Biashara ya Uchawi Tanzania

Pengine ingekuwa vema tungefahamu namna hii list ilivyopatikana. Otherwise suala la ushirikina kwangu linabaki zaidi kwa individuals wanaolifuatilia
 
Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.

Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa.

Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.

Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.

Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali.

Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari, kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja.

Wachawi wa Marekani na bara Ulaya wao hutumia sana usafiri wa fagio.
Dah!!!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
.
Yaani degree ya kwanza na ya pili inapatikana nchini ila hakuna chuo kikuu(university)? Hueleweki kabsaa!! Ni chuo gani kinatoa masters kisichokua kikuu?
P/se! Za mbayuwayu changanya na za kwako.
.

Mbayuwayu miaka ya 1970 alipomaliza shule ya msingi, alionekana ni kijana aliyekuwa na bidii sana katika masomo yake darasani. Wazazi wake Mbayuwayu waliona itafaa kijana wao pia akajua fani ya uganga, hivyo walimtafutia mtaalamu ambaye alianza kumfundisha elimu ya jadi ya ulozi.

Masomo aliyofundishwa na kuyaelewa vema ni jinsi ya kutengeneza majini, kuruka kwa ungo, kuchukuwa watu msukule na elimu ya nyota. Baada ya kuhitimu wazee walikutana kwenye mikutano ya wachawi usiku, Mbayuwayu naye alialikwa, alipongezwa sana kwa bidii aliyoonyesha kwenye masomo yake, na aliahidiwa tarehe ambayo atakabidhiwa cheti chake cha kuhitimu elimu ya ulozi.

Tarehe ilipofika waliruka kwa ungo hadi Kisiju, Mkuranga, walipofika eneo la shughuli walikuta wapo vijana wenzake wawili ambao nao walikuwa wapate vyeti. Muda ulipowadia wazee waliwaita na kuelekezwa waende kwenye chungu kilichokuwa kipo jikoni. Walipokaribia chungu, walikuta ndani kuna nyama iliyokuwa inachemshwa, walielekezwa kila mtu akate kipande cha nyama ya kila kiungo na waweke kwenye sahani, walipofungua chungu, wakangundua kuwa ile nyama haikuwa ya mnyama bali ni nyama ya binadamu.

Mbayuwayu bila kusita alitii amri ya wazee na akakata nyama za kila kiungo pamoja na supu yake, na kuanza kula. Wale vijana wawili walipogundua ile ni nyama ya binadamu waligoma kabisa kula, walilazimishwa na wazee lakini hawakukubali. Desturi za wachawi, damu na nyama za watu ni chakula cha kawaida, na ukishaingia kwenye ulozi unatakiwa uwe mtiifu na usitoe siri zao kwa mtu yeyote ambaye siyo mchawi.

Wale vijana kwa daraja la uchawi walilokuwa wamefikia na viapo walivyoapa, adhabu waliyostahiki ilikuwa ni kifo, ilishangaza kidogo wale wazee vigagula walifanya mambo yao haraka na wale vijana walianguka chini wakiwa maiti.

Wazee walimchukuwa Mbayuwayu usiku huohuo kwa usafiri wa ungo hadi makaburi ya Kinondoni, makaburi haya yapo karibu na baa ya Lang'ata ambapo wanazikwa Wakristo na Waislamu. Walikuta kaburi la Mkristo ambalo ni la siku kama tatu tangu marehemu azikwe. Wazee walifanya mambo yao ya kichawi na kaburi likafunguka, wakalipandisha juu jeneza, kisha wazee wakamwambia Mbayuwayu alivyunje kwa kulikanyaga kwa mguu wa kushoto. Jeneza lilipasuka na harufu ya kutisha ilitoka ndani, wale wazee walichukuwa kikombe kidogo kinachotumika kunywea kahawa mitaani, Wazee walimwambia Mbayuwayu achote majimaji yenye usaha toka ndani ya jeneza na anywe vikombe vitatu. Mbayuwayu bila ajizi wala kusita alitii amri, na kuchota ule usaha vikombe vitatu vilivyojaa na kunywa.

Mbayuwayu alibaki anashangaa, alifikiri cheti alichoahidiwa kupewa ni sawasawa na cheti alichopewa alipomaliza elimu ya shule ya msingi, kumbe cheti ni kulishwa vyakula ambavyo hatavisahau maishani mwake.

