Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni. Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.

“Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,” alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.

Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.

“Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,” alisema.

Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.

Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na yale ya Kiislamu.

Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.

Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na Tunduma.

Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.

Namsifu sana Rais Mstaafu Baba Mkapa pamoja na ufisadi katika kipindi chake lakini alifanya mambo bwana! mrith wake kwa kweli kuna kazi ya kufanya kabisa. mimi binafsi sitachoka kumpongeza Mkapa kwa sababu kwanza alijua kutoa matamko makali na mambo yakaenda
 
Jitahidi na wewe mr clean kwenye taasisi unaziongoza usafishe udini ili viongozi wa kizazi kipya wakuelewe
 
Kuna taarifa kuwa Ikulu inahaha kusaka picha na sauti vilivyorekodiwa baada ya baadhi ya magazeti kumnukuu Mkapa akiponda Serikali ya JK wakati wa kusimikwa kwa Askofu Mpya kule Bukoba.Eti Mkuu wa Kaya haamini kama kilichoandikwa ndiyo ukweli na uwazi wa Ben
 
ASIHAE KUTAFUTA VIDEO, kwani hajui shein ana mamlaka makubwa kuliko yeye TZ ndio maana akaongoza mamia ya watu akiwamo kikwete katika siku ya karume day.
 
Tuwekeeni nasi tuthibitishe

ni kauli gan,tujuze na wengine tuweze kuichambua
aQCAAlS6sFpKYEzAAAAAElFTkSuQmCC

BuW4rbDxxrMFQ3cbTTU1NRiNBFHPtIEkGymqmaZHLpvCzqan0w3qClJX0NMZY8Rl+qTb3NLSYqLpRooiSfL0T2QgSWNjI9VkMtE03WymzWa62WyiawMNBsPptv+hfwGs0Ud0Wy8vPgAAAABJRU5ErkJggg==
 
Hivi kabisa huwa anakaa na kusema anafanya hata 1/8 ya BMW? sasa video ya nini wakati anajijua kabisa hakuna analolifanya
 
hiyo sauti anayo Ansibert nguromo kwenye you tube,wasipate shida sana kuitafuta!!ukweli unauma....
sent from nokia 3310.
 
​Kwani ni uwongo kuwa serikali imeshindwa kudhibiti wachochezi!?
 
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni. Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.

"Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.

Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.

"Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema.

Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.

Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na yale ya Kiislamu.

Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.

Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na Tunduma.

Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.
 
yeye aliposema katika awamu yake amejenga kilomita nyingi za lami kuliko awamu zote wakati in reality anamalizia barabara alizoanza Mkapa alidhani Ben hana Tv na redio nyumbani kwake!!alimsikia and he now returns the favour.
 
​Kwani ni uwongo kuwa serikali imeshindwa kudhibiti wachochezi!?

Kipindi kile serikali ya Mwalimu Nyerere(R.I.P.) ilikuwa inawapeleka vijijini na kuwafungia huko bila ya kuruhusiwa kutoka hao unaowaita wachochezi. Unataka na serikali ya dunia ya leo ifanye vivyo hivyo?

Bila shaka serikali hii ya leo ikifanya kama ile ya Mwalimu Nyerere wewe ndiyo utakuwa wa kwanza kulalamika serikali inakandamiza uhuru wa watu kujieleza.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ila kikwete ana IQ ndogo sana,napata mashaka hata hiyo elimu yake sijui kama sio ya kununua.

Wewe ambaye maisha yamekushinda na kazi hutaki kufanya unaishia kuja kulialia mitandaoni ndiye mwenye IQ kubwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Watanzania mtanikumbuka! By Benjamin William Mkapa 2005
 
ASIHAE KUTAFUTA VIDEO, kwani hajui shein ana mamlaka makubwa kuliko yeye TZ ndio maana akaongoza mamia ya watu akiwamo kikwete katika siku ya karume day.

Aisee mkuu tpmazembe, nilifurahi sana siku ya Karume Day na ninaipongeza Zanzibar kwa kujitambua. Hakika Zanzibar ni wakati wenu wa kuwa na nchi yenye mamlaka kwa jina mlitakalo ninyi, thenu kuwe na ya Muunganoa kama Wananchi wa Bara na Visiwani wataridhia (maana wa awali wa kulazimisha and was not participatory) halafu tuwe na Tanganyika yet. Bravo His Excellency Shein!!
 
J kikwete atakumbukwa daima kwa maovu yake anayofanya katka utawala wake wakisultani hapa tanzania.
 
Back
Top Bottom