zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,037
- 28,685
Habari za jioni wana JF natumaini wote humu ni wazima.
Nlipokuwa naipitia uzi huu Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote! - JamiiForums
Mkuu Elungata aliibua hoja kuhusu Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja na nathan ila muanzisha uzi alipotaka ushahidi aliuwekea condition hii.
Baada ya kusoma hii comment nilisikitika sana na nilijiuliza sana kwamba inakuaje kila story ya watu waliotajwa kwenye bible watu wanataka reference kutoka ndani ya Biblia pekee as if Biblia imeandika kila kitu?? Kwanini tunapenda kujifunga akili kiasi hicho?
Baada ya kuona mentality hiyo imeanza kukua humu JF intelligence nikaona nilete mada jinsi Biblia yenyewe imetutuma tukasome vitabu vingine nje ya Biblia ili tuongeze ufahamu kuhusu baadhi ya watu na matukio ambayo Bibila yenyewe haikuandika yote kwa upana wake, hivyo nia ya uzi huu ni kwa wale waliojifunga kwenye kusoma maandiko pekee wabadilike na kuwa na fikra huru na kuruhusu maarifa kutoka kona zote kwa mithiri ya kujifunza zaidi na kupanua uelewa wa mambo.
Kwa kuanzia tu labda nitumie nafasi hii kumjibu mkuu wangu maishapopote kuwa hata biblia yenyewe inakiri kuwa maisha yote ya Daudi yameelezewa vizuri zaidi nje ya Biblia hivyo imetutuma tukasome vitabu hivyo mnavyoita vya kipagani ili tujifunze kwa ufanisi zaidi
1 NYAKATI 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.
Vitabu vilivyotajwa hapa ni Book of Gad the seer,Book of Nathan the prophet, Book of Samuel the seer (Sio samuel 1&2) ambavyo kwenye biblia havikuwekwa . Sasa kama Biblia inakiri kuwa sio kila story yake imeongelewa kwa upana wake katika biblia je kwanini siku hizi watu wakijengea hoja kuhusu personality za biblia mnalazimisha reference iwe ndani ya bible pekee??? Ina maana waandishi wa Biblia ni wajinga hadi watutume tukasome hivyo vitabu vingine ambavyo mnaviita vya kipagani??
MAANDIKO
Hapa chini nimeambatanisha vifungu vya Biblia hivyo ningeomba tuisome kwa makini kabla ya kuchangia hoja. Neno Tarehe kwenye maandiko haya kwa kiswahili rahisi inamaanisha Nyaraka/rekodi/kitabu au kwa kizungu book/journal/Annal.
1. Kitabu cha Yehu
2 Nyakati 20:34
34 Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.
2. Kitabu cha Nabii Gadi muonaji/ Kitabu cha shemaya
2 Nyakati 13:22
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.
2 Nyakati 12:15
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
1 Nyakati 29:29

3. Kitabu cha mfalme Ahasuero
Nehemiah 12:23
23 Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu
Pia kinatajwa Esther 10:2, 2:23, 6:1
4. Matendo ya Mfalme suleiman
1 wafalme 11:41
41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani (Book of Acts of Solomon)
5. Nyakati za wafalme wa Israel & Yuda
1 wafalme 14:19
19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.(chronichles of the kings of israel/Judah)
6. Kitabu cha Hozai
2 Nyakati 33:19
19 Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.
Hivi ni kwa uchache tu ila kuna vitabu vingine zaidi ya 20 vinatajwa kama reference point kwenye biblia ilihali havipo kwenye Biblia na wala havitambuliki na kanisa lakini leo hii akijengea mtu hoja anaonekana shetani!!
HITIMISHO
Baada ya uzi huu nisingetegemea tena kusikia wana JF wakitaka reference kutoka kwenye biblia pekee ilihali Biblia yenyewe inataka tukarefer kwenye vitabu vingine ambavyo vingi ni vya kipagani tu ili tupate uelewa zaidi ya watu muhimu kwenye bible.
However ningependa tujiulize maswali haya ili kupanua fikra zaidi
1. Kwanini vitabu hivi ambavyo Biblia inaturefer tukasome ili kuelewa baadhi ya matukio havikuwekwa kwenye biblia??
2. Na kama havikuwekwa kwa sababu yeyote ile je ina maana ni vya kipagani??
3. Na kama ni vya kipagani ni kwanini vimekuwa referred kwenye bible?
4. Kuna vitabu vingine ambavyo vimenakiliwa hapa ni halali kabisa katika kanisa la kale lakini kwa sasa viko categorized kama vitabu vilivyopotea.... Je nini hatma ya Biblia kama maneno ya Mungu ilihali yanaweza kupotea??
5. Na kama yamepotea je ina maana biblia haijakamilika sababu sehemu ya stori yake imepotea??
Naomba kuwasilisha
Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu

ntaleta maandiko hapa tuyachambue
sawa ila hakikisha hayo maandiko yanaongea unachosema,tukubaliane hakuna reference nje ya biblia!