Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

mimi nampongeza mh.Mkapa kwa kazi aliyofanya kipindi chake..wala huwez kufananisha uongozi wa mkapa na kikwete.
Kipindi cha mkapa,mchele kg 1 ilikuwa 500shs. Sasa hivi ni 2700,,sukari kilo ilikuwa 1000,sasa hvi robo 900..mkapa alijitahidi sana ijapokuwa alikabidhiwa nch ikiwa na madeni mengi,,alikabidhi kwa kikwete nchi isiyodaiwa,,mkapa aliiba pia ila nampongeza kwa kuwa alijua kula na kipofu,ila huyu mjomba amezidi na ameiua ccm,,baba yangu wa miaka sabini anapiga gwanda la cdm kisa huyu current mskaji

Kaka upandaji wa bei za vitu ni dunia nzima sio Tanzania tu;hata huyo Makapa angelikuwa raisi wa Tanznaia huvi sasa bei zingelipanda tu
Mkapa fisadi kaiweka Tanzania pabaya Kiwete karithi mambo mengi kutoka kwa mr Ben Fisadi
 
Tukiachana na mapungufu yake kama Ben bila shaka tutaona kuwa amenena ukweli.
 
acha kubwabwaja we mutu.si bora yeye hata kama aliiba lakini alisimamia uchumi tukanufaika na wengine?au si bora yey ambaye aliiweka wazi kampuni yake kuliko wengine waliochakachua majina wakaja na richmond/dowans?wezi kila kona wanaiba na ili kuficha wizi wao wanatufitinisha tuendelee kugombana wakati wao wako bize wanaiba?
ndugu yangu, soma post yangu uelewe, nimesema "baadhi"... neno baadhi lina maana sana kama wewe ni muangalifu lakini hupotea hata kwenye sentensi kama msomaji ni mtu anayeamua kabla ya kutafakari

Ni lazima uelewe kuwa systems hazifeli overnight, dowans nk hazikuanzia from nowhere, ni mianya iliyoanzishwa kabla, e.g. EPA na mchango wake kwenye kurutubisha ufisadi, ambao nao una mchango mkubwa sana wa kuzaa taifa la wajinga

ni taifa la wajinga tu ndilo linalobariki udini hadi ikulu... haiwezekani rais akaja baada ya siku mbili mambpo yakaanguka yote, lazima kulikua na abuse avenues ambazo rais JK alikuja na yeye na uzisasambua. Hakuna asilani system ya nchi inayobadilika in 3 year unless kulikua na mapinduzi ya ajabu, maana mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu, watendaji wakuu wa idara za serikali, ulinzi na usalama walikua walewale tu, ni culture iliyopo na iliyokuwepo ingawa imekua mbaya zaidi

Mikataba ya madini tu inatukosesha matrilioni, suala la land abuse, nk lakini jamaa bila aibu alikenua meno na kupokea "mkate" wa dhahabu...

Yes, Mkapa kuna aliyofanya mazuri, lakini pia si mtu sahihi kusimama tena kwenye sehemu takatifu na kujionyesha kwamba hana najisi..... huo ni unafiki

kumbuka hata Mo award, ni mwaka pekee ambao walifuta zawadi baada ya shortlisted candidates kuwa dhaifu, including MB

btw, anayebwabwaja ni bibi yako mzaa baba......... maana kama ni madomo machafu hata sisi tunayo
 
Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa, amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.

"Asema aliongoza taifa bila ya ubaguzi wa kidini, aonya viongozi wa sasa wafuate misingi ya Nyerere" Mkapa ameonya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

"Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu, pamoja na tofauti zetu za kiimani" Pia Rais Mstaafu Mkapa amesema "Kizazi kipya kimeanza kuonye mambo ya ajabu sana, kinadhalilisha utu wa watu na hakuna upendo, sisi sote ni waja wake Mungu."


CHANZO: mwananchi, Jumatatu, April 8, 2013 (kwa habari zaidi)
 
Baada ya kufanya mauaji ya kimbari pale Mwembechai na Zanzibar anajiona alikuwa kiongozi wa kupigiwa mfano ?
Labda kwa kusaidia kulistawisha KANISA hapa Tanzania !

