Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Afu hivi vijamaa vyote vimejiunga jf juzi! kutuhadaa hamtaweza kamwe..dont 4gt hii site ni home of great thinkers! mnavyosema watu wanavifikiria ati...
 
"wazimu wangu ukinipanda hata nguo ntavua"
wanaitikia : "vua"
" nivue muone"
wanaitikia : "vua"

hii nyimbo ya watu wa tanga inanikumbusha mengi leo
 
Natoka Kigoma... Nimeaga kwetu... Nitakufa kwa amri ya Mungu... Siogopi kufa. ..Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. (Zotto Kabwe - Mbunge Wa Kigoma Kas 2012).
 
hata kama hawakutumwa na chadema lakini maadam ni viongozi wachadema basi wanaidhalilisha chadema.wewe huoni mafisadi wanavyoidhalilisha ccm japo hawajatumwa na ccm?

acha kuzuga basi .......unafikiri tumesahau vimemo alivyo andika katibu mkuu wa ccm mangula kwenda bank kuu kwa balali mwaka ule kaa pembeni usitukumbushe mengine hii ni kuhusu ufisadi kupitia green tang na kag
 
Naamini baada ya kusherehekea ushindi wa Lema, CHADEMA lazima watakuja na tamko rasmi baada ya vikao halali ili kumaliza hili gogoro la vijana. Nadhani kuna mengi yanaendelea nyuma ya pazia ambayo kwa sisi tusio karibu na jiko la CHADEMA hatuwezi kujua.
Tumaini Makene na Michael Aweda huwa wanajitahidi sana kuleta majibu na matamko ya chama apa JF. Ukimya wao kwenye haya ya Masalia ya Bavicha na MP7 ni dalili tosha kuwa kuna vikao vingi vinaendelea huko jikoni.

lets wait and see
 
Sasa nimeelewa kwamba ,kikundi cha masalia kilikuwepo , na kilikuwa na lengo la kukidhoofisha chama na kiliundwa na Mwampamba, Juliana,Machange na kundi lao la Masalia. Bali Saanane na Mamuya walikuwa wanatumika kama Intellijensia ya chama, hawa ndiyo walikuwa wanatoa taarifa kwa uwongozi wa juu wa chama kwamba nani ni msaliti , Wenyewe masalia hawakulielewa hili walifikiri Saanane na Mamuya ni wenzao kumbe walikuwa shushu, nina Uhakika Saanane na Mamuya walichukua form za kugombea uongozi bavicha ,walikuwa wanazuga ili kutambua wanaoenda kinyume na ni wakina nani , nafikiri walifanikiwa kuwajua na kuwaripoti kwenye uongozi wa juu wa chama, ndio uongozi wa juu wa chama ukawaengua baadhi ya wagombea kwa kashfa ya Rushwa kazi aliyo ifanya Saanane na Mamuya .

ukitaka kudhibitsha hilo utakugundua kwamba mkuu Saanane alikuwa anajipendekeza kwa masalia ili kujua mipango yao yote ,na akishajua anailipoti kwenye uongozi wa juu, ndio maaana uongozi wa juu ulikuwa unachukua Taadhari juu ya vijana masalia , kiasi kwamba vijana Masalia walikuwa wanaona wanatengwa , sababu walikuwa hawaijui.kumbe ni matendo yao . yliyokuwa ynaripotiwa na Mkuu Saanane na Mamuya. Saanane amefanyakazi ya Intellejensia vilivyo.

kama ni kweli Masalia walikuwa na lengo zuri kwa nini ,wameanza kufumuka baada ya Saa nane kuweka Mambo hadharani? walitakiwa watoe ripoti juu ya hili kwenye uongozi wa chama.kitambo tu kama walikuwa na nia njema. ukisoma maelezo ya Mwampamba na Juliana utagundua kwamba hawa watu walikuwa wana fadhiliwa na Zitto wakishilikiana na kafulila, wakati huohuo walikuwa wanajua kwamba Saanane ni mwenzao, kumbe alikuwa anawapeleleza.


