Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,228
Mkapa na wasaidizi wake walifanya kazi yenye kuonekana pamoja na kuwa anayo mapungufu yake.Alipokea nchi ikiwa katika hali isiyoridhisha kiuchumi,tulikuwa hatukopesheki,hali duni sana ya wafanyakazi wa umma na sekta binafsi.
Mkapa na wasaidizi wake hakulalamikia utawala uliopita kabla yake,alipigana kiume.Alithibiti mfumuko wa bei na heshima ya mfanyakazi ilirejea.
Utawala wa Kikwete walipokea uongozi ktk hali ya kuridhisha ya uchumi.Miaka 8 uongozi wake hali imekuwa ni mbaya;uchumi mbovu,mfumuko mkubwa wa bei,mahusiano mabaya kijamii,usalama duni wa raia,elimu inazidi kudorora nk.Serikali inahangaika na CDM,pia kuhusisha udhaifu wao na uongozi wa awamu wa tatu.
Utawala wa mkapa ulihangaika na CUF, huku utawala wa kikwete ukihangaika na CDM wote walewale tu.Mkapa kajaribu kuiba kura Arumeru kwa Nassari akashindwa, igunga aliiba na ukatenguliwa.Hana confidence ya kuishi kimya kama kina CHISSANO ndiyo maana bado anahangaika na kuidhibiti CDM anajua fika wale wakitinga magogoni, yale yanayotokea Zambia na Malawi yatamkuta.The guy has no moral authority to comment on what he has done in Bukoba today