Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Ke
Habarini wana jamvi.

Sina mengi ya kuelezea ila hii issue ya BETTING tu, nimejitolea maeneo fulani na kwa mwezi naingiza 250K lakini nikiangalia maendeleo yangu tangu 2022 ni sawa na ziro, sina matumizi mengi kwa siku (hayazidi 4000/=) ila nimekuwa addicted na BETTING yaani siku haiishi bila kuweka mkeka.

Nimejikuta naingia kwenye madeni na kwa sasa nadaiwa zaidi ya 500K na watu watatu, huwa natamani kuacha ila wiki haikati narudi. Nilikuwa nimelenga kufungua studio/library mbili za kurusha movie na miziki lakini naona mwaka unaenda kuisha empty.

Deni lilianza kidogo tu ila nimekuwa na desire ya kulilipa kupitia BETTING. Nikipokea posho naweza kutumia hata laki kwa wiki nashinda lakini zote zinaishia hukohuko.

Naweza kuonekana wa ajabu lakini hii hali ndio napitia na inaniuma sana. Nimewakosea wazazi na majirani na Mungu lakini naamini huu utakuwa mwisho.

Nimeamua kwa sasa nijikite kwenykulipa madeni hayo japo naona naenda kudhalilika maana sina kitu kabisa na muda ndio huu.

Baada ya mwezi mmoja, yaani tar 30/06 nitakuja kutoa mrejesho, niombeeni ndugu zangu (seriously) niweze kuikwepa hii aibu.

Nisaidieni hata kwa ushauri wana Jf. Mwenyezi Mungu awabariki
Betting ni aina ya kamari. Ukitaka uharibikiwe maisha, cheza kamari. Ni aheri mlevi wa pombe, ni aheri mpenda wanawake, kuliko mcheza kamari. Mcheza kamari wakati wote anapoendelea kuliwa, anaendelea kuamini kuna siku atabahatisha. Akibahatisha mara moja, anapoteza zaidi ya mara 10.

Nimeona America, Ulaya na Australia, watu walioharibiwa na kamari. Wengine mpaka hela ya mafao yao ya mwisho wakati wanastaafu, wamemalizia kwenye kamari, mpaka wanakuwa kama mazezeta. Mpaka wengine wanapelekwa kwenye vituo vya counciling ili kujaribu kuwarudisha kwenye uhalisia wa maisha.

Usijiingize kwenye betting, kwa sababu betting ni kamari, na kamari inasababisha addiction. Ukiwa addicted, hata ushauriwe vipi, huwezi kuelewa.

Umefanya vizuri sana kurudi nyuma na kuyatafakari maisha yako. Sasa ufanye kiapo cha moyoni kuwa hutafanya betting, hutacheza kamari wala kujaribu kucheza mchezo wowote wa kubahatisha. Na uamini kuwa kupoteza hela kwenye betting au kamari, ni kukosa akili, na uape moyoni mwako kuwa hutaki kuwa mpum.bavu tena wa kupoteza pesa yako kwenye betting. Wazo likikujia la kutaka kufanya betting, jiambie moyoni mwako, sitaki, siwezi kufanya hivyo tena, kwa sababu mimi siyo mpumb,avu, betting ni kwaajili ya wasio na akili.
 
Mimi msimu huu wote nimepata kama mil 10 na ushee 5,900,000 nilipata kwa pamoja kwa dau la 3000 kwa timu 22 na mil 3,700,000 pia nilizipata kwa pamoja kwa dau la 300.
  • Hizi namba ndio haswaa zinazomfanya ashindwe kuacha.
  • Hapa tayari umemtamanisha ajaribu tena na tena, huenda akaangukia kwenye 10M kwa mtaji wa chini ya 10,000
 
Habarini wana jamvi.