Baada ya hiyo karamu ya makaburini, wazee walimwambia Mbayuwayu, ajitayarishe kwani kesho yake watampeleka kumtambulisha kuzimu kwa mkuu, kupitia lango la kuzimu la Upanga ........................

Je kuzimu ni wapi?
Je unaweza kuingia kuzimu na kutoka?
Ni nini kilimpata Mbayuwayu hadi akaokoka?

Tafuta kanda ya DVD itwayo "Ushuhuda wa Mwisilamu (mchawi) Aliyeokoka"

Mkuu hiyo namba nne kuna siri gani hapo? Mbona viongozi sijawaona hapo maana nasikia nao ni wateja wakubwa wa uchawi.
Nakuunga mkono namba nne umewaonea kabisa.
1.VIONGOZI (WANASIASA) mabosi wa idara za serikali na ulinzi (wanajeshi+polisi) ndio vinara wa ndumba.
2.Wafanyabiashara( wa aina yeyote i.e wahindi, waarabu, weusi, chotara, mamalishe,machinga)+wasanii

Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.

kategori nyingine siwezi kuchangia sijui umetoa wapi data hizo??
Shinyanga, mwanza, Iringa hazipo hata kidogo???
No 4. umewaonea, hapo vinara ni wanasiasa
No 3. kinamama wa uswahilini
 
mh kama niliwahi fika vile kwenye hichi kijiji, ila kinaonekana hakina idadi kubwa ya wakazi, au na wenyewe wameogopa wakakimbia?
 
Mkuu, haya mambo yapo, hayo uliyoyaandika ni madogo, laiti macho yako ya ndani yangekuwa na uwezo wa kuona ulimwengu, ungeshangaa dunia ilivyojaa uchafu.

Kwa mfano sasa hivi wapo watu wengi sana barabarani ambao siyo binadamu kabisa, na wengi wameolewa na kuoa bila kujua. Yapo magari mengi yanatembea barabarani jijini sasa hivi yakitokea kuzimu, na mara nyingi yanapomaliza shughuli zao za uharibifu hutoweka, wananchi wanabaki kudai serikali ijenge matuta kupunguza ajali, mtajenga matuta hadi mtashindwa kutembea ndani ya barabara zenu wenyewe.
Inatisha.
Majimoto na wewe ni mchawi bila shaka. Nisamehe ucnishukie
 
Mbayuwayu miaka ya 1970 alipomaliza shule ya msingi, alionekana ni kijana aliyekuwa na bidii sana katika masomo yake darasani. Wazazi wake Mbayuwayu waliona itafaa kijana wao pia akajua fani ya uganga, hivyo walimtafutia mtaalamu ambaye alianza kumfundisha elimu ya jadi ya ulozi.

Masomo aliyofundishwa na kuyaelewa vema ni jinsi ya kutengeneza majini, kuruka kwa ungo, kuchukuwa watu msukule na elimu ya nyota. Baada ya kuhitimu wazee walikutana kwenye mikutano ya wachawi usiku, Mbayuwayu naye alialikwa, alipongezwa sana kwa bidii aliyoonyesha kwenye masomo yake, na aliahidiwa tarehe ambayo atakabidhiwa cheti chake cha kuhitimu elimu ya ulozi.

Tarehe ilipofika waliruka kwa ungo hadi Kisiju, Mkuranga, walipofika eneo la shughuli walikuta wapo vijana wenzake wawili ambao nao walikuwa wapate vyeti. Muda ulipowadia wazee waliwaita na kuelekezwa waende kwenye chungu kilichokuwa kipo jikoni. Walipokaribia chungu, walikuta ndani kuna nyama iliyokuwa inachemshwa, walielekezwa kila mtu akate kipande cha nyama ya kila kiungo na waweke kwenye sahani, walipofungua chungu, wakangundua kuwa ile nyama haikuwa ya mnyama bali ni nyama ya binadamu.

Mbayuwayu bila kusita alitii amri ya wazee na akakata nyama za kila kiungo pamoja na supu yake, na kuanza kula. Wale vijana wawili walipogundua ile ni nyama ya binadamu waligoma kabisa kula, walilazimishwa na wazee lakini hawakukubali. Desturi za wachawi, damu na nyama za watu ni chakula cha kawaida, na ukishaingia kwenye ulozi unatakiwa uwe mtiifu na usitoe siri zao kwa mtu yeyote ambaye siyo mchawi.

Wale vijana kwa daraja la uchawi walilokuwa wamefikia na viapo walivyoapa, adhabu waliyostahiki ilikuwa ni kifo, ilishangaza kidogo wale wazee vigagula walifanya mambo yao haraka na wale vijana walianguka chini wakiwa maiti.

Wazee walimchukuwa Mbayuwayu usiku huohuo kwa usafiri wa ungo hadi makaburi ya Kinondoni, makaburi haya yapo karibu na baa ya Lang'ata ambapo wanazikwa Wakristo na Waislamu. Walikuta kaburi la Mkristo ambalo ni la siku kama tatu tangu marehemu azikwe. Wazee walifanya mambo yao ya kichawi na kaburi likafunguka, wakalipandisha juu jeneza, kisha wazee wakamwambia Mbayuwayu alivyunje kwa kulikanyaga kwa mguu wa kushoto. Jeneza lilipasuka na harufu ya kutisha ilitoka ndani, wale wazee walichukuwa kikombe kidogo kinachotumika kunywea kahawa mitaani, Wazee walimwambia Mbayuwayu achote majimaji yenye usaha toka ndani ya jeneza na anywe vikombe vitatu. Mbayuwayu bila ajizi wala kusita alitii amri, na kuchota ule usaha vikombe vitatu vilivyojaa na kunywa.

Mbayuwayu alibaki anashangaa, alifikiri cheti alichoahidiwa kupewa ni sawasawa na cheti alichopewa alipomaliza elimu ya shule ya msingi, kumbe cheti ni kulishwa vyakula ambavyo hatavisahau maishani mwake.

Baada ya hiyo karamu ya makaburini, wazee walimwambia Mbayuwayu, ajitayarishe kwani kesho yake watampeleka kumtambulisha kuzimu kwa mkuu, kupitia lango la kuzimu la Upanga ........................

Je kuzimu ni wapi?
Je unaweza kuingia kuzimu na kutoka?
Ni nini kilimpata Mbayuwayu hadi akaokoka?

Tafuta kanda ya DVD itwayo "Ushuhuda wa Mwisilamu (mchawi) Aliyeokoka"

Mayuway = Majimoto?????
 
Viongozi ni wateja wazuri, lakini idadi yao siyo kubwa
Asante mkuu kwa statistics, ila nina maswali yananijia nikiangalia "analysis" yako

mbona hivi vitu havina ushahidi? we ulijuaje kama sio moja wao? ulitumia method gani (ao source ipi)?
mbona mikoa ya nguvu za kichawi haziambatani na mikoa wenye wachawi wengi? is it quantity vs quality?
Unamaana gani unaposema wateja wakuu? wenye kuomba huduma mara nyigi ao wenye kutoa pesa nyingi?
pia tunaomba ka percentage ka how category hizo zinaperform nchini (like kigoma 30%, linfi 40%, mtwara 2,5% etc)

embu tueleze!!!
 
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza

Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida

Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera

Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.

Hii data umeipataje?
 
Asante mkuu kwa statistics, ila nina maswali yananijia nikiangalia "analysis" yako

mbona hivi vitu havina ushahidi? we ulijuaje kama sio moja wao? ulitumia method gani (ao source ipi)?
mbona mikoa ya nguvu za kichawi haziambatani na mikoa wenye wachawi wengi? is it quantity vs quality?
Unamaana gani unaposema wateja wakuu? wenye kuomba huduma mara nyigi ao wenye kutoa pesa nyingi?
pia tunaomba ka percentage ka how category hizo zinaperform nchini (like kigoma 30%, linfi 40%, mtwara 2,5% etc)

embu tueleze!!!

Zindiko la taifa lililofanywa na wachawi wa mkoa wa Lindi, lilisababisha kusambaa kwa mapepo yaliyowafanya wananchi zaidi ya 75% kutokuwa na maamuzi yao wenyewe, au wawe wanaongozwa kwa remote control kutoka kuzimu, kwa maana kwamba watawala wakitaka uongozi au jambo lolote, hushuka kuzimu, na kutoa kafara ya damu, kisha hunuiza maneno ya jambo wanalotaka litendeke nchini, shetani wa kuzimu hutumia remote yake na watanzania waliopangawa na hayo mapepo uwezo wao wa maamuzi huondoka na kubaki watu wa kusema ndiyo,hata kama wanatukanwa.
 
