Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

msichanganye mada, Mkapa yupo very specific kwa issue aliyozungumza na hapa hakuzungumzia swala la ufisadi,amesema katika uongozi wake ni kuwa hakuwahi kuambiwa anabagua watu kwa swala la dini nk nk!
kiufupi ni kwamba enzi hizo kulikua hakuna coverage kubwa ya media(mainstream media na social media).

Walimsema sana hasa kipindi ameua pale mwembechai,sema hakukua hata na jf kipindi hicho ambako mtu angetoa maoni na kama ilikuepo coverage ilikua ndogo sana.
 
Anacho jaribu kufanya ni kutakatisha makosa yake kama yeye alishindwa kumuenzi Nyerere akiwa hai alipo binafsisha NBC na KIWIRA na kurithia kuongeza mikataba ya TICTS kabla haijaisha anategemea nani atamuenzi marehemu yeye akae kimya ajilie bata maana hakuna wa kumhoji.
Rais Mstaafu Ben Mkapa amesema baada ya uongozi wake anashuhudia mambo mengi ya ajabu ikiwemo mitafaruku katika jamii.

Kwamba anachojivunia katika uongozi wake ni kuwa hakuwahi kuambiwa anabagua.

Amesema kizazi kipya cha uongozi kinatakiwa kurudi katika misingi aliyoacha Mwalimu Nyerere ambayo ni Amani na Utulivu.

Amesema hayo mjini Bukoba wakati akitoa salaamu baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katholiki la Bukoba Desidelius Rwoma aliyehamishwa kutoka Jimbo la Singida kuchukua na nafasi ya Askofu Nestory Timanywa aliyestaafu baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 39.
 
Ni kweli mitafaruki imekuwa mingi,kwafano CDM wanaendesha maandamano na mikesanyiko bila kibali,karibu mikoa yote na kusababisha mauaji mengi baada kukaidi amri za polisi,lkn hamna hukumu ya mahakama iliyatolewa zaidzaid wanaachiwa au kesi aziishi lkn cha ajabu kesi kama hizo kwa kwa waislam zimekwisha ndani ya wiki mwezi mmoja,na wamefungwa mwaka moja.tunajua kuna jamii zingine zitafurahia na nyingine zitalia sana lakini machozi yao hayataenda hivihivi.na wanajua na wanaakili.hizi ni zama zakujua mambo.
 
Mmmh Mkapa. Alikuwa na madudu mengi sana lakini aliyaficha chini ya uvungu wa utawala wa kidikiteta ambao aliutumia kwa kumtisha kila mtu alietaka kuuchokonowa utawala wake hata kama alikuwa mshirika wake katika kampeni ya kuwania Urais kama alivyokuwa swahiba wake mkubwa Generali Ulimwengu na alivyomfanya.

Kwa mfumo huu inawezekana yeye hakuona dosari nyingi za utawala wake likiwemo hili la dini kwa sababu watu hawakuwa na uhuru kumkosoa au kuonyesha hisia zao kwa njia yo yote ikiwemo za kijamii kama maandamano badala yake jamii ikawa inajenga chuki ya ndani kwa ndani.

Ukweli ni bomu la ubaguzi wa dini, kukuwa pengo kati ya aliyenacho na asiyenacho,ukosefu wa ajira kwa mamilioni ya vijana na ukosefu wa kazi kwa wananchi kutokana na mazingira duni kama hata mazao ya kilimo kokosa bei na kuwa hasara kwa wakulima, liliandaliwa katika kipindi chake cha udikiteta na watu kwa kuofia maisha yao wakanyamaza kimya yeye akajigamba kuwa alikuwa kiongozi mzuri kumbe.......

Hata wale wanaozungumzia uchumi kuwa alifanikiwa siyo kweli alichofanya Mkapa ni kumkamua ng'ombe maziwa asiyelishwa ni lazima siku moja atakufa kwa njaa tu, Mkapa alisimamia uchumi unaokua kwenye makaratasi na vyombo vya habari wa kupika ili CCM itowe matumaini kwa wananchi kama ya fisi usiku kufuata mkono wa binadamu unaotinga akidhani utaanguka hapa hapa au hapa hadi likamchea.

Ndivyo ilivyokuwa kwa uchumi wa makaratasi wa Mkapa yeye na wasaidizi wake walikuwa mabingwa kuwatuliza wananchi kwa madai uchumi unakuwa unakuwa lakini impact ya kukua kwa uchumi katika jamii haionekani kabisa wananchi wanapigika kweli kweli mazao ya kilimo hayanunuliki, viwanda vinauzwa na mbaya zaidi kili kilichokuwa kinapatikana kinachukuliwa na kikundi cha watu wachache kwa ubabe kweli.

Hebu fikiria alivyowaingiza Tanesco wale mafisadi kutoka Afrika ya kusini kwa mtutu wa bunduki wafanyakazi wa Tanesco waliyojaribu kukangamaa walifyata mkia kwa mtutu wa bunduki na Mkaburu akaingia Tanesco na Madhara yake wananchi yanawatesa mpaka leo huyo ni Mkapa.

