GwajiBoy
Member
- Jan 7, 2025
- 34
- 60
Habarini wana jamvi.
Sina mengi ya kuelezea ila hii issue ya BETTING tu, nimejitolea maeneo fulani na kwa mwezi naingiza 250K lakini nikiangalia maendeleo yangu tangu 2022 ni sawa na ziro, sina matumizi mengi kwa siku (hayazidi 4000/=) ila nimekuwa addicted na BETTING yaani siku haiishi bila kuweka mkeka.
Nimejikuta naingia kwenye madeni na kwa sasa nadaiwa zaidi ya 500K na watu watatu, huwa natamani kuacha ila wiki haikati narudi. Nilikuwa nimelenga kufungua studio/library mbili za kurusha movie na miziki lakini naona mwaka unaenda kuisha empty.
Deni lilianza kidogo tu ila nimekuwa na desire ya kulilipa kupitia BETTING. Nikipokea posho naweza kutumia hata laki kwa wiki nashinda lakini zote zinaishia hukohuko.
Naweza kuonekana wa ajabu lakini hii hali ndio napitia na inaniuma sana. Nimewakosea wazazi na majirani na Mungu lakini naamini huu utakuwa mwisho.
Nimeamua kwa sasa nijikite kwenykulipa madeni hayo japo naona naenda kudhalilika maana sina kitu kabisa na muda ndio huu.
Baada ya mwezi mmoja, yaani tar 30/06 nitakuja kutoa mrejesho, niombeeni ndugu zangu (seriously) niweze kuikwepa hii aibu.
Nisaidieni hata kwa ushauri wana Jf. Mwenyezi Mungu awabariki