Sina mengi ya kuelezea ila hii issue ya BETTING tu, nimejitolea maeneo fulani na kwa mwezi naingiza 250K lakini nikiangalia maendeleo yangu tangu 2022 ni sawa na ziro, sina matumizi mengi kwa siku (hayazidi 4000/=) ila nimekuwa addicted na BETTING yaani siku haiishi bila kuweka mkeka.

Nimejikuta naingia kwenye madeni na kwa sasa nadaiwa zaidi ya 500K na watu watatu, huwa natamani kuacha ila wiki haikati narudi. Nilikuwa nimelenga kufungua studio/library mbili za kurusha movie na miziki lakini naona mwaka unaenda kuisha empty.

Deni lilianza kidogo tu ila nimekuwa na desire ya kulilipa kupitia BETTING. Nikipokea posho naweza kutumia hata laki kwa wiki nashinda lakini zote zinaishia hukohuko.

Naweza kuonekana wa ajabu lakini hii hali ndio napitia na inaniuma sana. Nimewakosea wazazi na majirani na Mungu lakini naamini huu utakuwa mwisho.

Nimeamua kwa sasa nijikite kwenykulipa madeni hayo japo naona naenda kudhalilika maana sina kitu kabisa na muda ndio huu.

Baada ya mwezi mmoja, yaani tar 30/06 nitakuja kutoa mrejesho, niombeeni ndugu zangu (seriously) niweze kuikwepa hii aibu.

Nisaidieni hata kwa ushauri wana Jf. Mwenyezi Mungu awabariki
Na bado Samia anakuvuruga pole mchungaji gwajiboy
 
GwajiBoy
Nina amin kabisa utaacha kamari.
1. Sahau hela ulizopoteza nyuma
2. Ipigie budget hela yako unayopata kihalali
3. Punguza matarajio ya kuwa tajiri ndan ya siku moja.
4. Futa app za bet kwa simu yako
5. Usikae na wakamaria Wenzako au kwepa kwenda maeneo ambayo utakutana na washkaj na kwepa kabisa ile post ya mikeka😂😂😂

Kila la kheri
Tmr tar 1.
 
🤝🤝🤝
 
Nashukuru mkuu, nimeiscreenshot kabisa 🤝🤝🤝
 
Uliambiwa Cheza kwa kiasi wewe ukapitiliza Kwanini usiwe Maskini.
Kwenye Laki moja unatakiwa utumie alafu 10 tu kubetia, katika kubeti usifilie za kula mamilioni vikilia kupata hamsi imezi laki.
tena beti panga siku mbili za kubeti kwa wiki siyo kila siku na usitumie zaidi ya 6,000. kubeti chukulia tu kama sehemu ya kuzifahamu timu duniani, wala usifanye kama kazi.
Mimi msimu huu wote nimepata kama mil 10 na ushee 5,900,000 nilipata kwa pamoja kwa dau la 3000 kwa timu 22 na mil 3,700,000 pia nilizipata kwa pamoja kwa dau la 300.
laki 4 laki 2 kushuka chini nimepata mara kadhaa, hivyo tusiwe fedha unayoitgemea kuendesha maisha yako.
Huko hamna kaka, bora niwaeleze kwenye miradi midogomidogo kama kuajiri vijana wa mayai, Chipsi na bustani za mbogamboga
 
Mbona kina sativa wanasema wanapata mamilioni ? Kina baba Levo?

Nishagundua betting sio ya masikini, tafuta odds 2 , stake high! Kaa hapo agiza kuku na balimi baridi !

Sio unaweka jero mkeka odds 250 unataka ushindi laki 5 !!!

Kingine betting niseme sio ajira, ama njia kuu ya kipato,,,ile ni kama changamsha bongo tu !
Hata odds 1.12 nayo ina chana

Betting ni kisanga haijawahi kuwa na fundi wake.

Ndio maana huwa nashangaa eti unakuta wachambuzi wanauza odds kwa madai ya sure odds na watu wana jaa.

Hainaga formula ile
 
Back
Top Bottom