Utawala wa Mkapa haukuwa na huruma na wananchi wala hakujua kuwa kuwa wanananchi anaowatawala au walimchagua na kumpa madaraka wanalala na njaa katika nchi ndiyo maana hakushaurika hakuambilika na kwake ye yote anaemshauri iwe kisiasa au kwa njia ya habari akimjua amekwisha ndiyo maana alihakikisha magazeti yote yaliyokuwa na mlengo wa kumpinga aliyauwa kwa kutoyapa matangazo.

Kwa udikiteta huu ndiyo maana aliweza kuyafanya mambo mengi machafu mazito huku wananchi wake wakishindwa hata kuuza korosho zao na kuwaacha wakitabika na kudhurumiwa na wahindi zao ambalo yeye ndilo lililomlea lakini hakujali.

Mkapa alimjua Kikwete kuwa ni dhaifu na kwa hiyo katika utawala wake atakosa ujasiri wa kupeleka mswaada bungeni wa kufuta kinga ya kutoshitakiwa Rais mstaafu na alimhofia Salm A. Salimu kuwa angekuwa na ujasiri huo ndiyo maana aliwageuka wenzake wa CC ya CCM na kumsukuma Kikwete kwa madhumuni hayo ya kumlinda na ndicho kilchopo sasa ndiyo maana anasema hayo.

Hata kauli yake hiyo aliyoitoa katika kipindi hiki tete katika taifa hili kati ya Wakristo na Waislam na yeye kuitolea Kanisani ni moja kwa moja ni ya uchochezi mkubwa ya unafiki na Rais aliyopo madarakani anapaswa kumuonya kwa sababu yeye Ben ni Mkristo Mkatoliki na amekwenda kutoa kauli hiyo katika dhehebu lake hii ina maana yeye katika kipindi chake aliwapenda na kule kutoka kwake ndiyo wakristo wanaonewa hii ni kauli ya hatari kutolewa na kiongozi kama huyo katika kipindi hiki ambacho serikali inakabiliana na changamoto hii ya amani na utulivu wa taifa.
 
Ni kweli Mkaps alizidi dharau kwa wasomi na jounalists wa ki TZ. Aliwaita wote wenye mitizamo tofauti naye ni' maprofesa na waandishi mchwara', watu wenyye wivu n.k. Bei ya kila kitu, hasa viwanja ilipa baada ya issue ya EPA. Lakini pamoja na haya yote, Kikwete ni dhaifu sana kiuongozi compared to Mkapa
 
Kwa hili la kujiunga OIC sipo nawe. Mbona Vatican wana ubalozi hapa Tz, Watz tulidhirikishwa ktk suala la kufungua ubalozi hapa ilhali Vatican inajulikana wazi ipo kwa maslahi ya wakatoliki. Huoni dini nyingine zinadhulumiwa kwa hili. Hebu acha udini wako mfilisika mkubwa wa tafakuri we.

Vatican City [SUP]i[/SUP]/ˈvætɨkən ˈsɪti/, or Vatican City State,[SUP][12][/SUP] in Italian officially Stato della Città del Vaticano (pronounced [ˈstaːto della t͡ʃitˈta del vatiˈkaːno]),[SUP][13][/SUP] is a landlockedsovereigncity-state whose territory consists of a walled enclave within the city ofRome. It has an area of approximately 44 hectares (110 acres), and a population of just over 800.[SUP][3][/SUP][SUP][14][/SUP] This makes Vatican City the smallest internationally recognized independent state in the world by both area and population.

Source: Vatican City - Wikipedia, the free encyclopedia

Vatican City has an autonomous government, complete with a national currency, post office and flag. The Catholic pope resides here as both a political and religious leader.

Do your homework!!!!!!!!!!!!
 
Acha upopo wako hapa. Dhaifu kaachiwa mzigo gani??? Kumbuka kwamba Mkapa kamwachia JK akiba ya kutosha tu. Yeye kaitapakanya na kuanza kuombaomba.

nafikiri hayo anayo yasema yangekuwa kweli kwa nijuavyo siasa za wenzetu obama asinge pita tena embu aache kuongelea swala ambalo hana hakika nalo..
 
Kweli nimeamini baadhi ya viongozi wetu ni wanafiki,hivi kweli leo hii huyu aliyekuwa kiongozi mkubwa wa nchi yetu ndio anaongea maneno kama haya?! Kiongozi mkubwa wa nchi anakuwa wa kwanza kuvunja sheria na katiba ya nchi kwa kufanya biashara akiwa ikulu halafu tunaambiwa hawezi shitakiwa eti kwa sababu alikuwa rais wa nchi.Baada ya kumaliza uongozi wake ana shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" .mwenyewe mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira. Natamani sana aondolewe kinga ya kutoshitakiwa kisha apandishwe kizimbani kujibu,damn!
 