Asante mkuu kwa statistics, ila nina maswali yananijia nikiangalia "analysis" yako

mbona hivi vitu havina ushahidi? we ulijuaje kama sio moja wao? ulitumia method gani (ao source ipi)?
mbona mikoa ya nguvu za kichawi haziambatani na mikoa wenye wachawi wengi? is it quantity vs quality?
Unamaana gani unaposema wateja wakuu? wenye kuomba huduma mara nyigi ao wenye kutoa pesa nyingi?
pia tunaomba ka percentage ka how category hizo zinaperform nchini (like kigoma 30%, linfi 40%, mtwara 2,5% etc)

embu tueleze!!!

Utawala wa shetani ni wa kificho sana. Shetani hutawala dunia kwa kufuata mipaka ya nchi kama zilivyo, kama tulivyo na mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, katibu tarafa, mwenyekiti wa kijiji, shetani naye amepanga utawala wake kwa mfumo huo huo.

Anachofanya shetani ni kuhakikisha kuwa viongozi tunaowachagua au wanaopewa madaraka ya kuongoza, wizara, mikoa, wilaya, tarafa, kijiji, kaya nk. ni wale tu waliopitia kwa mawakala wake, tunaoishi nao ambao ni waganga wa kishenzi (kienyeji).

Ndiyo maana basi shetani anapofanikiwa kuwa mtawala wa ulimwengu usioonekana na ulimwengu unaoonekana, kamwe maendeleo ya eneo hilo huwa yanadumaa kabisa, kwani shughuli kubwa kabisa ya shetani ni kuharibu, kutesa na kuua.

Kuhusu maswali yako .Wateja wakuu ni watu ambao asili yao siyo wachawi, lakini wanatumia uwezo wao wa mapato kununua huduma ya uchawi.

Mikoa yenye nguvu kubwa ya uchawi, wao wanaishi kwa kutegemea uchawi kwa asilimia 100, na utakuta uchumi wa maeneo hayo upo nyuma sana, kwa mfano mkoani Tanga mchawi mwenye misukule 200 anaonekana ni mtoto katika mambo ya ulozi, biashara ya misukule ni biashara ya kawaida, bei ya msukule kwa sasa hivi ni kati ya shs. 300,000 hadi 600,000 kutegemea na umri na nguvu ya msukule, Ndiyo maana maeneo hayo utakuta siku nzima watu wamefunga misuri na kucheza bao, lakini wanaishi vizuri tu.

Mikoa yenye wachawi wengi, tuseme ni kama mila au utamaduni au wanachukulia kama ulinzi wa familia, ndiyo maana utakuta kila kaya kuna mchawi au familia nzima wanaujua uchawi. Wananchi wa maeneo haya wengi wanafanya kazi halali na zenye kuingiza kipato halali kwao na kwa taifa.
 
Sasa hivi zipo shule kabisa za kufundisha uchawi nchini Tanzania, Shule moja ipo Temeke masomo yake huchukua miaka saba hadi unahitimu.

Ukimaliza Temeke, unaweza kujiunga na elimu ya juu katika fani ya uchawi, chuo kipo Tanga hapo wanatoa digrii ya kwanza ya uchawi kwa miaka mitano.

Wanatoa pia digrii ya pili ya elimu ya ulozi ambapo utakaa darasani kwa miaka mingine mitano.

Master digrii ya ulozi, bado hapa nchini hakuna chuo, inapidi uende Mombasa nchini Kenya ndipo kilipo chuo kikuu cha elimu ya ulozi.
nahisi sasa hekaya za abunuwasi zishaaanza kuingia.... kwamba kuna chuo cha kufundi U-Harry Porter?:coffee:
 
hakuna hekaya za abunuasi....hapa ukweli upo maana hata BIBLE inakiri uchawi upo....ila shetani anawapotezea kwa kijifanya muamini sayansi huku yeye akiendelea kutekeleza uchawi wake katika maisha ya watu....uchawi upo na unafanya kazi kama dunia inayoonekana inavyofanya kazi na bila YESU KRISTO jamaa wanakufaidi sana hawa
mix with yours
 
Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.

Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa.

Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.

Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.

Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali.

Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari, kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja.

Wachawi wa Marekani na bara Ulaya wao hutumia sana usafiri wa fagio.

Mkuu sina any doubt, Jina lako tu linaonesha kuwa unaongea ukweli..)
 
Mbayuwayu miaka ya 1970 alipomaliza shule ya msingi, alionekana ni kijana aliyekuwa na bidii sana katika masomo yake darasani. Wazazi wake Mbayuwayu waliona itafaa kijana wao pia akajua fani ya uganga, hivyo walimtafutia mtaalamu ambaye alianza kumfundisha elimu ya jadi ya ulozi.

Masomo aliyofundishwa na kuyaelewa vema ni jinsi ya kutengeneza majini, kuruka kwa ungo, kuchukuwa watu msukule na elimu ya nyota. Baada ya kuhitimu wazee walikutana kwenye mikutano ya wachawi usiku, Mbayuwayu naye alialikwa, alipongezwa sana kwa bidii aliyoonyesha kwenye masomo yake, na aliahidiwa tarehe ambayo atakabidhiwa cheti chake cha kuhitimu elimu ya ulozi.

Tarehe ilipofika waliruka kwa ungo hadi Kisiju, Mkuranga, walipofika eneo la shughuli walikuta wapo vijana wenzake wawili ambao nao walikuwa wapate vyeti. Muda ulipowadia wazee waliwaita na kuelekezwa waende kwenye chungu kilichokuwa kipo jikoni. Walipokaribia chungu, walikuta ndani kuna nyama iliyokuwa inachemshwa, walielekezwa kila mtu akate kipande cha nyama ya kila kiungo na waweke kwenye sahani, walipofungua chungu, wakangundua kuwa ile nyama haikuwa ya mnyama bali ni nyama ya binadamu.

Mbayuwayu bila kusita alitii amri ya wazee na akakata nyama za kila kiungo pamoja na supu yake, na kuanza kula. Wale vijana wawili walipogundua ile ni nyama ya binadamu waligoma kabisa kula, walilazimishwa na wazee lakini hawakukubali. Desturi za wachawi, damu na nyama za watu ni chakula cha kawaida, na ukishaingia kwenye ulozi unatakiwa uwe mtiifu na usitoe siri zao kwa mtu yeyote ambaye siyo mchawi.

Wale vijana kwa daraja la uchawi walilokuwa wamefikia na viapo walivyoapa, adhabu waliyostahiki ilikuwa ni kifo, ilishangaza kidogo wale wazee vigagula walifanya mambo yao haraka na wale vijana walianguka chini wakiwa maiti.

Wazee walimchukuwa Mbayuwayu usiku huohuo kwa usafiri wa ungo hadi makaburi ya Kinondoni, makaburi haya yapo karibu na baa ya Lang'ata ambapo wanazikwa Wakristo na Waislamu. Walikuta kaburi la Mkristo ambalo ni la siku kama tatu tangu marehemu azikwe. Wazee walifanya mambo yao ya kichawi na kaburi likafunguka, wakalipandisha juu jeneza, kisha wazee wakamwambia Mbayuwayu alivyunje kwa kulikanyaga kwa mguu wa kushoto. Jeneza lilipasuka na harufu ya kutisha ilitoka ndani, wale wazee walichukuwa kikombe kidogo kinachotumika kunywea kahawa mitaani, Wazee walimwambia Mbayuwayu achote majimaji yenye usaha toka ndani ya jeneza na anywe vikombe vitatu. Mbayuwayu bila ajizi wala kusita alitii amri, na kuchota ule usaha vikombe vitatu vilivyojaa na kunywa.

Mbayuwayu alibaki anashangaa, alifikiri cheti alichoahidiwa kupewa ni sawasawa na cheti alichopewa alipomaliza elimu ya shule ya msingi, kumbe cheti ni kulishwa vyakula ambavyo hatavisahau maishani mwake.

Baada ya hiyo karamu ya makaburini, wazee walimwambia Mbayuwayu, ajitayarishe kwani kesho yake watampeleka kumtambulisha kuzimu kwa mkuu, kupitia lango la kuzimu la Upanga ........................

Je kuzimu ni wapi?
Je unaweza kuingia kuzimu na kutoka?
Ni nini kilimpata Mbayuwayu hadi akaokoka?

Tafuta kanda ya DVD itwayo "Ushuhuda wa Mwisilamu (mchawi) Aliyeokoka"

Mkuu hiyo DVD nitaipataje? inapatikana wapi hasa?
 
Back
Top Bottom