Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Ndugu zangu,

Ninafanya biashara ya kuchezesha games (ps2, ps3 na ps4) kwa siku za shule nimekuwa nafungua saa 9 jioni, kipindi hiki cha likizohuwa nafungua asubuhi saa 4 lakini muda wa saa 9 kasoro. Askari wakanikamata katika kipindi hiki cha likizo, wanadai muda bado.

Naomba kujua utaratibu ukoje, maana wanafunzi sasa hivi wapo majumbani

Asanteni
Mkuu hapo kuna faida kweli kama unafungua jioni??
 
nimepitapita mitandaoni kuona bei ya hizi PS kuna kitu nimegundua, bei ya Tz ipo juu sana ukilinganisha na bei ya kenya sijui shida ni nini mpaka bei ya kwetu inakiwa juu karibia mara mbili ya bei ya kenya. PS4 mpya ile slim ya 500Gb kenya inauzwa around 400k - 500k Tshs, huku kwetu wanauza zaidi ya 750k
 
Ndugu zangu vipi hii biashara na kununua bodaboda ipi itakuwa na tija naombeni mrejesho wakuu?
 
Ndugu zangu vipi hii biashara na kununua bodaboda ipi itakuwa na tija naombeni mrejesho wakuu?
Ps 3 ukipata eneo zuri ni bora zaidi ya bodaboda......rafiki angu ana PS 3 mbili tu...analaza 15-20 kilasiku siku chache anapata 10-12-13 Hivo biashara ikigoma sana anapata 10 hadi 9 napo ni siku mojamoja sana......

Kwenye bodaboda je unaendesha wewe mwenyewe kama unaendesha mwenyewe basi ujue unaweza kulaza 15-20 inategemea na ulipo, pia ukipata safari ya maana unaweza laza hata 40 kwa siku plus mizigo inatoa pesa kias.....

Ila kama hauemdeshi wewe hiyo bodaboda basi mikataba huwa ni 7000/= kwa siku unaletewa na chombo itabaki kuwa ya kwako....wengine ni 10000/= kilasiku ila mwisho wa mwaka chombo inakuwa ya utingo.....

but PS 3 haina risky sana kama ajali, wizi japo wizi nazo zinaibiwa vizuri tu ila ni biashara isiyosumbua sana ukifanya smart na kupata kijana smart..... Castr kaka unaweza ongezea
 
tafuta eneo lemye msongamano tena uswazi uswazi mkuu uweke hizo games....ujue wanaoenda games gan yami mpira, magari, mission ziwepo....

Pia bei yako iwe rafiki
Nna mpango niweke ps3 1 na ps2 1 uku weng bado wanatumia ps2 saaan niko pwan ushaur wakuu
 
Back
Top Bottom