Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

bora kangekufa hako kanafki kameshiriki mipango mingi ya mauji ndani ya chadema
c.c.madema b

Duh! Jamani ni mtu mwenye roho ya namna gani anayeweza kuzungumza maneno ya namna hii wakati wa ajali? Bila shaka atakuwa mchawi. Chuki nyingine hazifai kabisa.
 
Pole sana Ben, poleni sana familia za marehemu. RIP Allan and Faith
 
Tayari miili ya marehemu ipo mochwari muhimbili.... Na Ben karuhusiwa kuendelea na pumziko akiwa nyumbani... Mungu kaumba vitu vyote lakn binadamu kaumbika sana.... Inatia huruma
Ajali ya kupanga ile. (Rest in peace marehemu) yaani watu wamekufa wengine hata kukwaruzwa?
 
Soooo sad. Poleni sana makamanda. Mpone haraka tunawaombea.
 
Ajali ya kupanga ile. (Rest in peace marehemu) yaani watu wamekufa wengine hata kukwaruzwa?

Mimi huwa naamini humu duniani huwa kuna binaaadamu wanaishi pamoja na mapepo yanaishi sijui wewe upo kwenye hilo kundi la pili ama manake wewe si bure una pepo njoo ufanyiwe maombi kabla hujawa mento fresh
 
Kwa sababu uovu wenu umefanikiwa?

Mkuu niombe msamaha hukujua namaanisha nini kuandika hivyo binafsi nimesikitishwa sana. Nimeandika maandishi machache lakini kwa wenye kuelewa wanaweza elewa.
 
Hakika kifo ni siri kubwa sana aliyotuwekea Mwenyezi Mungu na ili kutukumbusha wanadamu kuwa tayari kwa vile hakuna ajuwaye sasa wala wakati Mwana wa Adamu atakuja kunyakuwa kilicho chake fay na allen wamepumzika Mungu awarehemu Mtihani unabaki kwetu sisi tuliobaki ni nani kati yetu anayejua salio la maisha yake lililobaki hapa duniani ? Basi tutiane moyo wapendwa tusichoke kusali kwa vile hakuna ajuaye siku wala saa tuwe tayari muda wote Mwenyezi Mungu awatie nguvu wafiwa na marafiki woote wa wapendwa waliotutangulia nasi tukijua tupo nyuma yao.
 
Lol! Habari mbaya sana hii jamani.....mwenyenzi Mungu awaguse wote wapone mapema waweze kupambana na mafisadi!

Jamani hivi vifupisho vya maneno ya kwenye mtandao tuvisome na kuvielewa, unaandikaje 'Lol!' kwenye habari mbaya kama hii?
Poleni majeruhi, Mungu awafariji wafiwa
 
Duh! Jamani ni mtu mwenye roho ya namna gani anayeweza kuzungumza maneno ya namna hii wakati wa ajali? Bila shaka atakuwa mchawi. Chuki nyingine hazifai kabisa.

Usione binadamu tunakutana nao tunaishi nao lakini wengine wana roho mbaya kupindukia, ni bora hata wachawi. Mwanasiasa au mwanachama wa chama chochote anaejua nini maana ya siasa huwa likitokea tatizo la upande wa pili anaacha tofauti zilizopo na kuungana kuwa kitu kimoja kwa mda ule...
 
quote_icon.png
By LiverpoolFC
Lol! Habari mbaya sana hii jamani.....mwenyenzi Mungu awaguse wote wapone mapema waweze kupambana na mafisadi!
laughing out loud...usiandike vitu usivyovielewa vizuri.
 
Pole kwa wote waliopatwa na msiba huu!!!
Mungu aendelee kulinda waja wake!!

Pole sana Ben Saanane, uchungu huo uwe chachu ya malengo mliyoweka pamoja na rafiki hao waliotangulia, wamekuachia deni kubwa la kutekeleza hayo!!!
Naamini utaweza na Mungu akubariki kwa msimamo huo juu ya maazimio yenu!!!

Aamin
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom