Biashara ya Mazao ya chakula inabaki kuwa ndo biashara yenye Fursa nyingi nzuri pamoja na changamoto zake

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,171
Wakuu naamini kila MTU Ana ndoto ya kufanya biashara Fulani ili afikie malengo yake aliyonayo.

Naamini Kuna wengi wanatamani kujua zaidi hii biashara kabala hawajaingia

Kuna Aina nyingi za Fursa katika biashara ya Mazao inategemea na MTU angependa kujikita wapi

Kwanza Kuna wale wanunulia shambani wanawalipa wakulima kabla ya kuvuna

Pili Kuna ambao wananunua kipindi Cha mavuno kutoka kwa wakulima Kisha wanakusanya kwa ajili ya wanunuzi wakubwa

Tatu Kuna wanunuzi wakubwa wananunua kwa jumla na kupeleka masoko makubwa na
nje ya nchi

Nne Kuna wananunua mazao na kuyahifadhi kwenye maghala wakisubiri Bei ipande

Tano Kuna waliona Fursa ya kujenga maghala ya kukodisha au kuhifadhia Mazao kwa malipo kila mwisho wa mwenzi

Karibuni kushare Fursa zaidi kwenye hii biashara ya Mazao ya chakula na kwa wenye uzoefu zaidi karibuni.

Screenshot_20231106-231535.png
 
Tunaweza kulinganisha Bei ya mwaka Jana na mwaka huu October ,,Mara nyingi hazitofautiana Sana ,
Mara nyingi Bei inaongezeka kadri muda wa mavuno unavyopita mpaka February huko Screenshot_20231107-193622.png

INGAwa mwaka huu naona hizi mvua zinaweza zisimamishe Bei au ishuke zaidi
 
Ulikuwa unaifanyia wapi mkuu
Nimefanya ya kununua mazao kwa wakulima vijijini na kupeleka masoko ya Dar na mikoani, faida ni kama uhakika flani ukijua nini unafanya. Mwaka huu tu ndo naona mishe za town hazijanipa nafasi ya kuingia chimbo.
 
Mi naona hii biashara Ni zuri ukiwa na frem yko kuliko kupeleka kwa madalali sokoni alafu muaze kuzungushana inakuwa shida
Yah hii Fursa nyingine ya Mazao ya chakula,
Muda mzuri wa kuanza Duka la kuuza nafaka Ni kipindi Cha mavuno, unahakikisha unanunua stock ya kutosha ,
Hadi kuja msimu wa uhaba umeshapata faida na mtaji umekuwa stable wa unazungusha kwa faida ya kawaida
 
Back
Top Bottom