Je, kwenye Biashara hizi uendeshaji na faida vinapatikanaje?

Aigle

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
711
6,186
Leo tuziangalie hizi biashara tupeane mawili matatu kwenye angle hii ya

Uwekezaji, kwamba mtaji wa kiasi gani unahitajika ili kufaidi faida kubwa

Uendeshwaji wake

Faida zinapatikanaje

Biashara hizo ni

Sheli ya mafuta

Kampuni ya MADINI

Karibuni kwa michango.
 
Mtaji wa kias gani unahitajika kwa mtu anayetaka kuingia kwenye biashara hii bila ya kujaribujaribu
Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga. Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi. Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.

Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg. Kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fika 10- 15 millioni, inategemea ukubwa wa kituo.

Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18 millioni.

Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni.

Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo, moja ni 34 millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni.

Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni. Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta, pamoja na kuchimba mfereji wa kupitisha Mafuta 3 millioni.

Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5 millioni. Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.

NB: Hizi ni gharama Kwa kituo standard, ila kama ukiamua kubana kwa maeneo ya vijijini unaweza punguza gharama kidogo.
 
Mtaji wa kias gani unahitajika kwa mtu anayetaka kuingia kwenye biashara hii bila ya kujaribujaribu
Mtaji umegawanyika sehemu mbili Kwa mtu anayeanza.
1. Gharama za kununua kiwanja na gharama za ujenzi.
2. Mtaji wa kuendesha kituo Cha Mafuta, ununuzi wa Mafuta kutoka depot kwenye makampuni makubwa,
Hapa unaweza agiza Mafuta kutokana Hela ulizonazo, mfano Ltrs 15000 or Yale magari ya Ltrs 36000 ukachanganya kwenye gari Moja petrol na diesel, kutokana na eneo husika ukaangalia kipi kinakwenda faster mfano petrol 20000ltrs na disiel 16000 Ltrs.

Ukisha Jenga kituo Cha Mafuta kazi inayobaki sio ngumu sana, haya makampuni makubwa huwa wanakopesha Mafuta Kwa wauzaji wa rejareja, sana sana watataka bank guarantee Eli wawe Wana supply Mafuta kwako. Kigumu ni kwenye kupata site nzuri na vibali, maana hata ujenzi unaweza pata mkopo bank.
Pia Serikali wanatoa mikopo ya ujenzi wa vituo vidogo vijijini.
 
Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga . Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi,
Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC , Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.
Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fikka 10- 15mullioni, inategemea ukubwa wa kituo,
Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18millioni.
Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni ,
Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo Moja ni 34millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni,
Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni.
Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta , pamoja na kuchimba mfeteji wa kupitisha Mafuta 3millioni
Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5nillioni.
Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.
NB: hizi ni gharama Kwa kituo standard , ila kama ukiamua kubana Kwa maeneo ya vinijini unaweza punguza gharama kidogo
Umerahisisha ufafanuz mkuu, asante..

Unaweza nielezea kwenye faida inavyopatikana
 
Faida ya Mafuta ni zaidi ya Tshs 120 Kwa Ltrs , hapo Bado hujampata punguzo kwenye manunuzi , inaweza pewa punguzo kuanzia Tshs 30 Hadi 50 Kwa Ltrs.
Fanya umepata Faida Kwa Kila Ltrs Tshs 120.
Chukulia mauzo yako ni Ltrs laki mbili Kwa mwezi , Kwa siku wastani wa Ltrs 6800. Unazidisha lites 200,000 mara Tshs 120 = 24,000,000/.
Umeme ,wa Tsh 250,000/
Wafanyakazi manager/ supervisor laki Tano.
Pump attendant 4 mara 200,000= 800,000/
Walinzi wawili =300,000/
Mtu wa usafi chooni na mazingira mengine 150,000/
TRA / Halimashauri service levy Haezidi 1,000,00. Kwa miezi mitatu
Lile punguzo unalipewa kule Kwa wauzaji wa jumla na wewe una wapa wateja wako Eli uongeze mauzo.
NB; Faida ipo kwenye mauzo, unapouza zaidi ndio unapata Faida kubwa, lazima uwe sales oriented person, lazima u focus kwenye kuongeza mauzo.
Ukipata location nzuri na team nzuri ya wafanyakazi unaweza uza more than 10,000 Ltrs per day Ukienda Kwa mwezi ni more than 300,000 Ltrs wewe unazidisha na margin profit yako
 
Nakuomba pm.
 