Ni UJINGA wa Watanzania tu hasa WAISLAMU ni kwanini mdudu huyu hajapelekwa the hague !
Mwembechai rais wetu alikuwa mzee rukhsa, ally h.mwinyi
 
Inamshinda nini kumwonya huyo teenager anayechekacheka kama hana akili nzuri huko ikulu? Ni rais gani Africa aliyekwisha onyesha ujinga wa kuiuza nchi yake kama kikwete? Mbona asimwambie tu ukweli badala ya kuzunguka mbuyu? Ni raisi gani aliyekwisha uwa elimu, matibabu, na usafiri wa miundombinu huku akichukua kodi za walalahoi wake kujitibia India yeye na viongozi wengine huku nyuma akitesa madaktari na kuwadhalilisha kiharamia? Ni rais gani anayetumia udini na kuupandikiza kati ya raia wake eti kisha apate nguvu ya kuingia ikulu? Hiyo ikulu bila amani ina maana gani? Ni raisi gani anayeruhusu nusu ya nchi ijiunge na jumuiya ya kiislamu bila ridhaa ya wananchi wa nchi nzima? Hiyo Zanzibar sii sehemu ya Tanzania? Kikwete ni mjiga periodi! Mkapa analijua hilo na inabidi amwabie ukweli kwani ameiharibu sana nchi yetu.
 
Mkapa hasafishiki,na hana lolote alilofanya zaidi ya kuidunisha nchi,miundomini alikuwa akiijenga ukweni kwake tu huko kilimanjaro,na kuipendelea mikoa ya wakristo ndio maana wanaomsifia ni wakristo,siku ikisimama jihadi Tanzania sijui itakuwaje.Maana kuna wengi sana wanahatia.Ila tegemeo letu ni mungu,itiqaf hatutaacha mungu atawadhalilisha wote wanaowaonea waislam kwa chuki zao.Fanya utafiti wa vifo vya wanadhulumu na kuwanyanyasa wengine,mwangalie farao(filauni) LTA
Nakubaliana na wewe ila naomba utakapokuwa unawaombea wengine hiyo itiqaf wewe pia uiweke vizuri miguu yako maana Mungu anahukumu kwa haki sio kwa sababu wewe umemuomba
 
Rais Mstaafu Ben Mkapa amesema baada ya uongozi wake anashuhudia mambo mengi ya ajabu ikiwemo mitafaruku katika jamii.

....

Nkapa tena? Unapofikiri sarakasi imefikia mwisho,anatokea gambaz ingine inaanzisha igizo jipya la sarakasi.
Anyway, Danganyikas/taifas like to be intertained.

Wakati Mkapa ana"tu"nunulia Radar na ndege ya Rais walisema tutakula nini?

Muzee ameondoka na EPA yake, Kiwira,kugawana nyumba za serikali? Igizo likaisha.

Hivi Richmond/Dowans wameshakinga bakuli? Igizo linaendelea.
 
Nakubaliana na wewe ila naomba utakapokuwa unawaombea wengine hiyo itiqaf wewe pia uiweke vizuri miguu yako maana Mungu anahukumu kwa haki sio kwa sababu wewe umemuomba

Mikoa ya Kikristu ipi?hii ni idiocy beyond belief
 
Rais Mstaafu Ben Mkapa amesema baada ya uongozi wake anashuhudia mambo mengi ya ajabu ikiwemo mitafaruku katika jamii.

Kwamba anachojivunia katika uongozi wake ni kuwa hakuwahi kuambiwa anabagua.

Amesema kizazi kipya cha uongozi kinatakiwa kurudi katika misingi aliyoacha Mwalimu Nyerere ambayo ni Amani na Utulivu.

