Kuzalisha bidhaa za ndani na kuuza masoko ya nje inabaki kuwa ndo fursa na kanuni muhimu ya kukuza uchumi wa nchi na mtu binafsi

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,171
Naomba tuangalie Fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo unaweza kuzifanyia kazi kwa ajili ya MAUZO ya nje (exports)

Wakuu tunaendelea kuangalia kila Aina ya Fursa kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira na salary au kipato kutokukidhi kwa wale wenye ajira, naona Ni vema tukashirikishana Kila Aina ya Fursa inayoonekana au kupatikana 🤝🤝

Naamini hata kama una Ajira bado Kuna maono yako unayo ya kukuongezea kipato Chako au kuweza kufikia Uhuru wa kiuchumi

Kwa leo ningependa tuangalie bidhaa ambazo ziko ndani ya uwezo wa watanzania walio wengi kuzizalisha na kupata nafasi ya kuziuza nje ,
Pia namna ya kupata soko lake

Kwa wale wenye maono ya kuuza bidhaa nje

Hakuna biashara ndogo Ila kila biashara unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka kufikia maono yako
vile vile kwa wale wenye maono ya kufanya biashara l Kuna mahali pa kuanzia kidogo kidogo Hadi kufikia malengo

Kwanza nikiri mchakato wa kuuza Mazao nje unahitaji umakini na uthubutu Ila inabaki kuwa Ni Fursa nzuri

Orodha ya bidhaa zinazozalishwa nje
1.Madini
2.Mazao ya biashara
3.Bidhaa za viwandani
4.Mazao ya uvuvi
5.Mazao ya kilimo bustani bidhaa za kilimo bustani zinazouzwa nje

Mazao ya kilimo bustani yanauzwa nje ya nchi kwa sasa
1.Matunda
2.Mboga mboga
3.Viungo
4.Maua

Katika bidhaa zote zinazozalishwa nje, Mazao ya kilimo bustani ni moja ya bidhaa ambazo uhijataji wake unakua na unaendelea kukua

Kwa hiyo Fursa ya kuzalisha Mazao bustani kwa ajili MAUZO ya nje bado Ni kubwa
Mazao ya bustani yanayowezwa kuzalishwa kwa wingi
1.Matunda Avacado
2.Pilipili Hoho
3.Nyanya nk

Pia Kuna Fursa ya kuanzisha kiwanda Cha kupack Mazao ya bustani ndani badala ya kupack nchi jirani Kama Kenya

Uwezo wetu wa kuzalisha Mazao bustani kwa mwaka
Bado Ni ndogo ukilinganisha na uhitaji wa nje

Uhitaji wa soko la nje Ni mkubwa Sana na unaendelea kuongezeka

Wadau wa kuwezesha kufikia soko la Mazao ya kilimo bustani
Wako wadau wengi wanaowezesha mchakato wa Mazao nje zikiwemo wizara husika

Kila biashara Ni mchakato muhimu Ni maono uthubutu na utayari

Hayo Ni Maoni yangu Karibu
 
Kwa wale tunaopenda kusoma twakwimu unaweza kupitia hili file uone demand ilivyokubwa
 

Attachments

  • HORTICULTURE_TANZANIA.pdf
    2.4 MB · Views: 26
Fursa ya kuibuka kiuchumi ni kutumia rasilimali zetu, ardhi ambayo ni rasilimali kubwa tumeanza kuigawa, bandari tunagawa, madini tunagawa bado tunauza bidhaa ghafi na kukubali kuwa soko la Mataifa mengine ndio maana tunagombana na wakulima wa pamba, korosho, chai na wengineo huku tukikazana kujenga mamall
 
Twakwimu zinaonyesha kilimo kinaajiri zaidi ya watanzania asimia 70
Pia kilimo bustani na mlolongo wake kinaajiri zaidi watanzania laki nne na nusu,
Hivyo tukifanikiwa kulifikia Soko la nje
maana yake tunaendelea kuwapa zaidi ya Kaya laki nne UHAKIKA wa kipato
 
Fursa ya kuibuka kiuchumi ni kutumia rasilimali zetu, ardhi ambayo ni rasilimali kubwa tumeanza kuigawa, bandari tunagawa, madini tunagawa bado tunauza bidhaa ghafi na kukubali kuwa soko la Mataifa mengine ndio maana tunagombana na wakulima wa pamba, korosho, chai na wengineo huku tukikazana kujenga mamall
Ahsante kwa mchango mkuu, je unafikiri nini tufanye tulikamate Soko la nje ?
 
Tusiuze bidhaa ghafi, wenzetu Kama bidhaa haijachakatwa wanaweka Bei kubwa. Ukiuza bidhaa iliyochakatwa unaongeza thamani, inatengenezwa ajira na Kodi inaongezeka.
Ni kweli kabisa mkuu,
Kwa mfano kwa Mazao ya kilimo bustani Kama matunda na mboga wenzetu jirani wanachukua tu wanapack yanaenda nje kwa brand yao na kwa Bei ya juu sana
 
Unalosema ni kweli Tanzania tunautajiri wa ardhi na hali ya hewa inayoruhusu uzalishaji wa mazao mengi hivyo mazao yapo shida nimasoko hasa ya nje kwani ya ndani yanazidiwa . Kiu yangu nini cha kufanya kupata soko la nje au nawezaje kupata mteja wa nje
 
Ni kweli kabisa mkuu,
Kwa mfano kwa Mazao ya kilimo bustani Kama matunda na mboga wenzetu jirani wanachukua tu wanapack yanaenda nje kwa brand yao na kwa Bei ya juu sana
Niambie ni bidhaa gani wakenya wananunua huku kwetu kisha wanaenda kupack kwao
Halafu jinsi ya kupata masoko ya nje 🙏🏻 nahangaika sanaa
 
Back
Top Bottom