Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Wee tatizo tamaaa, weka odds za 1.5-1.7 mbona unaenjoy maisha wikend kama hivi ungekuwa hapa samaki samaki unapapasa matako ya warembo.
Hamna biashara n,uri dunia i kama betting
Bro hapa naandaa mikakati ya kulilipa hilo deni, ila nimeachana na hizo issues
 
Wee tatizo tamaaa, weka odds za 1.5-1.7 mbona unaenjoy maisha wikend kama hivi ungekuwa hapa samaki samaki unapapasa matako ya warembo.
Hamna biashara n,uri dunia i kama betting
1.5-1.7 yani aweke laki ili apate buku 5- buku 8?
 
Kila kilichoharamishwa na Uislamu jiepusheni nacho

Pombe kamari uchawi kuangalia

Mwenye sikio na asikie
 
Kaka addiction inaambatana na maumivu
mimi siwezi kuwa na addiction ya kupoteza hela mara ya mwisho nilideposit 5000 sport nikatengeza plus na ya kukopi code nikapunwa yote wakanirudishia vishilingi vya free bet pia wakavipuna. Hiyo ilikuwa january sijabet hadi leo!
 
Habarini wana jamvi.

Sina mengi ya kuelezea ila hii issue ya BETTING tu, nimejitolea maeneo fulani na kwa mwezi naingiza 250K lakini nikiangalia maendeleo yangu tangu 2022 ni sawa na ziro, sina matumizi mengi kwa siku (hayazidi 4000/=) ila nimekuwa addicted na BETTING yaani siku haiishi bila kuweka mkeka.

Nimejikuta naingia kwenye madeni na kwa sasa nadaiwa zaidi ya 500K na watu watatu, huwa natamani kuacha ila wiki haikati narudi. Nilikuwa nimelenga kufungua studio/library mbili za kurusha movie na miziki lakini naona mwaka unaenda kuisha empty.

Deni lilianza kidogo tu ila nimekuwa na desire ya kulilipa kupitia BETTING. Nikipokea posho naweza kutumia hata laki kwa wiki nashinda lakini zote zinaishia hukohuko.

Naweza kuonekana wa ajabu lakini hii hali ndio napitia na inaniuma sana. Nimewakosea wazazi na majirani na Mungu lakini naamini huu utakuwa mwisho.

Nimeamua kwa sasa nijikite kwenykulipa madeni hayo japo naona naenda kudhalilika maana sina kitu kabisa na muda ndio huu.

Baada ya mwezi mmoja, yaani tar 30/06 nitakuja kutoa mrejesho, niombeeni ndugu zangu (seriously) niweze kuikwepa hii aibu.

Nisaidieni hata kwa ushauri wana Jf. Mwenyezi Mungu awabariki
 
Kituu
 

Attachments

  • IMG-20250530-WA0007.jpg
    IMG-20250530-WA0007.jpg
    67.5 KB · Views: 32
Hamna bwana upate 50k au 70k
Hiyo yako ni 1.05 ndio 100k ikupe buku 5
Mambo hayapo hivyo Muhindi anaijua hela hawezi kukuwekea mazingira mepesi ya wewe kula

Angalia hii ni odds 1.16
1748687258352.png
 
Namna ya kuacha kubeti.
Kwanza usikubali kumtamani mtu aliye win betting kwa kujipa moyo nawewe ipo siku utashinda. Betting ni bahati ya mtu na mtu,na kiuhalisia kama mtu kashinda 5M m,kuna uwezekano mkubwa kabla ya kushinda hiyo pesa ashaliwa kama 3M,na baada ya kushinda ataliwa tena zaidi ya 3M huko mbele kabla ya kushinda tena( siyo kwa wote,wapo wanaojaribu na kushinda,inabidi ukubali kuwa wewe siyo miongoni).

Ukisha ishinda roho ya tamaa ya pesa za kubeti; fanya maamuzi,kama mwanaume inabidi uwe mtu wa kushinda baadhi ya vitu vigumu. Mfano umefanya hiyo kazi kwa huo muda na haijakuletea matokeo zaidi ya hasara,achana nayo! Kubali haipo kwa ajili ya wewe.
Kama una account za betting futa. Jikubali kuwa umeacha. Nami nlishawahi kupitia wakati wa kujiuliza kama ntakuja acha betting,mpaka pale nlipokosea nikabetia 60% ya hela ya Ada ya chuo. Ilinifanya niichukie betting na mpaka sasa hata mtu niwe naye ashinde milion 500,hawezi nishawishi sababu hiyo itakuwa bahati yake siyo yangu.

Leo kuna UEFA final. Inter ambaye kafika fainal mara mbili kwa interval ya miaka 3 kapewa odds nyingi😁 Usibeti!
 
Habari. Nimekuwa mtumiaji wa 1XBET kwa miaka 8. Lakini Baadaya kufanya update imegoma inasema haipatikani nchini. Natumia simu ya IOS (Iphone 7plus storage ni 128GB.
 
Hatari sana hii kitu yanii balaa tupu..! ukishindwa anza kubet bila malengoo weka 200 wekaa 300 kwa slip ila ukiweka malengo ya kushinda mil 10 kwa kubet laki 2 kazi unayo
 
Back
Top Bottom