Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

hahahahaaaaah Mungu yu pamoja na CHADEMA, makapi yoote yanaanza kuanikizwa hadharani, na kuna andiko lasema , atawapiganisha adui zako........!
 
Duhh ndio maana Zitto alisema swala la kuuana,Kumbe ni kweli.Nilikua nampuuzia TUNTEMEKE alipokuwa anasema Ben saanane ni jasusi wa kimataifa.Kumbe Lol
SERIKALI IPO WAPI ???kijana huyu ni haramu

Mkuu, kunani? Mbona unaji-quote mwenyewe???
Au ndiyo kupitiliza kwa ushabiki na mapenzi ya unachokitetea?

Kulingana na maandiko yako na unavyojibu hoja za JF kuhusiana na mada hii, unaonesha kabisa kwamba wewe ni wa kundi la Bw. Machange and Co.

Inasikitisha sana kuona vijana ambao ndio tegemeo la maendeleo ya taifa wakilumbana kwa hoja mufilisi zisizojenga ndani ya JF.

Kwa maoni yangu, huyo Saanane amewapiga bao la kisigino kwa kitendo chake cha kukiri makosa yake na kuomba msamaha.
Ameonesha uungwana tofauti na ninyi ambao mnadai kufahamu makosa lukuki ya bw. Saanane lakini hamkuyatolea taarifa pahala popote, si ndani ya chama chenu wala kwa vyombo vya usalama, hususan hilo la kukamatwa akitaka kumdhuru Mhe. Zitto.

Mtaandika mengi na utetezi wa kila aina, lakini kwa werevu watajua kwamba ni harakati za mfa maji tu.
 

hamjajibu ata hoja moja ya ben,mnachofanya ni kumshambulia tu...au tupigie mstari alichokisema???
 
I'M TOTALLY CONFUSED

Hoja za hawa jamaa ni nzito sana

Naomba mwana JF yeyote ACHAMBUE hizo hoja na atupe analysis ukweli mzigo wa ushahidi unaelemea kwa nani




Nahisi kuna ukweli wa kitu fulani miongoni mwa hoja za ZITTO, BENN, MACHANGE, na MAMUYA


 

Sikupenda kuingia tena katika majadiliano haya zaidi ya kusubiri vikao vya Chama.Kwa kuwa kundi hili linaendeleza mjadala na upotoshaji wa pale alipoishia kiongozi wa kundi nimeona si vyema kukaa kimya.Mchange anasema hakuwa wa kwanza kunitafuta mimi as if hii ni hoja ya Msingi sana.Hata Zitto sikuanza kumtafuta mimi ila yeye hasa baaada ya kuenguliwa uchaguzi wa BAVICHA.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yake ya kwanza yakiwemo ya tarehe 29/05/2011 siku iliyofuata baada ya kuenguliwa BAVICHA.

Kwanza NI KWELI kundi hili la PM7 lilikuwepo.Ni kweli tulishirikana kaktika mpango huu.Kwanza jina PM7 ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa miongoni mwa majina mengine.E-Mail aliyotuma Mchange hapo juu ni e-mail ambayo nilimtumia Zitto Kabwe na tulikubakliana mimi na yeye isajiliwe taasisi ambayo tutakua tukiendesha harakati bila kujipambanua waziwazi na malengo ya taasisi hiyo.Lengo kuu la Taasisi hii lilikua ni kuanzisha vuguvugu la vijana na kulitumia kama platform ya kisiasa na kijamii ambayo ingekuwa non-partisan baada ya taasisi ya ADO kutokuwa active.Pia ingekuwa taasisi ambayo ingefanya harakati za baraza huru la vijana.Zitto alipokea wazo hili kwa furaha.Hata hivyo lengo la Taasisi lilibadilika na kuwa na malengo ya kisiasa ndani ya chama na wakati huo huo tukitafuta njia ya kubeba kundi la masalia kisiasa.Zitto alikuwa ameshaanza kuzunguika na kundi hili kwenye mikutano ya hadhara mikoani.Mimi ndiye niliye-draft contents zote ambazo hata hivyo Mchange hajathubutu kuziweka zote hapa.Tulitohoa jina la PM kutoka katika taasisi hiyo niliyoipa jina la Youths Patriotic Movement

Ninayo mawasiliano yangu na Zitto kuhusu kundi hili na alinihimiza wakati huo akiwa Songea kwenye kampeni za udiwani kwenye chaguzi ndogo za udiwani akiwa na akina mwampamba na Shonza.Tulikubaliana kwamba hii taasisi isajiliwe haraka sana iwezekanavyo namnukuuu YPM MUST BE REGISTERED SOON AND GO COUNTRYWIDE mwisho wa kunukuu.Ndugu Zitto,bila shaka anaweza kuthibitisha hili

Nikiwa Geita wanachama wa kundi la Masalia walikua wakinipigia simu mara kwa mara na hata Message za kunitaka nirudi Dar haraka hata kwa muda mfupi tu tuweke mipango ya kuanzisha kundi hili pamoja na kufungua bank account.Tarehe 01/05/2012 nilifika Dar es Salaam kikazi. Siku hiyo hiyo tulikutana na Habib mchange,Mtela mwampamba,Juliana shonza na Festo Sanga pale Lunch time hotel.Siku hii ndiyo niliyotambulishwa kwa Festo Sanga. Wote walikua na shauku ya kupata mawazo yangu kwa kuwa zitto alishawadokeza juu ya mkakati huu hasa baada ya kikao cha kamati kuu.Nadhani ilikua ni matokeo ya kikao cha kamati kuu na mambo yaliyotokea humo ambayo sitaki kuyaandika hapa kwa sababu ni siri za vikao.

Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua
-David Kafulila
-Mwigulu Nchemba
-Deo Filikunjombe
Na baadhi ya wafanyabiashara

draft niliyoandika ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wale ambao walikua potential donors.

Pia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili.Zitto alisafiri siku hiyo bila kutuambia na tulilalmika sana sana.Baada ya hapo alikua akiwasiliana na mtu mmoja mmoja.Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi.Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA,Mchange-Mdude,Shonza-Benazir,Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au Dogo

Role yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha.Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chama.

Shonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA.Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti,Mwampamba Katibu,Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba.tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika.sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matatani

Hata hivyo baadae nilikubali na niliandaa bajeti ya Sh.25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.
Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao.PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama.Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7.Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati.Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri

Actually,niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki,nilikutana na Dr.Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili.Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji.Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu.Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi,yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana.Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese,Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&.Kwa bahati nzuri shonza,Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu.Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo.uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili

Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila.ilikua Tarehe 4/07/2012.Tulikutana Tamal Hotel.Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA,tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu.Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane.nilimwambia nitafikiria.Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile.Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto.Tulipanga kukutana siku iliyofuata.Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza.Siku hii mchange hakuwepo

Tarehe 7/07/20012 nilikua ndani ya Ofisi ya CHAUMMA.Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati.Mingine sitaiandika hapa kwa sasa.walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway.Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively.Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM.MAliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa.Kafulila anaweza kuthibitisha hili.

Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7.Hapa Dr.Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA.Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA.Nilikua nikifahamiana naye hapo kabla.Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa .Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password.Kafulila alitaka nimpe paswd yeye,Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi.Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA.Alitaka tuende kimya kimya.Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE..Nitaendelea....
 
Duh! I am confused as confused can be!

You people need to grow up.
 
Sasa mkuu wangu, hiyo e-mail ya Saanane aliyokutumia wewe nawe ukaamua kutuwekea humu JF katika kuongezea uzito wa hoja ya mada yako ina kasoro gani?

Kwangu mimi naiona ni ya mzalendo, mwana harakati ambaye amechoshwa na umaskini wa nchi yake (TZ) ambao unaepukika lakini unaoletwa na viongozi wasiowajibika na wabinafsi kwa muono wake.

Sioni madhara yoyote wala sijaona usaliti wowote wa ujumbe huu kwa CHADEMA, labda kwa kuwa hicho ki-inglishi sikijui vizuri. Lakini nadhani ni cha kawaida sana ambacho nimediriki kukisoma bila kuhitaji usaidizi wa kamusi.

Kama ushahidi wenyewe wa usaliti ndio huu, mkuu, naomba ukajipime upya uwezo wako wa kuwa mwanasiasa. Yawezekana umevamia fani usiyokuwa na wito nayo.
 
Hauna haja ya kuendelea,wakati tushakujua wewe ni mnafiki mkubwa,subiri ndoa,yako pia yataletwa na hao wenzako.
 

mkuu kwenye blue na taswira is one and the same rat
 
Ben Saanane;

Ni Kheri uweke tu kila kitu wazi kwani hakika mambo ni mengi sana miongoni mwetu humu jamvini!


Mchange
TUNTEMEKE
Ben Saanane

Hakika nawaambieni ya kwamba nina hofu hata mpaka sasa mu pamoja na Zitto

Fungukeni tuwasikie! Kha ha ha ha ha haaaaa!
 
Last edited by a moderator:
Kaaaazi kweli kweli. Naona Ben anafunguka hapa. Sijaona aliyefanikiwa kumshinda kwa hoja.

Tuendelee......
 

True dat bro,
 

Tama ni kweli mkuu basi TISS yetu ina watu ambao hawatakiwi kuwa huko kabisa.
 

this is getting interesting and sexy..mkuu ben ianzishie thread hii kitu...kuiweka chini ya thread ya huyu m.bwiga mchange ni kumpa promo
 
WAKUU MNAUWEKA SANA KWENYE HUU UZI, SHONZA KASHAANZISHA UZI MWINGINE TUNAHITAJIKA TUKAMUUNGE MKONO OOH! MWAKA WA MAVUNO HUU WATU WAPO KAZINI KUTEKELEZA KAZI WALIZOPEWA! HAYA TWENDENI...

2[h=2]
Udhibitisho wa kazi maalumu ya ben saanane na hujuma za dr.slaa kwenye siasa za juliana shonza[/h]
Ndugu wana jf,
nimepokea kwa masikitiko makubwa kashfa zinazoenezwa dhidi yangu juu ya yale yaliyoandikwa na exaud mamuya na ben saanane kuhusu mimi kama mmoja wapo wa kundi la masalia kutumika na zitto kuwachafua viongozi wa chama pamoja nakuratibu mipango[movement]ya kuhujumu chama.

Ndugu wana jf, nimewaunganisha wote kwa maana ya ben na mamuya kwasababu ni dhahili kabisa kwamba lao ni moja,wamelenga kunichafua mimi na wenzangu mchange,mwampamba,gwakisa ,sanga akiwemo kiongozi mwandamizi wa chama naibu katibu mkuu ,na mbunge mh Zitto Zubery kabwe.Huku wakimtuhumu zitto kuwa ndiye mmiliki wa masalia katika harakati za kuhujumu chama na kuwachafua viongozi mtandaoni.


Ndugu wana jf,sio mala ya kwanza majina haya kuandikwa vibaya mtandaoni na watu ambao wamekuwa wakijificha sura zao kwa kuvaa vinyago[mask]wakidhani kwamba hawafahamiki.
Kabla sijaanza kujibu hoja za ben na mamuya niweke wazi kwamba zitto ni kiongozi wangu,Namheshimu kabisa kabisa kama ninavyo mheshimu mbowe na slaa na wengine wote ndani na nje ya chama.

Ndugu wana jf,hoja alizotoa mamuya dhidi yangu ni hoja zisizo na mashiko yoyote kwa mstakabali wa vijana,chama na taifa kwa ujumla ,maana ni hoja mufitini,ambazo zimelenga kuwagawa baadhi ya vijana waonekane kwamba wao ndio bora zaidi ya wenzao huku wakiwachafua wenzao kwa majina mbalimbali kama vile mamluki,wasaliti na masalia.
Exaud mamuya naweza kumuelezea kwamba ni kijana ambaye akili yake haijiongezi,asiye na msimamo,mkurupukaji,na mpika majungu .katika kuthibitisha hili mamuya atakumbuka kipindi cha uchaguzi wa bavicha alipokuwa anagombea nafasi ya naibu katibu mkuu bavicha alinipigia simu akiniomba tushirikiane ashinde kwakuwa ametelekezwa na viongozi wakuu wa chama na Godbless Lema baada yakugundua kuwa kawasaliti na kuhamia kambi ya zitto.Akajinadi kwamba ni kweli amehamia kambi ya zitto.kwakuwa mimi si mnafiki kama alivyodhani majibu niliyomjibu najua anayakumbuka na matokeo yake aliyapata Dodoma baada yakujikuta umeambulia kura sifuri.

Exaud Mamuya
nikwambie wazi kwamba huna dira maana umechagua kufanya siasa za majitaka ,Napata shida kidogo nikifikiria wapi hasa umetoa ujasiri wakumzushia zitto maneno ya uwongo pamoja na hao mnaowaita masalia.kama suala ni kundi la zitto basi lazima kuna uwepo wa kundi jingine ambalo wewe unapigania maslahi yake ukiwa kama muumini wa kundi hilo.
Wewe sio wa saizi yangu,endelea kutuita masalia jina la kubenea kupitia mwanahalisi .
BEN SAANANE
​
Huyu namfahamu kama kijana wa chadema japo sijawahi kumuona kwenye shughuli yoyote ya kujenga chama zaidi ya kubomoa na kufitinisha viongozi na wanachama kama alivyofanya kutimiza matakwa ya maboss wake.
Swali.Kama kuna yeyote amewahi muona ben saanane kwenye kazi za chama yoyote ile ya shina au ta kitaifa aje hapa na ushaidi wake.

Shutuma ulizozielekeza kwangu kwamba tulikaa kikao chakujadili kwenda kula kiapo kwa waganga.Ben ni wapi tulikaa kujadili suala la kwenda kwa waganga?Nakana wazi kwamba hakuna kikao chochote nilichokaa na wewe nikakuunga mkono suala la kutokwenda kwa waganga au kwenda.Wewe ni mwongo unapaswa kupuuzwa maana shughuli yako imejionyesha wazi kwamba una lengo mahususina sio kujenga chama na ndio maana hujawahi kuonekana kwenye shughuli za ujenzi wa chama zaidi yakuzunguka kwenye mahotel kufanya vikao na ndugu zako kupitia ruzuku ya chama unayolipwa pale makao makuu.

Ben saanane katika kukutana kwangu mm na wewe hakuna siku tuliyowahi zungumzia,au mhusisha Zitto na swala lolote la kuharibu au kuhujumu chama zaidi ya kumsifia kwamba ni kiongozi anayefaa kuigwa ndani ya chama.
Nina ushahidi wakutosha kwamba ben saanane analipwa na chama cha chadema na yupo kwenye payrol ya chama kila mwezi kwa kazi hii ya kumchafua zitto kabwe na kufanya kazi ya kijasusi ndani ya chama.(nipo tayari kuwasilisha udhibitisho huu mbele ya chama)
NAMNA DR SLAA ANAVYONIHUJUMU KISIASA.
​
​



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…