kila mtu angependa role model wake awe raisi lakini sio kwa njia za kinafiki na uzandiki ,mimi Role model wangu ni Profesa Safari , ningependa awe raisi lakini sio kwa manufaa binafsi ni kwa manufaa ya chama , haina haja ya kuleta unafiki , na kutumia shortcuts kila mtu ajipange Chama kimpe baraka agombee lakini sio kwa kutumia unafiki, uzindaki ,uchawi . Siiungi Mkono kundi bali naunga mkono Maslai ya chama. Mwampamba na juliana shonza hamjakomaa bado,nyinyi na akina nape naona muko sawa . Mkuu Zitto nakuheshimu sana najua wewe ni jembe,lakini kuwa mvumilivu mvumilivu hula mbivu waangalie vijana wenzako Mnyika, Lissu ,Sillnde ,Msigwa, Vincent nyerere, Mdee, wanajenga chama , Achana na Kafurila hayapo kundini alishaondoka chadema zamaini, Achana na akina Shyrose Bhanji,achana na JK, achana na Wasira ungana viongozi wenzako wa JUU MBOWE na DR. Slaa mujenge Chama ,Unafiki hautakiwi. Watanzania tunakuamini kwamba ni kijana Tunaekutegemea baadaye kama kiongozi wa chini Lakini kwa sasa sifa zako zinapungua ,zinahamia kwa Mnyika ,Vincent Nyerere na Msigwa. Achana na Propaganda za ccm na NCCR ,kijenge chama mkuu. waambie wakina Mwampamba na Juliana waache Siasa za Maji taka Warudi kwenye mstarii wakijenge Chama.
Najua Dr. Kitila aliingia Kwenye Mkumbo bila yeye kujua, Nina uhakika kwa sasa ameshajua kwamba alikuwa anakitumikia chama au Mtu. na atajirekebisha


Mimi kila siku nabishana na Tuntemeke humu ndani JF kumbe nabishana na kundi la watu?
Kuna watu walikuwa wanamponda DR. Slaa nilifikiri ni magamba kumbe ni wanachadema wenzetu, hatari sana.


Tuache Siasa chafu Tukijenge Chama, "Maslahi ya Chama mbele"


jangakuu@yahoo.com

mkuu unawezakua GREAT THINKER!
 
you know what!!! ili kuondoa hii hadithi ya kulaumiana na kushtakiana....please viongozi wa juu wa chadema....i mean the chairman Mbowe.....na wale wazee wenye busara...kina Prof.Baregu, Dr.Kitila, Prof.Safari, Marando....hata kina Lissu na Mnyika...vijana kwa wazee in short...ebu waiteni hawa vijana woote wenye matatizo....wajieleze live....bila kujificha nyuma ya keyboards......itisha hawa woote kina Ben Saanane, Mchage,Mwampamba,yule dada Shonza na Zitto....hata Dr.Slaa ahojiwe kijulikane...maana nae anatajwatajwa sana hapa...wote hawa waitwe wawekwe kitu moto...waseme wanachokisema hapa....alafu ajulikane mnafiki nani...maana wanataka kuua chama hawa vijana.....Sasa hivi watu wanafurahia ushindi wa Lema......yaani ongezeko la nguvu ya chama.....alafu hawa majamaa wao wanasemana kwenye mitandao......NINGEKUWA KIONGOZI WAO NINGEADHIBU WOTE HAWA......HATA KAMA MTU NI KIONGOZI.....Its high time now for big time action against these hypocrites.....
 
Mjinga akifanya ujinga. kila mwenye akili anajua ukweli. kujisafisha hakusaidii. mchange uwongo umezidi.
 
Mjadala huu napenda uwe chachu kuelekea kushikana mikono kwa hawa vijana ambao wamekua wakichafuana na kukichafua chama na viongozi kwa ujumla.

