Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

R.I.P kwa ndugu zetu makamanda mliotangulia and get well soon kwa majeruhi.
 
Poleni sana makamanda! Pole sana Ben Saanane, Mungu Akupe faraja ya kweli na Amani katika kipindi hiki. Mungu Awapumzishe mahali pema makamanda waliotangulia na Awafariji wote walioguswa!
 
Last edited by a moderator:
Poleni Ben kwa kufiwa na marafiki zako,vifo vyote vibaya ila cha ajali kinatisha mno hasa kama umeshuhudia.
 
Kifo ni fundisho kwa sisi tuliobaki kujifunza na kumtambua mungu,pole sana Ben Saanane kwa kuondokewa.
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli PRADO siyo gari salama yaani kupoteza uelekeo ni haraka sana, mimi hii gari huwa sipendi kabisa kuendesha

unachosema inaweza ikawa kweli kabisa...zile gari kwa mtazamo ni kama nyembamba halafu zipo juu..
 
Ugua pole Ben Saanane, ingawa sikufahamu lakini kupitia JF nimeweza angalau kujua japo kidogo unachosimamia na hicho kidogo kimenipa faraja kwamba bado wapo vijana wazalendo ndani ya taifa hili. Pole sana kwa kuwapoteza rafiki zako na Mungu mwenye faraja akupe nguvu katika wakati huu mgumu, upone haraka ili uweze kuendelea na harakati zako za kimaendeleo kijamii, kisiasa na kiuchumi.
 
Last edited by a moderator:
Duh pole sana Ben na pole sana kwa wafiwa wote.

Mungu awarehemu wote, kweli kifo ni mtihani mkubwa mno. Mungu atujalie kumkumbuka tungali hai.
 
Mungu anakupenda Sana ndugu Ben. Ili uwepuke dhambi na kiama cha mwisho. Endelea vizuri?¡:
 
Poleni sana.

Dada hembu wafundishe hao kaka zako ifeero sijui na huyo mwingine msalani adabu maana naona wameamua kujitoa ufaahamu wape elimu dunia na akhera inaweza wavusha hapo walipo wana hali mbaya sana amini hivyo.
 
Inasikitisha sana

Pole Ben

Poleni ndugu wa marehemu.

RIP Marehemu Allan na Faith
 
Chuki za namna hii ni za ukada tu wa chama au na mambo binafsi? Kwa sababu najua kwenye siasa hicho kinachogombewa kikimalizika watu huanza tena kuchekeana. Lakini ikifikia mtu kutaka mwenzake afe au kumwua, basi huyo tena ana roho nyingine. Laiti watu wangejua kuna maisha baada ya haya iwe ni motoni au mbinguni.

Usipoteze muda na watu wenye umasikini wa kifikra na hapa leo wametudhihirishia kumbe huwa tunaongea na mapunguani si wazima hata kidogo amini hivyo.
 
Back
Top Bottom