Ni aibu kwa Dodoma na Kagera kuwa kwenye list ya mikoa 10 maskini zaidi Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Kwa wale ambao mlikuwa hamjui basi hiyo ndio taarifa kamili.

Pamoja na sifa za watu wa Kagera na Serikali kuweka Nguvu kubwa Dodoma ila Bado haijasaidia kuitoa Mikoa hiyo kuwa kwenye orodha ya Mikoa yenye watu maskini wengi ambao Wana kipato duni kabisa yaani mafukara.

Kwa mujibu wa Takwimu kutoka BoT, Jumla ya Mikoa 14 Ina kipato ambacho Kiko chini ya wastani wa kitaifa wa Milioni 2.8(Dola 2) Kwa mwaka sawa na Dola 3 Kwa siku.

Lakini Mikoa 10 yenye Hali mbaya zaidi (poorest Regions) ni hii ifuatavyo:

1. Simiyu
2. Kagera
3. Singida
4. Pwani
5. Dodoma
6. Tabora
7. Kigoma
8. Katavi
9. Songwe
10. Rukwa

My Take:
Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Katavi, Songwe na Rukwa Iko kwenye list kwa bahati mbaya tuu Kwa sababu ni Mikoa mipya ila mwaka ujao itakuwa imejiondoa kwenye List of shame.

View: https://twitter.com/NuktaTanzania/status/1712367469963145246?t=3-tfd4WrURVl12v3zQHtyQ&s=19
 
Mkoa wa Pwani halali kuwa masikini wa kutupwa sababu elimu duni na uvivu uliopitiliza.
Washukuru viwanda vipo bingo, wao ni watu wa kuuza ardhi tu.
 
Kwa hiyo Lindi na Mtwara ni mikoa tajiri hizo takwimu za kisiasa hizi
Unadhani Lindi na Mtwara Kuna maskini kama huko Kagera? Uliwahi ona wapi maskini analima.korosho,mbaazi ,ufuta,Uvuvi nk?

Endelea kukariri hivyo hivyo
 
Kagera kuna ardhi nzuri, Ziwa Victoria, ndizi, vanilla na kahawa sijui wanakwama wapi!
Ndizi tangu zimekumbwa na magonjwa uliwahi sikia serikali imepeleka wataalamu kupambana nayo? Kwanza kuzisafirisha ni mtiti ukizubaa kidogo zimeiva.

Vanilla ungejua bei yake kwa kilo. Gharama ya kuhudumia ni kubwa kuliko faida ya mauzo. Tanzania nzima hakuna zao pasua kichwa kama hilo, mwaka huu kilo inauzwa laki moja kisa wakulima wameng'oa miche. Miaka miwili baadae kilo inakuwa elfu 10, mwaka kesho yake hakuna mnunuaji mazao yanaharibika shambani. Wapi uliwahi sikia mchele umeuzwa 2000 kwa kilo na mwakani ukauzwa 200 na mwakani ukakosa mteja?

Kahawa hivyohivyo kama vanilla. Kilo mara elfu mbili, mara elfu tatu mara elfu moja. Hela ndogo ndogo tu. Uganda hawana bandari ila kahawa kwao always bei huwa ni mara mbili zaidi ya Tanzania. Na vanilla kwao ni mara mbili vilevile. Kusafirisha hayo mazao kuna urasimu mkubwa sana na vizuizi vya kutosha. Magendo hayatoshi kukamilisha soko na mpaka wa Uganda sio wide kama mpaka wa Kenya.

Lini uliwahi ona serikali imepeleka uko viuatilifu, mbolea ya ruzuku, mikopo ya trekta na power tiller? Hayo mambo si kuna mikoa yake ndio hupewa.

How do you expect Kigoma, Lindi, Kagera na Kigoma kuendelea wakati serikali haitaki na kila option ya unafuu iliyojitokeza inadidimizwa?

Hii nchi kuna mikoa haipendwi na serikali. Hali ikiendelea hivi utasikia watu wanataka kujitenga. Kila mkoa unaoona ni maskini serikali imeamua, kila mkoa tajiri serikali imeamua. Pwani kuna nini cha kuifanya ipendelewe kila kitu.
Serikali ikiamua kuiua Mtwara inaleta siasa kwenye korosho, kilo inauzwa buku na hamna kitu mtafanya, marufuku kusafirisha kwa gari, marufuku kupeleka nje bila kibali (wenye vibali ni makada). Mbaazi kilo 400 kama kipindi cha Magu mwanzoni, ufuta ni vita tu mara usinunuliwe mara ushuke bei mara kumi. Hapo sasa mkoa kwisha habari yao. Hiyo multiplier effect itagusa kila kitu mkoa huo.
 
Mama amedhamiria kubadili historia ya Kagera.

Kahama 👇

View: https://www.instagram.com/p/CyRZrRZNjEy/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Kwa hiyo kilimo korosho mbaazi na ufuta kimeanza mwaka huu??
Vimepewa msukumo na Serikali awamu ya 6 Kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani na pembejeo za Bure plus soko hivyo wakulima Wana uhakika.

Usisahau kwamba hiyo Mikoa Iko very untapped and so watu wanakimbilia huko kufanya uwekezaji.
 
Unapima utajiri kwa Kipato; Vipi Matumizi ya Sehemu Husika ?

Unaweza ukawa UK unakula takribani Laki Tisa kwa Wiki lakini hapo inabidi ulipie gesi, na kodi ya nyumba (kijumba) ni robo tatu ya pato lako..., alafu unajiona tajiri kuliko mdau aliyepo huko Kijijini anaingiza elfu kumi kwa mwezi lakini hata elfu tano hamalizi na hapo Bata anakula na ku-enjoy maisha kuliko mtu anayefukuzana na muda huko UK....

Inabidi ujiulize Utajiri ni nini na vipi unapimwa (sababu kuupima kwa dola ngapi kwa siku ni kupotoka)

By the way hivi Kagera wanalisha watu kiasi gani kwa Matoke ? Badala ya kuona ni kiasi gani wanawapa Walamba Asali (Mchwa wa Serikali ambao hakuna Value for Money) tuangalie ni kiasi gani wanatuweka mjini....
 
Mbona huna argument kwann dodoma na kagera hazikupaswa kuwa mikoa maskini
Jibu hoja yangu harafu uulize swali lako.

Toka mumejikwamua kwenye List of shame ya umaskini mumeanza kusumbua sana 😁😁
 
Back
Top Bottom