Je, biashara ya gaming lounge bado ni nzuri kwa mwaka 2023-24?

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Habari wana-JF! Nipo na 5m ambayo nafikiria kuwekeza kwenye biashara. Nimepitia mawazo mengi ya biashara ila gaming lounge naona ni biashara nzuri kuanza kwa mtaji nilionao.

Faida ya eneo nilipo ni karibu na chuo, kama tunavyojua vyuoni wengi ni vijana ambao kwa % kubwa wanafuatilia mpira wa miguu hivyo huwa na interest ya kucheza video games kama FIFA n.k.

Nimeona ni eneo zuri kuweka biashara hii ila nikaona ni vyema kuja hapa kupata maoni kwa kile ninachokiwaza kutoka kwa watu ambao wameshafanya hiyo biashara au wanaijua. Binafsi nimeshafika gaming lounge nyingi kama gamer tu na siyo kwa lengo la kuijua biashara hiyo.

Kama wazo hili litakuwa ni zuri nafikiria kuanza na PS4 Slim (2), PS5 (1) & HDtv (3). Kwasababu sitatumia UHDtv au 4Ktv naona sitahitaji PS4 Pro ila PS5 ni nzuri ili kuwa na latest console. Baada ya biashara kukaa vizuri ndiyo naweza kuongeza console ya Xbox.
 
In biashara nzuri kama ukipata sehemu yenye mzunguko mzuri wa watu. Ila isiwe ndo biashara pekee unayoitegemea maana kuna muda flow ya wateja inapungua.

Ushauri , usiweke games peke yake jaribu kuchanganya na vitu vingine , Mfano weka na movie library itakusaidia kuvutia wateja na pia utakula kote kote.
mwenyewe nafanya movie library na nyuma nimewka ps games, 30k - 50k kwa siku ni kawaida.
 
Back
Top Bottom