Napenda usaulishe vidondo vyote vilivyotokea wakiitwa meza moja moja wasiwe na chuki wala uhasama bahati mbaya sana leo sikumuona ben mahakamani ningemuona ningempa huu ushauri nakumbuka alikuja na bandiko la wasaliti wote wafukuzwe ndani ya chama nilimpinga kwa hoja kwamba nisingependa hawa vijana wafukuzwe bali waitwe wawekwe chini wamalizwe.

Sasa ukaja huu utoto wamechafuana wewe lakini wamekipa chama damage kubwa tukubali tukatane sio leo wala kesho kutwa damage hii itaondoka niseme wazi tusiitane wasaliti ndani ya chama kama kweli hawa vijana wana nia ya kuendelea waombe msamaha wasamehewe wachukuliwe kama vijana ambao wengi hawajafika 30 wako kwenye mihemuko ya ujana.


Wengi hatujamjua vizuri Zitto:
Niweke wazi nishafanya mijadala ya wazi kwenye twitter na mh zitto mingi ilikua ya kujenga nchi kuona wapi tunafika zaidi ya hapa tulipo sasa kumuita zitto msaliti bado tunakosea sana wana chadema kwanini leo ndo akisaliti chama wakati alikitumikia miaka yote hiyo ya mwanzo kabla hajawa mbunge bila kukisaliti.

Tuwe wakweli bila baadhi ya michango ya zitto chama kisingekuwa hapa kilipo hata siku chama kishika madaraka atakua ameplay part kubwa sana kuanzia kwenye operation sangara mbona alishiriki hakukua na maneno.Najiuliza kitu zitto ameulizwa kuhusu kushiriki M4C amesema amepangiwa kanda ya Singida muda wake haujafika kwenda hiyo kanda ukifika atakwenda ni zitto huyu aliyeenda Rombo kwenye uchaguzi wa udiwani ni Zito huyu aliyeenda Karatu ni zitto huyu huyu aliyeenda Tanga kwenye operation ya Katani.

Hoja za ben saanane kwa zitto kuwa ni msaliti kupita kikundi chao inavyoonyesha ben alikua na mawasiliano ya simu tu na zitto na hata kwenye msg zinaonyesha zitto angekuwa na msaidizi ya kuweza kuzijenga sera za chama Chauma kwenye gas na mafuta tunajua zitto hakufurahi kufukuzwa kwa kafulila na vijana wenzake tulipoteza seat 4 bungeni kufanya mamuzi ya haraka.

Tuache yote hayo yaliyopita si ndwele tugange yajao kujenga chama chetu kiwe na mfumo imara tuingie 2013 tukiwa tumemaliza tofauti zetu siamini zitto anaweza isaliti chadema na sitaamini bado ninamuona ni kijana imara kama ilivyo kwa dr slaa hata mwenyekiti wote mbowe.

Suala la zitto kutangaza kugombea uraisi:
Zitto kama mshamsoma ni kiongozi ambaye akishapanga kitu hata kama kina negative effect kwake huwa haangalii nyuma atakwenda nacho ukishamuelewa kiongozi wa aina hii wala usipate nae shida jaribu kujenga hoja lazima atarudi.

Zitto ametangaza kuwa atagombea uraisi mwaka 2015 pia Shibuda naye alitangaza hivyo hivyo kuwa atagombea uraisi mwaka huo zitto kuiongezea hoja yake mashiko akasema yoyote atakayepitishwa na chama yeye atamsupport hatagombea ubunge tena atarudi kufundisha chuoni watu wakapayuka anaharibu chama je angekaa kimya bila kutangaza angezunguka nchini kuweka mamuliki kujipigia kampeni ili apite mwaka 2015 tungesemaje.

Zitto ameonyesha nia ya kuutaka uraisi kwa kipindi hiki wana jf na watanzania wote tumpime uadilifu wake na utendaji kazi wake je atafaa kuwa raisi wetu na sio kumvunja moyo sijui mamluki anatumia na wana ccm kisa yuko rafiki na makamba na jk unapokua mwanasiasa unayetafuta kuingia ikulu lazima ujichanganye na watu wote wale watanzania kwa sababu wewe utakuja kuwa kiongozi watu wanaleta picha alizopiga na jk sio ishu picha kitu cha kawaida sana.