Umerahisisha ufafanuz mkuu, asante..

Unaweza nielezea kwenye faida inavyopatikana
Bei za kununulia Mafuta Depot Kwa wauzaji wa jumla bandari ya Dar es salaam
Petrol Kwa Ltrs Moja Tshs 2952.48 na
Disiel Kwa Ltrs Moja Tshs 2946.09.
Hizo ndio Bei rasmi bila punguzo , ukiongea nao wanakupa punguzo.
Ukitaka kujua Faida Kwa Ltrs Moja unachukua Bei ya kuuzia kwenye vituo vya mtani kwako una toa na hiyo Bei ya kununulia kutoka Kwa wauzaji wa Jumla.
NB; Kuna issue za usafirishaji ambazo huwa kama ifuatavyo kupeleka Mafuta Mwanza gharama zake ni Tshs 100-120 Kwa Ltrs na Mbeya na Tunduma Bei ni hiyo hiyo . Ndio maana Bei Zina tofautiana Kila mkoa ama Kanda Kwa sababu ya issue za usafiri. EWURA wanatoa Bei mpya Kila jumatano ya mwanzo wa Mwezi, wao hitoa Bei elekezi Kwa Nchi nzima
 
Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga . Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi,
Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC , Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.
Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fikka 10- 15mullioni, inategemea ukubwa wa kituo,
Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18millioni.
Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni ,
Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo Moja ni 34millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni,
Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni.
Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta , pamoja na kuchimba mfeteji wa kupitisha Mafuta 3millioni
Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5nillioni.
Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.
NB: hizi ni gharama Kwa kituo standard , ila kama ukiamua kubana Kwa maeneo ya vinijini unaweza punguza gharama kidogo
Kuna sehem hawa wenye shell za meru wamemuhamisha mtu alikuwa road kwa mil 800 cash aise na eneo ni la kawaida sema ni potential kwa business ya shell just imagine mtu ananunua eneo tu kwa mil 800 bado hajaanza construction na mambo mengine so mtaji ni mrefu mno
 
Meru, Olympic, Petroafrica, ATN, ADMIRE, GUDAL, Lake oil, Camel, GBP, Rawakal, Panone, ,Hao ni wakubwa kwenye Hii industry hata maeneo wanayonunuwa ni kwaajili ya uzaji mkubwa, Wana oder za Malori ya teansit, Malori ya local, Mabasi, minara ya simu, Mashirika mbalimbali , migodibi na ma contractors wa barabara, majengo.
Wao Wana point maeneo ambayo ni potential sana Kwa gharama zozote zile
Kuna vifuo vya mafuta vinauza zaidi ya Ltrs 1.2milloni Kwa mwezi
 
Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga . Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi,
Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC , Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.
Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fikka 10- 15mullioni, inategemea ukubwa wa kituo,
Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18millioni.
Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni ,
Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo Moja ni 34millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni,
Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni.
Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta , pamoja na kuchimba mfeteji wa kupitisha Mafuta 3millioni
Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5nillioni.
Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.
NB: hizi ni gharama Kwa kituo standard , ila kama ukiamua kubana Kwa maeneo ya vinijini unaweza punguza gharama kidogo
Hizi gharama ulizotaja unatakiwa uzidishe mara 3 au 4
 
Kuna aina mbili za vituo vya mafuta
1. Filling station na
2 Services. Station.
Kwa filling station gharama zake ni hizo ila Kwa filling station inabeba mambo mengi, mfano super market, car wash, services point za magari,
Tena kwenye filling station ukiwa mjanja gharama zinapungua hapo kama unataka kujenga Kwa kuunga unga , Shida yenu mnatuma mafundi wakanunue material anakupa full cost wewe unatoa Hela yeye anakwenda kununua.
 
Back
Top Bottom