Wanakwaya Jimbo Katoliki Bagamoyo wapata ajali mbaya Singida

Wanakwaya Jimbo Katoliki Bagamoyo wapata ajali mbaya Singida

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,926
Kwaya ya Damu Takatifu ya Yesu, Parokia ya Yohana Mtume na Mwinjili, Tegeta Jimbo Katoliki Bagamoyo wamepata Ajali Mbaya katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida walipokuwa wakielekea Jimbo Katoliki Singida kwa ajili ya Ziara ya Uinjilishaji.

Hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kufuatia ajali hiyo, zaidi ya majeruhi kadhaa ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo vya afya vilivopo Wilayani humo. Tuendelee kuwaombea Majeruhi wote uponyaji wa haraka na moyo mkuu wa kutokata tamaa katika safari hii ya Uinjilishaji kwa njia ya Uimbaji, licha ya mashaka makubwa yatokanayo na tukio hili.

Bikira Maria salama ya Wagonjwa, Utuombee!

Screenshot 2026-07-02 230316.png
 
View attachment 3620885
🙏
 
Pole nyingi kwao, furaha yetu wote watoke salama .
Ni bahati mbaya sana, bahati mbaya vyombo vyetu vya usafiri hitimisho la usahihi la usalama wa safari hivyo kila hatua tumuombe mwenyezi Mungu kwa wingi wa huruma yake na upendo wake atutangulie.

Ila binafsi nimekuwa na maulizo mengi sana juu ya hizi safari za kidini, huwa ,zina gharama kubwa sana kuzifanikisha.
Iwe ni makongamano, semina , warsha, ziara za kitume , kwaya nk.
Tunakuwa tunachangishwa michango huko kanisani kwa nguvu nyingi na bila hiana tunatoa na kufanikisha mpango mzima,

Vile vile tunachangishwa sana kwenye ujenzi na vifaa kwa hajili ya huduma za kikanisa na kweli tunafanikisha.

Jimbo hilo hilo la Morogoro kanisani kwetu tumekuwa na michango kadhaa ya ujenzi na mengine zaidi ya billion na imefanikiwa na bado tunaendelea kuchangia.

Ni katika jamii hio hio kuna watoto wanakosa ada, kuna watu wanakosa matibabu, kuna watu hawana makazi , kuna watu wana madeni makubwa , kuna wengine hawana mtaji wengine hawajui wata kula nini ama kuvaa nini !

akuna hata mmoja mmoja katika viongozi ameitisha mchango kwa ajili huduma kwa muumini na jamii kwa ujumla, ila matamasha , makongamano semina na ziara kama hizi ni milions of money zinachangw lakini hatua chache na hapo kanisani kuna familia inalala na njaa.

Mungu ni mwema .
 
Poleni sana wanakwaya ila naona School basi nayo hapo ,kwani walipanda School bus? Naona kama mara ya pili kwaya ya TEGETA wanapata ajali.
 
Poleni sana wanakwaya.

Tegeta to Singida na school bus nadhani shida ilianzia hapo. Kuna masuala ya kujiuliza na kujifunza pamoja na kuwa siku zote ajali haina kinga.
1. Huyo dereva ni mzoefu wa safari ndefu?
2. Je huyo dereva alikuwa anaijua hiyo ruti vizuri kabla ya luanza safari?
2. Je hilo basi lilikaguliwa vizuri na wataalamu kabla ya kuanza safari?
3. Je dereva alipumzika vizuri siku moja kabla ya safari - yaani hakuwa na uchovu wowote?

Ushauri wangu wa bure kwa kanisa katoliki. Siku nyingine msiwe mnaruhusu safari ndefu kama hizo kwa vyombo vya usafiri ambavyo vinaonekana kabisa ni kwa ajili ya safari fupi. Kama michango haijatosha ni bora kuaihirisha safari kabisa. Ni vyema basi kukikwa na safari ndefu kama hizo ni bora mara mia wakakodisha mabasi makubwa pake Ubungo/shekilango kuliko kutumia school bus kama hiyo inayoonekana pichani. Safari ya Tegeta - Singida sio sawa na safari ya Tegeta - Visiga.

Mungu awape nguvu majeruhi wote mpate nafuu na kupona haraka mrudi kwenye majukumu yenu.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom