaweza kiwe halali Catholic ila kikawa haramu Anglican!
 
Mkuu ww ulikataa vitabu nje ya Biblia sio vya kipagani ndio nmekuonyesha mifano ya hivyo viwili jinsi vilivyo kinzana so nataka kwanza ukubali je ni vya kipagani au lah?? Na kama umekubali unazungumziaje kitabu kitakatifu kuchukua reference ya vitabu vya kipagani?? Huu ndio mzizi wa hoja
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66, viliunganishwa pamoja kwa kuangalia vitabu vyenye manufaa kwa watu wa Mungu, unataka vitabu vinavyoongelea "ushoga" wa Daudi(Kama unavyodai) ili ujifunze nini hapo? Vitabu vipo vingi sana zaidi ya hivyo 66 au 72, lakini havina mantiki ya kuwekwa kwenye Bible, hakuna cha kujifunza. Kuna wafalme, manabii na watu wengine wa kawaida, lakini ni kwamba hawakuandika kwa utashi wa kufundisha njia za wokovu; bali waliongelea historia(nyingne binafsi) na maanguko ya watu! Bila kufundisha matendo mema; kwanini kuhangaika navyo? Havina sense ya mafundisho kwa watu wa Mungu,
 
Wapi nimesema daudi alikuwa shoga unaweza ukaweka hapa hyo post??

Swali langu sio vitabu 66 au 72 nachouliza ni upi msimamo wako kwa Bible ambacho ni kitabu kitakatifu kuchukua reference kwenye vitabu ambavyo ni vya kipagani?? Hili ndio hoja yangu
 
1. Vitabu vingapi?? Alikusanya nani?? Mbona kila kanisa lina vitabu vyake?? Nani yuko sahihi?? Kma namba zinakinzana iweje uviite vya kiimani ilihali tunajua Mungu hajipingi mwenyewe

2. Una maanisha Biblia haijakamilika? maana unadai kuna vitabu vya kiimani vilivyopotea? Je una maana neno la Mungu linaweza kupotea kama gazeti la uwazi tu??

3. Canonical rules ni zipi?? Kama zilikuwepo hizo rules kwanini namba ya vitabu inatofautiana?? To be specific unaongelea Biblia gani maana kila Biblia ina canonical rules zake!! hivyo kitabu A kinaweza kiwe halali Catholic ila kikawa haramu Anglican!
Wakatoliki wana Biblia ya vitabu 72, Madhehebu ya Kiprotestanti wana Vitabu 66 (vingine kama Tobiti , Makabayo, Yoshua bin Sila na ambavyo Wakatoliki wanavitumia, Waprotestant hawavikubali kama havikidhi canonical rule yao). Hizo canonical rules naamini ni kanuni ya kukubaliana kwa maandiko ingawa kutoka Nabii mmoja hadi mwingine wamepishana kwa karne nyingi. Unaweza kutafuta zaidi mwenyewe.

Makanisa ambayo hayatumii au kukubali Biblia hiyo wanazo Biblia zao kama vile Mashahidi wa Yehova wanaotumia New Word Translation na madhebu mengine yanayohesabika kuwa cults eg Momorns, Unification church, Jehova Witnesses etc).

Biblia iliyopo imekamilika na inajitosheleza kwa mafundisho. Hata hivyo kuna baadhi ya Maandiko na Nyaraka zilipotea au hazijapatikana mfano Waraka wa Paulo kwa Walaodikia (Kolosai 4:16), Vitabu vya manabii kama Gadi nk.

Nashangaa kuwa unashangaa kuna vitabu vilipotea, ni kuwa hata hivyo vilivyokusanywa kwenye Biblia kuna kazi kubwa ilifanyika, manuscripts zilipatikana sehemu tofauti tofauti, kwa hiyo sio ajabu nyingine hazijapatikana na zilizopatikana zinathibitisha kuwa vipo vitabu vingine kama maandishi ya Nabii Gadi na Waraka kwa Walaodikia. Ikiwa vitapatikana na kufikia viwango vilivyopo kwenye canonical rules huenda vikaongezwa kwenye Biblia ingawa vilivyopatikana kama hivyo vinavyodaiwa kuwepo kama Injili ya Thomaso na Barnabas.

Vv
 
Ila mkuu dhambi ile ya daudi ambayo hata kwenye biblia iliandikwa tumeona pia adhabu aliyopewa Daudi na alikemewa juu ya hiyo dhambi ila hiyo dhambi nyingine sijaona Nabii gani alienda kumkemea na adhabu yake ilikua ipi?
Taja hizo dhambi ili tukufahamishe mahali pa kusoma.

Vv
 
. Ikiwa vitapatikana na kufikia viwango vilivyopo kwenye canonical rules

Vv
Ndio rules zipi hizo mkuu maana canonical rules zinafika mamia je ni za Tawahedo church... Za Eastern orthodox... Za Council of Nicaea,Trent au alexandria.... ?? Be specific unieleweshe mkuu.

Biblia iliyopo imekamilika na inajitosheleza kwa mafundisho.

Vv
Biblia ipi mkuu?? Ya vitabu 66 au 73 au 84 au 68?? Be specific na iliyojitosheleza ni ipi kiasi wengine waongeze vitabu na wengine wavipunguze.... Kama unashauri mtu kama mimi je nitumie ipi kati ya hizo??

Ubarikiwe
 
Wakatoliki wana Biblia ya vitabu 72, Madhehebu ya Kiprotestanti wana Vitabu 66 (vingine kama Tobiti , Makabayo, Yoshua bin Sila na ambavyo Wakatoliki wanavitumia, Waprotestant hawavikubali kama havikidhi canonical rule yao).
Vv
Canonical rule ya protestants ndio ipi hiyo?? Unaweza kutusaidia hapa?? Wakati Biblia inapitishwa kwa mara ya kwanza tokea AD 300+ kulikuwa na protestants?? Ila mbona kulikuwa na Biblia ya vitabu 66??

Embu tuwekane sawa hapo mkuu
 
Kwa mtazamo wa kimadhehebu ukiondoa cults, Wakatoliki wameongeza vitabu zaidi kutoka 66 hadi 72 wakati Waprotestant wamegoma kuvitambua vitabu vilivyoongezeka kwenye Biblia kutoka 66 hadi 72. Kwa historia uliyeweka kama ni sahihi, basi kuna vitabu vingine vilipatikana baadaye na Wakatoliki wakaona viingie kwenye Biblia wakati Waprotestanti wakavikataa.

Bila kujali authority ya vitabu vilivyopo, ukweli kuwa kuna vitabu havijulikani kuwa viko au haviko/kupotea, ikiwa vitapatikana utakuwa ni uamuzi wa kanisa vijumuishwe kwenye Biblia au Biblia ibaki kama ilivyo sasa.

Vv
 
Habari za jioni wana JF natumaini wote humu ni wazima.
View attachment 885770
Nlipokuwa naipitia uzi huu Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote! - JamiiForums

Mkuu Elungata aliibua hoja kuhusu Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja na nathan ila muanzisha uzi alipotaka ushahidi aliuwekea condition hii.

Baada ya kusoma hii comment nilisikitika sana na nilijiuliza sana kwamba inakuaje kila story ya watu waliotajwa kwenye bible watu wanataka reference kutoka ndani ya Biblia pekee as if Biblia imeandika kila kitu?? Kwanini tunapenda kujifunga akili kiasi hicho?

Baada ya kuona mentality hiyo imeanza kukua humu JF intelligence nikaona nilete mada jinsi Biblia yenyewe imetutuma tukasome vitabu vingine nje ya Biblia ili tuongeze ufahamu kuhusu baadhi ya watu na matukio ambayo Bibila yenyewe haikuandika yote kwa upana wake, hivyo nia ya uzi huu ni kwa wale waliojifunga kwenye kusoma maandiko pekee wabadilike na kuwa na fikra huru na kuruhusu maarifa kutoka kona zote kwa mithiri ya kujifunza zaidi na kupanua uelewa wa mambo.
View attachment 885772
Kwa kuanzia tu labda nitumie nafasi hii kumjibu mkuu wangu maishapopote kuwa hata biblia yenyewe inakiri kuwa maisha yote ya Daudi yameelezewa vizuri zaidi nje ya Biblia hivyo imetutuma tukasome vitabu hivyo mnavyoita vya kipagani ili tujifunze kwa ufanisi zaidi

1 NYAKATI 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.

Vitabu vilivyotajwa hapa ni Book of Gad the seer,Book of Nathan the prophet, Book of Samuel the seer (Sio samuel 1&2) ambavyo kwenye biblia havikuwekwa . Sasa kama Biblia inakiri kuwa sio kila story yake imeongelewa kwa upana wake katika biblia je kwanini siku hizi watu wakijengea hoja kuhusu personality za biblia mnalazimisha reference iwe ndani ya bible pekee??? Ina maana waandishi wa Biblia ni wajinga hadi watutume tukasome hivyo vitabu vingine ambavyo mnaviita vya kipagani??

MAANDIKO
Hapa chini nimeambatanisha vifungu vya Biblia hivyo ningeomba tuisome kwa makini kabla ya kuchangia hoja. Neno Tarehe kwenye maandiko haya kwa kiswahili rahisi inamaanisha Nyaraka/rekodi/kitabu au kwa kizungu book/journal/Annal.
View attachment 885773

1. Kitabu cha Yehu

2 Nyakati 20:34
34 Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

2. Kitabu cha Nabii Gadi muonaji/ Kitabu cha shemaya

2 Nyakati 13:22
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

2 Nyakati 12:15
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

1 Nyakati 29:29

3. Kitabu cha mfalme Ahasuero

Nehemiah 12:23
23 Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu

Pia kinatajwa Esther 10:2, 2:23, 6:1

4. Matendo ya Mfalme suleiman

1 wafalme 11:41
41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani (Book of Acts of Solomon)

5. Nyakati za wafalme wa Israel & Yuda

1 wafalme 14:19
19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.(chronichles of the kings of israel/Judah)

6. Kitabu cha Hozai

2 Nyakati 33:19
19 Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.

Hivi ni kwa uchache tu ila kuna vitabu vingine zaidi ya 20 vinatajwa kama reference point kwenye biblia ilihali havipo kwenye Biblia na wala havitambuliki na kanisa lakini leo hii akijengea mtu hoja anaonekana shetani!!
View attachment 885774

HITIMISHO
Baada ya uzi huu nisingetegemea tena kusikia wana JF wakitaka reference kutoka kwenye biblia pekee ilihali Biblia yenyewe inataka tukarefer kwenye vitabu vingine ambavyo vingi ni vya kipagani tu ili tupate uelewa zaidi ya watu muhimu kwenye bible.

However ningependa tujiulize maswali haya ili kupanua fikra zaidi

1. Kwanini vitabu hivi ambavyo Biblia inaturefer tukasome ili kuelewa baadhi ya matukio havikuwekwa kwenye biblia??

2. Na kama havikuwekwa kwa sababu yeyote ile je ina maana ni vya kipagani??

3. Na kama ni vya kipagani ni kwanini vimekuwa referred kwenye bible?

4. Kuna vitabu vingine ambavyo vimenakiliwa hapa ni halali kabisa katika kanisa la kale lakini kwa sasa viko categorized kama vitabu vilivyopotea.... Je nini hatma ya Biblia kama maneno ya Mungu ilihali yanaweza kupotea??

5. Na kama yamepotea je ina maana biblia haijakamilika sababu sehemu ya stori yake imepotea??

Naomba kuwasilisha

Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu

Kweli kabisa mkuu , hivyo vitabu wanavyodai vya kipagani ndvyo vimejaa maisha halisi kwa kirefu na upana zaidi kuhusu wahusika wote wa kwenye biblia.

Sikujua kama King Solomon alikua anatumia majini na Ndio waliokua wanampa utajiri , akili na nguvu za ajabu, kuna kitabu nilikisoma ( sipendi kukitaja jina ) kuhusu mfalme Suleiman , kimejaa mambo ya kishetani na ya kutisha , kinafundisha hadi mbinu ya kuyaita majini aliyokua akiyatumia suleman

Vile vile sikujua temple aliyoijenga Solomon Ndio msingi halisi wa Freemason .

Kuna siri nzito sana zimejaa kwenye maandishi, tujitahidi sana kusoma na vitabu vingine sio biblia pekee, ukitaka kuilewa biblia basi kasome vzur vitabu mnavyoviita vya kipagan

Warumi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vile vile sikujua temple aliyoijenga Solomon Ndio msingi halisi wa Freemason .

Sent from my iPhone using JamiiForums
Huu ni ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia..... Ukisoma hata Muongozo wa ibada za Scottish rite freemasonry degree ya 6 inahusisha kutafuta missing pieces kwenye hekalu la suleiman. Kwahiyo kuna patterns unatakiwa uzitafute kwenye ramani ya lile hekalu ambapo inahusisha kusafiri kiroho/kiakili hadi wakati ule hekalu linajengwa.

Ni ibada nzito sana na kwenye katiba yao inaongelewa vizuri sana ila ukileta huo mjadala humu unaweza onekana ni ibilisi fulani hivi maana watu wamemsoma kwa upande mmoja tu.
 
Mwenye Sikio na asikie, na mwenye kuelewa aelewe....

Mambo mengine tunayoyasoma yanatisha sana , mpaka kuna mambo mengine ukiyasoma wanakwambia ule kiapo kabisa kabla hujaendelea kusoma kuwa chochote utakachokisoma kitabaki kuwa siri yako mwenyewe usimwambie mtu.

Ila ipo siku wataelewa tu unachokisema, hata mimi nilikua kama wao , nikisoma mambo kama haya najisemea maajent wa shetan at work , ila kumbe nilikua nimejifunga kitanzi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huu ni ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia..... Ukisoma hata Muongozo wa ibada za Scottish rite freemasonry degree ya 6 inahusisha kutafuta missing pieces kwenye hekalu la suleiman. Kwahiyo kuna patterns unatakiwa uzitafute kwenye ramani ya lile hekalu ambapo inahusisha kusafiri kiroho/kiakili hadi wakati ule hekalu linajengwa.

Ni ibada nzito sana na kwenye katiba yao inaongelewa vizuri sana ila ukileta huo mjadala humu unaweza onekana ni ibilisi fulani hivi maana watu wamemsoma kwa upande mmoja tu.
Nilipata bahati ya kuingia pale Masonic lodge ,enzi za Mzee sir Andy Chande, ndani mule kuna vitabu /biblia, kimoja ni kitabu cha Seleman

MTC | 101|
 
Pambania maisha na uzima wako ,kulia na pumzi za marehemu wa kale ni somehow Cracked Interest
 
Habari za jioni wana JF natumaini wote humu ni wazima.
View attachment 885770
Nlipokuwa naipitia uzi huu Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote! - JamiiForums

Mkuu Elungata aliibua hoja kuhusu Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja na nathan ila muanzisha uzi alipotaka ushahidi aliuwekea condition hii.

Baada ya kusoma hii comment nilisikitika sana na nilijiuliza sana kwamba inakuaje kila story ya watu waliotajwa kwenye bible watu wanataka reference kutoka ndani ya Biblia pekee as if Biblia imeandika kila kitu?? Kwanini tunapenda kujifunga akili kiasi hicho?

Baada ya kuona mentality hiyo imeanza kukua humu JF intelligence nikaona nilete mada jinsi Biblia yenyewe imetutuma tukasome vitabu vingine nje ya Biblia ili tuongeze ufahamu kuhusu baadhi ya watu na matukio ambayo Bibila yenyewe haikuandika yote kwa upana wake, hivyo nia ya uzi huu ni kwa wale waliojifunga kwenye kusoma maandiko pekee wabadilike na kuwa na fikra huru na kuruhusu maarifa kutoka kona zote kwa mithiri ya kujifunza zaidi na kupanua uelewa wa mambo.
View attachment 885772
Kwa kuanzia tu labda nitumie nafasi hii kumjibu mkuu wangu maishapopote kuwa hata biblia yenyewe inakiri kuwa maisha yote ya Daudi yameelezewa vizuri zaidi nje ya Biblia hivyo imetutuma tukasome vitabu hivyo mnavyoita vya kipagani ili tujifunze kwa ufanisi zaidi

1 NYAKATI 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.

Vitabu vilivyotajwa hapa ni Book of Gad the seer,Book of Nathan the prophet, Book of Samuel the seer (Sio samuel 1&2) ambavyo kwenye biblia havikuwekwa . Sasa kama Biblia inakiri kuwa sio kila story yake imeongelewa kwa upana wake katika biblia je kwanini siku hizi watu wakijengea hoja kuhusu personality za biblia mnalazimisha reference iwe ndani ya bible pekee??? Ina maana waandishi wa Biblia ni wajinga hadi watutume tukasome hivyo vitabu vingine ambavyo mnaviita vya kipagani??