Anajua pamoja na madudu mengi aliyofanya katika utawala lakini madudu ya mrithi wake ni mengi zaidi ndio maana akapata mshipa wa kusema hayo yote, ametenda yake anyamaze tu watz ndio tunajua tumuweke ktk fungu gani,naungana na mchangiaji mmoja aliyesema udhaifu wa JK ndio unamfanya Ben aonekane shujaa.
 
pamoja na kauli nzuri ya Rais mstafu nasikitika kusema kuwa hajatusaidia sana watanzania. kwanza yeye na chma tawala awanawajibika moja kwa moja kuusimika utawala anaoulalamikia na bahati mbaya hatujaona akiushauri kuenenda vyema. pili hata pale palipoonekana waziwazi makosa na hasa haya ya kuchovhea udini yakifanyika hakutyoa kauli. kwa mfano katika uchaguzi mdogo kule Igunga taasisi ya dcini iliposema waxiwaxi maxuala ya uchaguzi na kuhimiza watu wasichague chama fulani kwa misingi ya ufini, Rais mstaafu ambaye aliongoza kampeni ya chama chake hakutoa kauli yoyote kuashiria tatio la matendo hayo. na hii ni kwa sababu ilionekana kukisaidia chama chake!

je ni viongozi wapi wa kizazi kipya anaoongea Mheshimia Rais mstaafu? Maana ukiangalia safu ya iongozi waliopo serkalini ikiwemo na Rais wetu bado tunaona wazee waliolelewana Nyerere! Au hii ni katika kuandaa hoja ya kurejesha walioshindwa katikakipindfi kilichopia. ebu angalia kaujli zilizotolewa na Waziri Mkuu mstaafu (wa kipindi chake) na katibu mkuu mstaafu wa ilihokuwa OAU. Is thhis a coincifdence?
 
Huyu ndie alikuwa fisadi kaiba sana na mali za watanzania live. Leo anaishi kuula pesa za wizina familia yake. Huyu nae ni wa kufunguliwa mashtaka na kunyanganywa mali zetu watanzania mali haswa pesa.

aligeuza ikulu kua gulio kimyume na nyerere aliuza NBC kwa bei ya kutupa Nyerere alimkatza hakuelewa akijimilikisha mgodi bila haya ayo ni 3 kati ya mamiaya ufisadi alimwandalia Kikwete mazingira magum sana ya kudeal na mafisad wa nchi hii. na kama nchi lazima tutampeleka the hugue
 
Ni kweli mitafaruki imekuwa mingi,kwafano CDM wanaendesha maandamano na mikesanyiko bila kibali,karibu mikoa yote na kusababisha mauaji mengi baada kukaidi amri za polisi,lkn hamna hukumu ya mahakama iliyatolewa zaidzaid wanaachiwa au kesi aziishi lkn cha ajabu kesi kama hizo kwa kwa waislam zimekwisha ndani ya wiki mwezi mmoja,na wamefungwa mwaka moja.tunajua kuna jamii zingine zitafurahia na nyingine zitalia sana lakini machozi yao hayataenda hivihivi.na wanajua na wanaakili.hizi ni zama zakujua mambo.

We subiri ipo siko tutaheshimiana tu kama ilivyokuwa kwa rwanda sasa hivi.Wamezichapa na kuuana sasa hivi wanaheshimiana na maendeleo yanaonekana .Hawataki kusikia lakini ipo siku itaombwa nafasi ya suruhu halafu itakosekana.
 
kweli nimeamini baadhi ya viongozi wetu ni wanafiki,hivi kweli leo hii huyu aliyekuwa kiongozi mkubwa wa nchi yetu ndio anaongea maneno kama haya?! Kiongozi mkubwa wa nchi anakuwa wa kwanza kuvunja sheria na katiba ya nchi kwa kufanya biashara akiwa ikulu halafu tunaambiwa hawezi shitakiwa eti kwa sababu alikuwa rais wa nchi.baada ya kumaliza uongozi wake ana shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na waziri wake wa zamani wa nishati na madini daniel yona "mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira" .mwenyewe mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira. Natamani sana aondolewe kinga ya kutoshitakiwa kisha apandishwe kizimbani kujibu,damn!

hakika!
 
aligeuza ikulu kua gulio kimyume na nyerere aliuza NBC kwa bei ya kutupa Nyerere alimkatza hakuelewa akijimilikisha mgodi bila haya ayo ni 3 kati ya mamiaya ufisadi alimwandalia Kikwete mazingira magum sana ya kudeal na mafisad wa nchi hii. na kama nchi lazima tutampeleka the hugue

Mitaani wanasema hata kifo cha Nyerere kina mkono wake!
 
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni. Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.

"Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.

Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.

"Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii," alisema.

Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.

Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na yale ya Kiislamu.

Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.

Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na Tunduma.

Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.
 
Minaona tupigeni magoti tuswaaal.hatuna ujanja nch ishatekwa na kizaz cha .com
 
Huyo ndiye Mkapa ninayemfahamu! Hongera Mr Clean.

Huyu jamaa ni mr clean kweli maana kuna majizi mengine yamekamatwa red handed lakini mpaka leo hayataki kukubali. Huyu alivyobanwa kuhusu kiwira alikubali na akaomba radhi kisha akaurudisha mgodi kwa serikali. Hongera mr clean kama una vijisent kule uswis sio mbaya ukiturudishia. Mungu akubariki sanaaaa. wote semeni ameen
 
Back
Top Bottom