Kipindi hiki chadema kingemjenga Zitto:
1.Wazee wangemuita na kupunguza hasira kumpa ushauri usingeona jibu la kutishia lile la majuzi

2:wazee wangemuambia sasa ni wakati wa wewe kuwa na mwenza wako hatuwezi kuwa na kiongozi muhuni tu ikulu

3:wazee wangemjenga na kumsimamisha imara

4:muda huu tungetumia kuchunguza mali za zitto je ana mali haramu yoyote muda huo tungemjenga zitto zaidi kwenye media na yoyote yule atakaye tangaza anautaka uraisi

5:muda huu zitto angezunguka na chama na M4C nchi nzima hapa namlaumu zitto hazunguki aanze sasa kuzunguka

Hakuna kuita mtu msaliti chama si cha demokrasia kama zitto kweli anakubalika ndani ya chama ungeitishwa uchaguzi huru ashindanie nafasi na watakao jitokeza na mshindi mmoja apatikane apeperushe bendera ya chama.

Nakuja kwa MaMuya na BEN Saanane:
Nyie ni vijana kwanini haya malalamiko yenu mlishindwa kupeleka kwa chama mmesababisha mmekivua chama nguo hapa na kukitia aidu hakika hii itatutafuna je mmekubali mlipanga mbinu chafu hapo mwanzo?? Na je mshakubali makosa na kuomba msamaha chama kiendelee mbele zaidi kusahahu yaliyopita tujenge chama imara zaidi.

Swali dogo kwa ben hivi ungekua ndo mwenyekiti wa Bavicha sasa ungeunda kile kikundi chenu?

Kwanini haya hukuyapeleka kwenye chama mapema??

Kwanini sasa ndo mmeyatoa tena hadharani je ni kweli ben unakitakia mema chama cha chadema kuanikana hadharani??

Kwanini msingekuatana na viongozi mkayamaliza kuliko kutuletea sisi na dunia nzima sasa mnaitana wasaliti??


Habib Mchange:
Wewe ni kijana imara sana uligombea ubunge mwaka 2010 ukiwa mdogo sana je ungekua mwenyekiti wa bavicha ungekubali kuunda kikundi cha uasi??

Lakini kama unakipenda chadema kweli kwanini hukupeleka malalamiko yako ndani ya chama mapema??

Kama kweli zitto alitaka kuuliwa kwanini hakupeleka kwa polisi na kwa chama??

Je uko tayari kuomba msamaha kuanzia kwa kina john mrema,dr slaa na viongozi wote mliwachafua kwenye social network??

Je uko tayari bila kinyongo kusamehana na wenzako na mjenge chama bila kuleta vinyongo vya ajabu mbeleni??

Juliana Shonza:
Wewe ni kijana mwanamke mwenye uwezo tu mzuri msomi naweza kusema kiongozi wa chama makamo mwenyekiti,je ni kweli wewe kujiunga na hiki kikundi ni uchungu heche kulipwa 700000 na wewe haulipwi kitu.

Je uko tayari kuomba msamaha kwa viongozi wote mlivyo wachafua na tugange yajayo?

Mimi wala simlamu dr slaa kukuweka pembeni aliona inafaa kubali kosa kijana tujenge chama

Huyu dada tatizo hapa ni heche kulipwa hela tunarudi yale yale siasa kuwa chanzo cha ajira vijana wetu hawa lazima wapate matatizo.

Mtela mwamapamba:
Wewe kijana hapana tena ukamtukana kabisa hapa kiongozi wako je una chuki naye ipi?

Je uko tayari kusamehe yote yaliyopita na mjenge chama kwa nguvu moja?

Je ungekua mwenyekiti wa Bavicha ungejiunga na kikundi chenu cha uasi?

je uko tayari kuomba viongozi wote ulioshawahi kuwatukana na tujenge chama sasa?

Pili fanyia kazi kwenye uandishi huwezi kuandika kitu ukiwa na hasira.

