Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

KAUDO

Senior Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
138
Reaction score
67
Rais Mstaafu Ben Mkapa amesema baada ya uongozi wake anashuhudia mambo mengi ya ajabu ikiwemo mitafaruku katika jamii.

Kwamba anachojivunia katika uongozi wake ni kuwa hakuwahi kuambiwa anabagua.

Amesema kizazi kipya cha uongozi kinatakiwa kurudi katika misingi aliyoacha Mwalimu Nyerere ambayo ni Amani na Utulivu.

Amesema hayo mjini Bukoba wakati akitoa salaamu baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katholiki la Bukoba Desidelius Rwoma aliyehamishwa kutoka Jimbo la Singida kuchukua na nafasi ya Askofu Nestory Timanywa aliyestaafu baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 39.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni. Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.

"Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.

Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.

"Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema.

Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.

Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na yale ya Kiislamu.

Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.

Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na Tunduma.

Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.
 
yawezekana kabisa baadhi ya mbegu za kibaguzi na social injustice alizipanda au hata kuzimwagilia yeye, hasa ufisadi

ni rais wa ajabu anayefungua co. ltd akiwa ikulu na kutumia anuani ya ikulu

He cant escape responsibilities for what we are now as a nation
 
Huyu ndie alikuwa fisadi kaiba sana na mali za watanzania live. Leo anaishi kuula pesa za wizina familia yake. Huyu nae ni wa kufunguliwa mashtaka na kunyanganywa mali zetu watanzania mali haswa pesa.
 
Kesi ya nyani anaizungumzia ngedere


Sent from my EyePhone
 
Da kweli uchafu wa mlisho unamfanya benja aonekane msafi!

Kweli mh benja utashuhudia mambo ya ajabu sana!

1. Utashuhudia ccm wakijipindua december
2. Nadhani utashudia ccm wakijipa matenda
 
Huyu kwenye utawala wake walimfavor mgeni dhidi ya mzawa katika ubinafsishaji wa Kilimanjaro hotel?

Kwake kila Mtanzania alikuwa akihoji chochote ni amesukumwa na wivu nani mvivu wa kufikiria.
 
Hata kama Mkapa alikuwa fisadi na kuanzisha AnBen Company akiwa Ikulu lakini hakuruhusu madudu tunayoyaona sasa ya udhaifu wa kiongozi na kulikuza ombwe la uongozi Tanzania. Alichukua hatua mara moja. Rekodi ya serikali ya Mkapa kiutendaji iko mbali sana ukilinganisha na hii ya Kikwete. Thibitisheni. kwa kutoa mfano wa sekta moja tu iliyostawi katika miaka 8 ya utawala (ambao hauwezi) wa Kikwete.
 
He is the one who starts to pull our nation buck,majanga yote yaliyoshamiri kwa sasa chanzo ni uongozi wake,asije jifanya kuhepa kivuli chake,yeye ndiye source kwa kuanzisha tabia ya kudharau WATANZANIA na kuziba masikio kutopokea ushauri.NA MBAYA ZAIDI MIKONO YAKE IMEJAA DAMU YA WAZANZIBAR.Sasa aona Taifa lazama anataka ruka kimanga.
 
This is becoming routine now. Kila rais mstaafu anataka tuamini yeye alikuwa tofauti saaana.

Granted, Mkapa alikuwa no-nonsense kwa mambo mengi ambayo Kikwete aliyakenulia, he also had a lot of issues.

So asitake kutufanya tuamini kwamba yeye alikuwa tofauti saaana.
 
Hivi huyo jamaa anaonge hivo wakati yeye ni mshauri wake na huyo ndo aliyeanza kubagua watanzania pale alipokuwa anapiga kampeni kwenye jimbo la joshua nasri,,uovu na ubaguzi umeanzia pale aliposema kwamba wanachama wa vyama pinzani ni mafedhuri,na je? Kama mutu unajiheshimu unaweza fanya upuuzi kama alivyofanya yeye.

