Rais Samia, Mazao ya Mahindi na Mpunga Sasa ni Mazao ya Biashara

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,727
Rais Samia amesema mazao ya Mahindi na Mpunga Sasa ni rasmi mazao ya biashara sio ya Kilimo pekee kama hapo awali hivyo Serikali inayachukulia kama mazao ya kimkakati yanayoweza ingizia Serikali pesa za kigeni Kwa haraka..

My Take
Tuendelee kulima Mahindi na Mpunga,Kwa awamu ya 6 ni Neema inaweza kututoa,kama bei zitaendelea kuchangamka kama ilivyo Sasa basi Samia ni 💯💯 Mitano tena .

=====

Miongoni mwa hatua hizo ni kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini na watalii wanaoendelea kumiminika, wanaliingizia taifa fedha za kigeni ambazo kwa sasa uingiaji wake serikalini si wa kuridhisha.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati Rais akifungua kikao cha 14 cha Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais Samia alisema uchache wa fedha za kigeni unaoendelea duniani, Tanzania inaweza kuzipata kwa haraka kupitia mazao ya kilimo.

“Wazalishaji wa mazao ya chakula sasa hivi, mpunga na mahindi ni mazao ya biashara. Zamani yalikuwa mazao ya chakula na hapa nchini tunatarajia kupitia mazao hayo tunaweza kuvuna haraka na kuuza tupate fedha za kigeni,” alisema.

Rais alisema wamechukua hatua za marekebisho katika mauzo ya chakula nchi za nje na wamefanya utafiti mdogo ulioonyesha mauzo ya mpunga na mahindi na mambo mengine yanachangia kiasi gani kwenye fedha za kigeni.

“Tukaona fedha nyingi za kigeni zinakuja kwenye mazao yanayotolewa nje ya nchi na hata hayo mengine hayaleti fedha za kigeni. Wajanja wananunua ndani kwa fedha ya ndani, wao wanauza kwa fedha za kigeni ambayo hairudi tena ndani. Kwa hiyo serikali inachukua hatua kurekebisha hilo kuhakikisha mazao yanaleta fedha za kigeni ndani ya nchi,” alisema.

Rais Samia alisema utalii ni moja ya sekta muhimu kwa uchumi, hivyo ni muhimu kuwapo kwa udhibiti wa fedha za kigeni ili ziingie katika uchumi.

“Mpaka sasa tumeona watalii wengi na malengo ya 2025 tunaweza kuyafikia lakini bado hatujaona fedha kuingia serikalini. Kwa hiyo tutakamatana kidogo huko ili fedha irudi serikalini. Natumaini mikononi kwenu kuna dola nyingi sana zinaingia kuliko zinazoingia serikalini. Tutawaita sekta ya utalii tukae pamoja tuone namna na ninyi mnavyoweza kuisaidia serikali kurudisha dola ndani ya nchi,” alisema Rais.

Alisema kazi kubwa iliyofanyika baada ya Filamu ya The Royal Tour imewezesha kuleta watalii wengi na wanatarajia mwakani wataongezeka.

Rais alisema anatambua changamoto ni kwamba wageni wanaokuja mwakani na mwaka utakaofuata watakosa mahali pa kulala endapo hawatachangamka kujenga hoteli kwa sasa, hivyo akaitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa hiyo.

Alisisitiza suala la utoaji wa vibali kwa taasisi zinazohusika kuhakikisha wanapunguza mlolongo wa kutoa vibali vya ujenzi vya hoteli.

“Utafiti mdogo uliofanyika wageni waliokuja mwaka jana waliorudi ni asilimia 30. Hii inaonyesha watu wanakuja lakini wanasema Tanzania haturudi tena pamoja na vivutio tulivyo navyo. Waangalie hizo kasoro ili wageni wawe wanarudi. Takwimu zinaonyesha wageni wanaotaka kuja na hofu yao ni sehemu ya kulala,” alisema.

MIFUMO KUSOMANA
Pia alisema kazi kubwa watakayoifanya serikalini ni kuhakikisha mifumo ndani ya sekta ya umma inasomana na kuwa na vigezo vya kimataifa. Alisema changamoto zilizotajwa zikiwamo za Kariakoo zimesababishwa na mifumo.

“Si zaidi ya miezi sita ninawaahidi tutakuwa tunasoma kinachotokea bandarini nakisoma mimi Ikulu,” alisema.
Kuhusu baraza hilo, alisema mategemeo yake litaendelea kuwa moja ya vyombo rasmi cha kuishauri serikali kuhusu hatua muhimu za kuboresha mazingira ya biashara kwa lengo la kujenga uchumi himilivu, shirikishi.
Alisema mashauriano hayo yawe ni njia ya kuimarisha uwezo wa sekta binafsi kuzalisha bidhaa za huduma zitakazopunguza uagizaji na kuongeza mauzo katika masoko ya kikanda na kimataifa.
Alisema hatua hiyo itasaidia nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kuongeza mapato na kuimarisha uchumi wa nchi.

PATO LA TAIFA
Rais Samia alisema pato la taifa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka jana liliongezeka hadi kufikia Sh. trilioni 45.2 kutoka Sh trilioni 39.9 mwaka 2021.

Pia aliwataka mawaziri na makatibu wakuu kuyachukua yale yaliyozungumzwa katika kikao hicho na kuyafanyia kazi. Pia aliwataka viongozi ngazi zote kuendeleza majadiliano hayo kupitia mabaraza ya biashara ya mkoa na wilaya na kuwasilisha taarifa zake kila robo mwaka au wanapokutana.

Pia alisema eneo ambalo halijafanyika vizuri ni kuweka mifumi ya kujitathimini na kufuatilia ambalo litakuwa linawapa taarifa nini kimefanyika vizuri na kitu gani bado, kasoro ni nini na tatizo lipo wapi. Alisema hatua hizo zikichukuliwa zitaimarisha ukuaji wa sekta binafsi, kuongeza ushindani wa bidhaa kwa Tanzania na masoko ya dunia.

KAULI YA TPSF
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Mwenyekiti mwenza wa baraza hilo, Angelina Ngalula, aliiomba serikali kuhakikisha mifumo inasomana katika kutatua changamoto zao ili kupunguza mzigo hasa kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwenye usimamizi wa mapato.

Alisema wamebaini kuwa spika zinazoingizwa nchini hazina ubora unaotakiwa, hivyo kuliomba Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufuatilia ili kupata vifaa vyenye ubora. Ngalula alisema urasimu uzembe na kukosekana kwa ufanisi katika uendeshaji wa bandari, umekuwa ni mradi unaowapatia watu mabilioni ya fedha.

Alisema TPSF inaipongeza serikali kwa hatua ngumu iliyochukua ya kukaribisha sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari hiyo, jambo ambalo wanadhani litaongeza ufanisi, na hivyo kuharakisha ukuaji uchumi kupitia rasilimali hiyo.

Alisema bandari zinazoizunguka Tanzania zinafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na uzembe na kukosekana kwa ufanisi kwenye bandari.

“Urasimu huu umechochea rushwa na hivyo kuongeza gharama, hivyo sisi tuko na wewe katika hili,” alisema.
 
Back
Top Bottom