Amesema hayo mjini Bukoba wakati akitoa salaamu baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katholiki la Bukoba Desidelius Rwoma aliyehamishwa kutoka Jimbo la Singida kuchukua na nafasi ya Askofu Nestory Timanywa aliyestaafu baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 39.
ASKOFU MPYA WA BUKOBA
MHASHAMU ASKOFU DESIDERIUS RWOMA

2_Rwoma.jpg
Waamini na wapenzi wa Bukoba na Kagera wamefurahi sana kumpata Baba Askofu Desiderius Rwoma kama askofu wa Jimbo la Bukoba kumrithi askofu Nestor Timanywa ambaye amestaafu kufuatana na sheria za kanisa.

4_Bukoba_Born_Bps.jpg
Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa.

3_Bp_Rwoma_and_Nestor.jpg

Alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Nestor Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.
​

  • Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani. Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.
  • Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa karibu nao.
  • Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa singida alikuwa makamu wa askofu na hivyo kulijua jimbbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.

6_Bp_Rwoma_in_Singida_(4).JPG

Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.

Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa walei

Askofu Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusiano mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.


futari+ikulu.JPG

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki
wa jimbo Kuu la Dar es salaam Methodius Kilaini ambaye alishiriki katika futari
iliyoandaliwa na rais, Ikulu jijini Dar es Salaam ambayo imehudhuriwa na
waalikwa wa kutoka sehemu mbalimbali.



TimaandKila.jpg
Askofu Mstaafu Nestory Timanywa wa Jimbo Katoliki Bukoba akiwa na Askofu msaidizi wake Methodius Kilaini
Askofu-Mkuu-Norbert-Mtega-Placidus-Gervasius-Nkalanga-na-Kadinali-Policarp-Pengo1.-8-June-2011.-Hanga-abbey..jpg
Askofu Mstaafu Jimbo Katoliki Bukoba Gervas (Placidus) Nkalanga OSB aliye katikati katika picha
kushoto kwake ni Askofu Mkuu Norbert Mtega wa Jimbo Kuu la Songea na kulia ni Mwadhama Policarp
Cardinal Pengo Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Dar es Salaam. Hapa ni nafasi alipofanya Jubilei ya
Uaskofu miaka 50, amekuwa mtawa wa Hanga Abbey kwa miaka karibu 30.

​

Askofu Gervas (Placidus) Nkalanga OSB ambaye alikuwa mtangulizi wa Askofu Nestory Timanywa Jimbo la Bukoba kwa sasa ni mtawa wa shirika la St. Ottilien la watawa Wabenediction ambalo maskani yake ni Hanga Abbey, Songea. Baada ya kustaafu aliamua kuishi maisha ya kitawa uamuzi ambao ni nadra mno kwa wengi waliokwisha onja heshima ya ukuu wa jimbo. Kabla ya kuwa Askofu wa Jimbo la Bukoba alikuwa askofu katika jimbo moja wapo la huko Uganda.


100_3177-300x225.jpg
Bishop-Plasdus-OSB1.-300x225.jpg
Z
A-photo-with-bishops-and-religious-women-who-played-a-good-role-in-the-celebration-of-50-years-of-Bishop-Placidus-G1.-Nkalanga-O-300x225.jpg
Monks-of-Hanga-and-bishops-of-Tanzania-participated-fully-in-celebrating-the-golden-jubilee-of-bishop-Placidus-Gervasius-Nkalan1-300x225.jpg
Bishops-of-Tanzania-and-the-monks-of-Hanga-abbey1.-8-June-2011.-300x225.jpg
Bishop-Placidus-Gervasius-Nkalanga-OSB-is-going-for-the-Holy-mass1.--225x300.jpg

​

Askofu Gervas (Placidus) Nkalanga OSB ni askofu pekee aliyebaki hai mkatoliki tuliye naye ambaye alishiriki Mkutano Mkuu wa Kanisa Katoliki Vatican Rome mwaka 1962-1963 ujulikanao kama Mtaguso Mkuu wa Vatican II, wakati huo alikuwa pamoja na hayati Mwadhama Laurean Cardinal Rugambwa, na hayati Askofu Carol Msakila wa jimbo La Karema ambaye baada ya kumeguka jimbo la Kigoma akawa Askofu wa jimbo Katoliki Sumbawanga ambalo nalo limemeguka kuzaa jimbo la Mpanda.