Mwisho:
Matatizo ya hawa vijana wote kwanza walifanya siasa kuwa ajira sasa baada ya kuingia ndani ya siasa na kukuta hamna pesa na wachache ndo wanapewa pesa ikabidi waanzishe movement za kupiga pesa hawa wote wasitudanganye lengo lilikuwa ni pesa tu.

Vijana wengi wanaingia kwenye mapambano haya wakijua watapata kitu sasa wanagombea nafasi fulani wakikosa wanakua hawana kingine cha kufanya kinabaki kupiga majungu mtaani na kutafuta pa kutokea kisiasa.

Vijana hawa wawekwe chini wote kuanzia kina ben,mtela,juliana,mchange wapewe onyo kali na watubu maovu yao yote chama kianze upya sitafurahi nasikia kuna kina kafulila wengine bungeni wameingia kupitia chauma mambo ambayo tulishindwa maliza ndani ya chama.

Je chama kifanye nini haya mambo yasirudie:
1.Chama kiwaite bavicha wabuni miradi ya kukiingiza chama pesa nilitoa wazo la maduka ya bidhaa za chadema makao makuu,arusha,dodoma,kilimanjaro,mwanza haya maduka unaweza kuwa mradi wa bavicha wausimamie wajue chama kinauza combat ngapi kwa mwezi na kinapata sh ngapi

2.Miradi mingine kama radio nk

Ukishakua na hii miradi ni rahisi vijana wanakosa nafasi kwenye chama kuwaingiza na kuwapa ajira fupi huku wakijipanga zaidi.

NARUDIA TENA HAKUNA MAPAMBANO HUKU UKIWA NA NJAA utanunulika tu lazima.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo naomba moderator wasiunganishe uzi huu tuwasikie ben na wenzake wanasamehana hapa hatuhitaji majibishano tena tumekesha siku zaidi ya 3 hakuna cha suluhisho.ni wakati nyie vijana kuamuana kama mtakiokoa chama chenu mpatane.

Na tusiitane wasaliti tena atakayekuja kuchangia humu wala mamuluki tuwe wastaarabu tujenge chama.

Sitamaliza bila kutoa pongezi kwa makamanda wote tulikuwa mahakamani leo heche,lissu,mbowe,lema,myika,kiwelo na wengine wengi mshikamano daima.

Hakika tutoke hapa tukale sikukuu za kumaliza mwaka tukiwa wamoja mwakani turudi na M4C ya nguvu ambapo kina shonza na mchange na ben watasimama pamoja wakiendeza sera za chama kuwaamsha watu nyumba hadi nyumba.

Tusiposamehana sasa tuna muda mchache sana kabla ya uchaguzi mkuu 2015 siamini katika kufukuza kijana siamini kabisa waombe msamaha kuteleza sio kuanguka turudi tujenge chama.

Mapambano yanaendelea

Fred Kavishe.
 
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .
Yaani mchange kaandika utumbo aliopewa na zito halafu akakupigia simu usiku wa manane ili uje umuunge mkono huku, au umempa na password kabisa..maana hata ile ID ya TUNTEMEKE mlikuwa mnaipiga mande.

Hakika wewe mwanamke ni hatari hufai hata kuwa CD achilia mbali hawara.
 
Nilichoelewa: 1.Weye na Saanane nyote 'mnarekodi' vikao vyenu....very interesting! 2. Mko kundi moja 'linalosambaratika lenyewe'. 3. Umetumwa kumsafisha Zito ingawa hujafanikiwa na badala yake kumfanya Saanane aaminike zaidi alichomwaga. 4. Vijana nyie nyooooote ni aibu sio tu kwa CDM bali Taifa!
 
mlimshtukia too late jamaa ana ushahidi wa video,audio,still pictures,text messages and all that stuff...naona jamaa aliwazidi ujanja,..huyu jamaa ni kama CIA
Mkuu Nyabhingi Umenilisha maneno ya Mchange.Jaribu kupitia hoja mbalimbali za Mchange utaona mchezo mchafu aliokuwa akiufanya ndani thread hiyo ya kuambatanisha hoja zake kwa mtu mwingine .

