MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Biashara ya wanadamu ni kubwa sana inayofanyika katika ulimwengu usioonekana. Vijana na watoto ndio walegwa wakuu katika soko hili haramu.
Watu wengi wamekuwa wakijifariji kwa maneno kama "kazi ya Mungu haina makosa", " Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe" , "RIP (Rest in Peace) n.k.
Kwanza ieleweke wazi kuwa MUNGU kamwe hajawahi na hatawahi kuumba au kutengeneza kitu kinachoitwa ugonjwa wa aina yoyote ile kwa ajili ya mwanadamu, narudia hajawahi kabisa kufanya hivyo.
Zipo aina nne, wachawi wa nchi wanazotumia kuhamisha watu kutoka ulimwengu unaoonekana kwenda ulimwengu usioonekana.
1. Utasikia maumivu makali sana ya kuumwa kichwa, sehemu ya mbele ya paja la uso na baada muda mfupi sana utasikia mtu amefariki.
Kinachofanyika ni kuwa, wachawi wanakutumia jini linaingia ndani ya mwili wako, kisha jini linailaza roho yako, na mtu huyo huonekana amekufa, baada ya mazishi, wachawi usiku hufukua kaburi na kukutoa, wanakupulizia dawa za kichawi na lile jini lililoikaba roho yako huachia na kuzinduka. Kisha unaambiwa ukimbie kuelekea pande nne za dunia, baadaye wanakupulizia dawa nyingine ya kukupumbaza na kuondoka na wewe.
2. Usiku utasikia unaitwa jina lako, ukiwa umelala, unapoitika unawafuata hao wachawi waliokuita ukiwa mzima mzima.Ndugu wanabaki kukutafuta polisi, mahospitalini, matangazo kwenye tv na kila mahali lakini kamwe hawatakupata tena.
3. Wachawi wanatengeneza dawa na kukuona ndani ya kioo au TV ya kichawi, kisha huanza kuzungumza na wewe kirafiki wakikumbembeleza sana uonane nao, ukikubali utawafuata mwenyewe popote pale walipo kwa kutembea kwa miguu. Ukifika unakaribishwa, wanakupulizia dawa za kichawi kuondoa ufahamu wako, kisha wanakuvua nguo zote. Kuna dawa wanayokupaka mwili wako mzima kuazia kichwani kwenye nywele hadi chini ya nyayo za miguu, ni lazima dawa hiyo ifunike mwili wako wote, unapotembea nje watu hawakuoni kabisa lakini wewe unawaona.
Kisha huita pepo na kulivika zile nguo zako walizokuvua, lile pepo huchukua sura na umbo lako kabisa, pepo linafanana na wewe kama mapacha. Kisha huliachia hilo pepo na kurudi kule nyumbani kwako ulikotoka, pepo likifika huanza kusingizia ugonjwa, ndugu wanaanza kazi ya kukuuguza, kawaida hilo pepo muda wake wa kuishi ni siku saba tu. Lakini wachawi wanaweza kuliongezea muda ili pesa yenu iendelee kupotea mkiuguza pepo.
4. Wachawi wanachukua roho ya mtu na mwili wake unabaki ukiwa hai.
Wachawi hupendelea sana aina hii ya kuchukua watu, nitajaribu kuelezea nini kinafanyika, na naamini kabisa maelezo nitakayotoa huenda katika familia au watu unaowajua yupo mtu mwenye dalili hizi.
a) Unaweza ukawa na mtoto na anasoma shule na maendeleo yake shuleni ni mazuri sana, siku moja akiwa anarudi nyumbani mtoto akaanguka chini ghafula, baadaye akazinduka na kuamka na akarudi nyumbani, lakini akarudi akijisikia vibaya au anaumwa. Mtoto akatibiwa na kupona kabisa. Lakini baadaye utaona tabia ya mtoto inaanza kubadilika sana, anakuwa mjeuri, maendeleo yake shuleni yanakuwa mabaya, anakuwa mtu wa kusahau na anakuwa ni mtu wa kukumbushwa kila kitu. Mbaya zaidi anapokuwa ni mtoto wa kike wazazi wanahisi mtoto wao kaanza tabia mbaya ya umalaya n.k.
b) Kumetokea kifo katika familia yenu, labda baba amefariki.
Wakati wa kuaga maiti kaka au dada mkubwa au ndugu yeyote anaaguka na kupoteza fahamu, anahudumiwa na anazinduka, lakini akiwa bado katika hali ya maumivu na kuchanganyikiwa na anakuwa amesahau mambo mengi.Siku zinapoendelea hali yake ya afya nayo inazidi kuzorota, anakuwa ni mtu wa kulala kitandani muda wote. Ndugu na marafiki wanaishia kusema kaka yetu kweli alimpenda baba, kiasi kwamba baba alipokufa tu ndiyo siku alianza kuchanganyikwa.
Wachawi wa nchi wanapokusudia kumchukua mtu kwa staili hii, hujitokeza katika hali ya kutokuonekana na watu wengine lakini mhusika huwaona na humpulizia dawa inayoondoa ufahamu wake na ananguka chini, anapoanguka wachawi huchomoa roho yake ndani ya mwili wake, na kwa sababu mwili bila roho hauwezi kuishi, huchukua pepo na kuliingiza ndani ya mwili kisha humpulizia dawa nyingine ya kumzindua.
Pepo aliyeingizwa ndani ya mwili anakuwa hajui chochote alichokuwa akifanya huyo mtu kabla, pepo huanza kujifunza kuishi maisha ya kibinadamu, ndiyo maana kama ni mwanafunzi husahau kila kitu, husahau hata chumba gani alikuwa analala, na magonjwa kwa huyo mtu huwa hayaishi.