Askofu Nkalanga pamoja na umri mkubwa, na heshima aliyokuwa nayo amekuwa mnyenyekevu wa hali ya juu na kuishi maisha ya kitawa kufungu, kusali na kuiombea dunia ambayo wengi hawawezi kuamini huku akiendelea kutoa mchango wake wa kiroho na kimwili kwa jamii na shirila lake. Amekuwa na shamba la migomba ambalo alilianzisha na amelitunza vizuri na kuwa kivutio kwa wageni wengi kuangalia zao hilo linavyoweza kuendeshwa kitaalamu na kutoa matunda ya kujivunia.


Bishop Methodius Kilaini Mategemeo ya wengi Kurithishwa jimbo
Wakati ukiwa Askofu Msaidizi wa Jimbo mara nyingi inaelekea kuwa na nafasi kubwa ya kurithi kiti cha Jimbo mara itokeapo Vacancy katika jimbo hilo, na pengine jimbo jingine kuwapo na kiti wazi kuna nafasi kubwa ya kuhamishiwa huko. Kwa hili la bukoba baada ya Askofu Nestory Timanywa kustaafu, ni mategemea makubwa ya wengi kwamba Askofu Msaidizi Methodius Kilaini angeshika hatamu za jimbo, mambo yamekuwa kinyume cha matarajio ya wengi.

Kanisa Katoliki ni muhimu sana kuchunga ulimi, kuruhusu kutoa matamko kama ilivyozoeleka katika madhehebu mengine kila mwenye jimbo anajitolea tamko lake kwa Catholic ni haramu, inafuata hierarikia ya kanisa. Huenda kasoro hiyo tu inaweza kutompa nafasi kukalia kiti, maana akiwa na sauti katika Jimbo mambo yanaweza kuwa kana kwamba jimbo limejitenga kutoka hierarikia ya kanisa kwa kuwa na sauti pekee yake bila ridhio la jumla kikanisa.
 
Mikoa ya Kikristu ipi?hii ni idiocy beyond belief
utakuwa umenikuu vibaya, huwa simkubali mkapa lakini kwa maelezo wanayotoa baadhi ya watu kama kasoro za mkapa zimeufanya mjadala uwe wa kitoto
 
Inamshinda nini kumwonya huyo teenager anayechekacheka kama hana akili nzuri huko ikulu? Ni rais gani Africa aliyekwisha onyesha ujinga wa kuiuza nchi yake kama kikwete? Mbona asimwambie tu ukweli badala ya kuzunguka mbuyu? Ni raisi gani aliyekwisha uwa elimu, matibabu, na usafiri wa miundombinu huku akichukua kodi za walalahoi wake kujitibia India yeye na viongozi wengine huku nyuma akitesa madaktari na kuwadhalilisha kiharamia? Ni rais gani anayetumia udini na kuupandikiza kati ya raia wake eti kisha apate nguvu ya kuingia ikulu? Hiyo ikulu bila amani ina maana gani? Ni raisi gani anayeruhusu nusu ya nchi ijiunge na jumuiya ya kiislamu bila ridhaa ya wananchi wa nchi nzima? Hiyo Zanzibar sii sehemu ya Tanzania? Kikwete ni mjiga periodi! Mkapa analijua hilo na inabidi amwabie ukweli kwani ameiharibu sana nchi yetu.

Kwa hili la kujiunga OIC sipo nawe. Mbona Vatican wana ubalozi hapa Tz, Watz tulidhirikishwa ktk suala la kufungua ubalozi hapa ilhali Vatican inajulikana wazi ipo kwa maslahi ya wakatoliki. Huoni dini nyingine zinadhulumiwa kwa hili. Hebu acha udini wako mfilisika mkubwa wa tafakuri we.
 
Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa, amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.“Asema aliongoza taifa bila ya ubaguzi wa kidini, aonya viongozi wa sasa wafuate misingi ya Nyerere” Mkapa ameonya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. “Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu, pamoja na tofauti zetu za kiimani” Pia Rais Mstaafu Mkapa amesema “Kizazi kipya kimeanza kuonye mambo ya ajabu sana, kinadhalilisha utu wa watu na hakuna upendo, sisi sote ni waja wake Mungu.” CHANZO: mwananchi, Jumatatu, April 8, 2013 (kwa habari zaidi)
sisi tulioongozwa ndo tunapaswa kumwelezea mkapa si yeye,kama alifata misingi ya nyerere mbona aligawa migodi,nyerere hakua na kampun ila tuliisikia ANABEN,CHIN YA UTAWALA WAKE ALIWATWANGA RISAS WAISLM MWEMBE CHAI PALE NA KUWAUA WAPINZAN 2001 ZENJ
 
Inamshinda nini kumwonya huyo teenager anayechekacheka kama hana akili nzuri huko ikulu? Ni rais gani Africa aliyekwisha onyesha ujinga wa kuiuza nchi yake kama kikwete? Mbona asimwambie tu ukweli badala ya kuzunguka mbuyu? Ni raisi gani aliyekwisha uwa elimu, matibabu, na usafiri wa miundombinu huku akichukua kodi za walalahoi wake kujitibia India yeye na viongozi wengine huku nyuma akitesa madaktari na kuwadhalilisha kiharamia? Ni rais gani anayetumia udini na kuupandikiza kati ya raia wake eti kisha apate nguvu ya kuingia ikulu? Hiyo ikulu bila amani ina maana gani? Ni raisi gani anayeruhusu nusu ya nchi ijiunge na jumuiya ya kiislamu bila ridhaa ya wananchi wa nchi nzima? Hiyo Zanzibar sii sehemu ya Tanzania? Kikwete ni mjiga periodi! Mkapa analijua hilo na inabidi amwabie ukweli kwani ameiharibu sana nchi yetu.

Kikwete huwezi kumshauri. Hiyo ni personality yake.

Alikimbilia ikulu kwa ajili ya anasa zake na wala si maendeleo ya watanzania na ndiyo maana anawaona na kuwatreat kama nguchiro. Ni sawa na fisadi Lowasa anavyonyemelea nyemelea, hila za kwenda ikulu. It is not for any public interest. Anafanya kila hila aingie ikulu for his ego and pride. Mtaniambia.

Kosa ni ujinga wa kumpa mtu kama kikwete, kuna habari kwamba hata mwl Nyerere alisema anajuta kumpa nchi mwinyi.

Watu design hii hawafai kuongoza nchi. Wanaturudisha nyuma sana ki maendeleo. DAWA HAKUNA KUWAPA NCHI TENA. WATABAKI VIONGOZI WA KAWAIDA ILI WAWE CHINI YA UTAWALA WA MTU MWENYE AKILI.
 
Kwa hili la kujiunga OIC sipo nawe. Mbona Vatican wana ubalozi hapa Tz, Watz tulidhirikishwa ktk suala la kufungua ubalozi hapa ilhali Vatican inajulikana wazi ipo kwa maslahi ya wakatoliki. Huoni dini nyingine zinadhulumiwa kwa hili. Hebu acha udini wako mfilisika mkubwa wa tafakuri we.

kwani kuwa na ubalozi hapa ni kumwa mwanachama wa Vatican?
 
Kwa hili la kujiunga OIC sipo nawe. Mbona Vatican wana ubalozi hapa Tz, Watz tulidhirikishwa ktk suala la kufungua ubalozi hapa ilhali Vatican inajulikana wazi ipo kwa maslahi ya wakatoliki. Huoni dini nyingine zinadhulumiwa kwa hili. Hebu acha udini wako mfilisika mkubwa wa tafakuri we.

Kuna tofauti gani kati ya ubalozi wa Vatican na Ubalozi wa Saudi Arabia? Au kwa kuwa Vatican ni nchi ndogo?
 
Back
Top Bottom