MAANDIKO
Hapa chini nimeambatanisha vifungu vya Biblia hivyo ningeomba tuisome kwa makini kabla ya kuchangia hoja. Neno Tarehe kwenye maandiko haya kwa kiswahili rahisi inamaanisha Nyaraka/rekodi/kitabu au kwa kizungu book/journal/Annal.
View attachment 885773

1. Kitabu cha Yehu

2 Nyakati 20:34
34 Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

2. Kitabu cha Nabii Gadi muonaji/ Kitabu cha shemaya

2 Nyakati 13:22
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

2 Nyakati 12:15
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

1 Nyakati 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.

3. Kitabu cha mfalme Ahasuero

Nehemiah 12:23
23 Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu

Pia kinatajwa Esther 10:2, 2:23, 6:1

4. Matendo ya Mfalme suleiman

1 wafalme 11:41
41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani (Book of Acts of Solomon)

5. Nyakati za wafalme wa Israel & Yuda

1 wafalme 14:19
19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.(chronichles of the kings of israel/Judah)

6. Kitabu cha Hozai

2 Nyakati 33:19
19 Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.

Hivi ni kwa uchache tu ila kuna vitabu vingine zaidi ya 20 vinatajwa kama reference point kwenye biblia ilihali havipo kwenye Biblia na wala havitambuliki na kanisa lakini leo hii akijengea mtu hoja anaonekana shetani!!
View attachment 885774

HITIMISHO
Baada ya uzi huu nisingetegemea tena kusikia wana JF wakitaka reference kutoka kwenye biblia pekee ilihali Biblia yenyewe inataka tukarefer kwenye vitabu vingine ambavyo vingi ni vya kipagani tu ili tupate uelewa zaidi ya watu muhimu kwenye bible.

However ningependa tujiulize maswali haya ili kupanua fikra zaidi

1. Kwanini vitabu hivi ambavyo Biblia inaturefer tukasome ili kuelewa baadhi ya matukio havikuwekwa kwenye biblia??

2. Na kama havikuwekwa kwa sababu yeyote ile je ina maana ni vya kipagani??

3. Na kama ni vya kipagani ni kwanini vimekuwa referred kwenye bible?

4. Kuna vitabu vingine ambavyo vimenakiliwa hapa ni halali kabisa katika kanisa la kale lakini kwa sasa viko categorized kama vitabu vilivyopotea.... Je nini hatma ya Biblia kama maneno ya Mungu ilihali yanaweza kupotea??

5. Na kama yamepotea je ina maana biblia haijakamilika sababu sehemu ya stori yake imepotea??

Naomba kuwasilisha

Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu
Mkuu Zitto junior kwa kuwa nimeona unayo Imani juu ya maandiko au biblia basi naomba nikukumbushe kuwa Kusoma kwingi kuna geuza akili . Tunahitaji Maarifa yanayoweza kutupa Uzima wa milele hilo tu mengine yanabaki kuwa mbwembwe

Hivi kwa mfano ukijua King David alikuwa na mahusiano hayo uliyoyasema na Yonathan je utataka kuhalalisha Ushoga ?

"Zamani zile za ujinga Mungu alijifanya Kama hazioni ,bali Sasa anawaagiza watu wote kill mahali watubu " Mdo 17:30
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwa maoni yako, kiini cha mjadala haikuwa ushoga wa Daudi bali nahalalisha kwamba reference za kihistoria kwa characters wa Biblia hazipatikani tu ndani ya Biblia ila pia nje ya Biblia,

Hivyo inapaswa wasoma Biblia wote wasome na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa ya masuala ya Biblia, mfano hatma ya Cain, utata wa Melchizedek, Mnara wa babeli n.k wameongelewa kwa undani katika kitabu cha Yashari lakini ukikifanya reference humu unaonekana mpagani ilihali Biblia hiyo imekinalili humo.

Yote kwa yote kuongeza maarifa na imani yetu sababu naweza kukuuliza swali mfano Biblia inaeleza kuanzia mwanzo 6 kuwa dunia ilichafuka kwa wanefili na hivyo gharika likaja. Lakini mara baada ya gharika ukifika mwanzo 14 utaona tena Wanefili/Warefai wamerudi. Sasa kama Nuhu pekee alipona hawa wanefili walirudije duniani ilihali kizazi chote duniani kilikufa???

Hili swali ukiweza kujibu kwa reference ya Biblia pekee basi nitaomba wana JF wote wapuuze huu uzi wangu.
 
Pambania maisha na uzima wako ,kulia na pumzi za marehemu wa kale ni somehow Cracked Interest
Hatuwezi kwenda mbele bila kujua tulipotoka..... Yaani huwezi amini tu kila kitu bila kuhoji. Naamini ukristo ni dini ya reasoning sio kufuata upepo tu. Kama wanaJF hatuoni faida ku-revisit history ili kuweka precedence kwenye imani yetu basi naweza kuelewa kwanni mitume na manabii wana wafuasi wengi vile wakiwauzia mafuta na sabuni za upako!!!
 
Back
Top Bottom