Mkitaka kuona kwamba yeye hafai,muwekeni kwenye friji kama dakika tano na mumwambie atoe historia ya mwalimu nyerere alipokuwa anaumwa mpaka kufa,kama hajatoa jasho ka mvua ya mawe na kwikwi lenye njaa kali,,huyo mzee aende south africa alikoficha mali zetu akapumzike afie huko,si hatumtaki.
 
Tutamshukuru kwa kumwacha fastjet ili aiue na kuiondoa nyinyiem madarakani 2014/15 ..ila wote watapelekwa the hague 2016
 
Obama amebeba mzigo wa bush na ndio maana anaoneka rais mbovu katika wote marekani.
JK yamemkuta hayo hayo.
 
Huyu kwenye utawala wake walimfavor mgeni dhidi ya mzawa katika ubinafsishaji wa Kilimanjaro hotel?

Kwake kila Mtanzania alikuwa akihoji chochote ni amesukumwa na wivu na ni mvivu wa kufikiria.

Yako mambo ambayo Mkapa sijubaliani naye lakini usimsingizie mengine. He stood as a man, he spoke as a president and he acted as as a leader. Hakuwa nyoronyoro na mtu wa kulialia kama tuliyenaye sasa.

Ndiye aliyerejesha heshima ya mfanyakazi katika sekta ya umma. Ndiye aliyeboresha si maslahi yao tu bali hata mafao yao. Alipunguza deni la serikali na kukuza akiba ya taifa (si kama huyu kiwavi).

Hoja zenye mashiko alikuwa anazikubali katika utendeaji kazi.

Katika uongozi wake stability ya nchi ilikuwepo. Sema kama sasa kuna stability yoyote toa mfano mmoja tu.

Kwenye red hapo juu UMESEMA UONGO. Kukuonyesha namna uongo wako ulivyo nimebold key words zenye kuleta na kukuza uongo wako.
 
Huyu wa
1. Kiwira ndo anatamka haya?
2. Kujengewa hoteli za kitalii South Afrika na Barick Gold ndo anatamka haya?
3. Huyu wa acheni wivu wa kijinga kwa wawekezaji ndo anatamka haya?
4. Huyu anayejuwa kurusha/kurushiwa sturi ndo anatamka haya?
5. Huyu wa ......

pamoja na hayo nakusifu kwa kurudisha heshima ya kusoma iliyopotezwa na mzee ruksa... Kwa kupunguza percentage ya fedha iliyokuwa mikononi mwa watu au kwenye mzunguko
 
..one of the biggest mistakes alifanya Mkapa ni kumwachia nchi JK.....maana weaknesses nyingi za JK zilikua zinajulikana kwa hawa kina Mkapa kabla hata hawajaamua kumpa nchi JK....kwa maana ya kumpitisha kugombea urais...Ninaamini sana kuwa huko ccm kulikua na better candidate zaidi ya JK wakati huo...pamoja na kwamba huwa wanafanya lobbying za kuchafuana kupata candidates...i still believe Mkapa could have avoided this guy....if he had wanted......Sasa hivi its too late kwa Mkapa kulalamika.....the damage has already been done to TZ....na gharama yake ni haya yanayotokea TZ leo.....
 
..one of the biggest mistakes alifanya Mkapa ni kumwachia nchi JK.....maana weaknesses nyingi za JK zilikua zinajulikana kwa hawa kina Mkapa kabla hata hawajaamua kumpa nchi JK....kwa maana ya kumpitisha kugombea urais...Ninaamini sana kuwa huko ccm kulikua na better candidate zaidi ya JK wakati huo...pamoja na kwamba huwa wanafanya lobbying za kuchafuana kupata candidates...i still believe Mkapa could have avoided this guy....if he had wanted......Sasa hivi its too late kwa Mkapa kulalamika.....the damage has already been done to TZ....na gharama yake ni haya yanayotokea TZ leo.....

Hilo la kumwachia JK si la Mkapa pekee, bali la CCM kwa ujumla wao
 
Back
Top Bottom