Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,076
- 134,463
Dr.slaa alitukanwa???Kisa kumytuma ben saaanane?
Mkuu haya sio matusiiiii
Namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuepushia wakina IDDI AMINI katika taifa letu la Tanzania maana ni bora vita ya kifisadi tunayopigana sasa kuliko vita na ukabila na udini inayotengenezwa ndani ya taasisi zetu huku watanzania wakifumbia macho na kuitana makamanda. Wale tuliojitolea kujenga chama kwa kwa moyo wote na nguvu zote kwa uaminifu ndio tunaoitwa wasaliti kwa sababu tunawakosoa! Wale wanaoishi kwa kutumia kodi zetu(ruzuku ya chama),wenye kadi mbili, wanaolipwa mishahara minono, wale wanaowatumia mahawara wao kuzunguka mikoani na kutafuta wagombea ubunge kwa kutumia kodi zetu, wale wanaopewa pesa na wanachama wa CCM(Sabodo), wale wanaofadhiliwa na CCM katika maisha yao ndio wanaoitwa makamanda kwa sababu ya ushabiki na ulimbukeni wa kisiasa tulionao baadhi ya vijana tuliojiunga ndani ya vyama baada ya uchaguzi mkuu na wanadhani kwamba viongozi ni mwingu watu na kuna watu wanaotakiwa kukosolewa na watu wanatakiwa kuabudiwa!