sasa kama hakuwa anahujumu chama kwanini aseme alikuwa msaliti na sasa ameokoka?..
saa nane wa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 anawezaje kuokoka na kuwashinda watu ambao wamepoteza nguvu, muda na akili zao katika kampeni za kupigania chama?..kama nawe ni mwanachadema hebu nitajie jina lako halisi na ili nikuulize swali...
hakuna jinsi saa nane anaweza kuukwepa huu mtego wake wa kinafiki..saa nane alitaka kutufanya sisi mabwege ili awaambie mabosi zake kuwa kuna makundi ndani ya chama. hakika hakuwa na mikakati madhubuti kufikia malengo yake hayo. ndio maana ilikuwa rahisi kumshukia.....
Haya ni maelezo ya Mchange na si yangu.
 
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.




Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7.(V4C-VOICE FOR VOICELESS) Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7. a.K.a V4C(VOICE FOR VOICELESS)?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

KATIKA KUUTHIBITISHA UNAFIKI WA SAA NANE KWA WALIOMTUMA. NAOMBA NIWEKE NAKALA YA EMAIL ALIYONITUMIA JUU YA KUANZISHA KIKUNDI CHA PM7 AMBACHO ALITAKA TUKISAJILI KAMA NGO IITWE VOICE FOR VOICELESS KISHA IZUNGUKE MIKOANI KUFANYA USHAWISHI KWA VIONGOZI WA CHAMA WA HUKO...

----- Forwarded Message -----
From: Ben Saanane <bensaanane@yahoo.com>
To: mchangehabibu@yahoo.com; mchangehabibu@gmail.com
Sent: Friday, June 10, 2011 1:52 AM
Subject: V4V values & Objctvs


The tragedy of Tanzania is a pervasive pathology. Its leadership selection process
excludes its best while celebrating mediocrity. The incremental influence of that
pathology has created a failing state that is unable to do much more than uphold the
conclave of looters that hold the country hostage. In many ways, every election
process turns out to be much worse than the preceding cycle.
Upon taking power after stolen polls, the new leadership often proceeds to enthrone
a ruling ethos that is defined by a searing contempt for the people. That is why,
despite the billions of dollars that the Tanzania state has earned over five decades,
Tanzania remains at the bottom of the human development league. It is a fate that
Tanzania must reject because a better life is possible.​
Fifty years into Tanzania’s attainment of nationhood, it still has the status of what
domestic and international observers call a failed state, failing state, or failed asset.
Tanzania’s failure to belong to the comity of successful and functional states that
obtained the status of independent nationhood within the same decade is not
attributable to the lack of material and human resources. On the contrary, the
country’s economic, social, and political failure has resulted from the non-adherence
to the practice of true federalism and the consequent mismanagement of the nation’s
resources by most of its political managers since independence. Such managers have
ranged from military dictators to civilian presidents and governors imposed on the
electorate through rigged elections

What to do now?
What is direly needed now is how to get
Tanzania out of the hole of underdevelopment, corruption, and mismanagement.
Now is the time for truly patriotic Tanzanians to join the movement to save Tanzania
from its current state of failure by joining forces with the Voice for the Voiceless Tanzanians (V4V) Group.
Now is the time to liberate Tanzania from the grips of its predators. V4V believes that​
Tanzanias’s failure is avoidable; that Tanzania can be saved. But to stop the politics of
self-imposed failure, a new crop of leaders with a patriotic outlook and a
transformational vision from those of its predatory leaders must move to the centre
of the country’s political space to re-engineer it away from chronic failure and chart
a new course in the direction of success. The V4V is blazing the trail of change and
transformation in Tanzania. V4V values has been designed to bring liberty,
security, and prosperity to all Tanzanians, is being made available to all Tanzanians, through building strong citizens to create wealth and
make contributions to modern global civilization.

ninyi wote ni wajinga sana aisee, wote mliounda hilo kundi lenu la kijinga, na mwisho wenu umekaribia, wengine tunajua ni usalama wa taifa, ila mtauja juta!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom