Duhh ndio maana Zitto alisema swala la kuuana,Kumbe ni kweli.Nilikua nampuuzia TUNTEMEKE alipokuwa anasema Ben saanane ni jasusi wa kimataifa.Kumbe Lol
SERIKALI IPO WAPI ???kijana huyu ni haramu
pumba anazo yule ambaye anakimbia kivuli chake,anayetaka kuuaminisha umma kwamba hatumiwi wakati huo huo maelezo yake yanajifunga,soma vizuri maelezo ya mchange utaelewa maana kamaliza kila kitu.bado sijafunguka nitakapo amua kufunguka nitafunguka kivingine,ila kwa leo dozi ya mchange inatosha
Hii kesi ni rahisi sana. Kitu cha kwanza ni ku prove kama Ben na Zitto wanafahamiana.
Hapo ndio uzuri wa kuwa na camera kila sehemu maana mnafiki na mwongo angejulikana haraka sana.
Je ni kweli Ben na Zitto wamewahi kukutana sehemu wakiwa peke yao?
Hii kesi hata Mwandishi tu wa habari anaweza kuchunguza na baada ya muda ukweli wote ukawa wazi.
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..
Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!
Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.
Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.
Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.
Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.
Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.
1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)
2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.
3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).
Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.
4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.
Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.
5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)
6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.
Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.
7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.
SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.
1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.
2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ''patriotic movement seven'' na akakifupisha PM7.(V4C-VOICE FOR VOICELESS) Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.
3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)
4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.
5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.
6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.
7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.
8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi '' kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote''?...saa nane..''kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo''…mimi..''kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung'unikia kila leo?''..saa nane.. '' hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa''….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?''…saa nane..''Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango''… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.
Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.
Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.
Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7. a.K.a V4C(VOICE FOR VOICELESS)?
Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.
Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.
Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.
Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.
Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.
Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.
Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.
Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..
Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.
Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.
Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.
SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.
SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..
KATIKA KUUTHIBITISHA UNAFIKI WA SAA NANE KWA WALIOMTUMA. NAOMBA NIWEKE NAKALA YA EMAIL ALIYONITUMIA JUU YA KUANZISHA KIKUNDI CHA PM7 AMBACHO ALITAKA TUKISAJILI KAMA NGO IITWE VOICE FOR VOICELESS KISHA IZUNGUKE MIKOANI KUFANYA USHAWISHI KWA VIONGOZI WA CHAMA WA HUKO...
----- Forwarded Message -----
From: Ben Saanane <bensaanane@yahoo.com>
To: mchangehabibu@yahoo.com; mchangehabibu@gmail.com
Sent: Friday, June 10, 2011 1:52 AM
Subject: V4V values & Objctvs
The tragedy of Tanzania is a pervasive pathology. Its leadership selection process
excludes its best while celebrating mediocrity. The incremental influence of that
pathology has created a failing state that is unable to do much more than uphold the
conclave of looters that hold the country hostage. In many ways, every election
process turns out to be much worse than the preceding cycle.
Upon taking power after stolen polls, the new leadership often proceeds to enthrone
a ruling ethos that is defined by a searing contempt for the people. That is why,
despite the billions of dollars that the Tanzania state has earned over five decades,
Tanzania remains at the bottom of the human development league. It is a fate that
Tanzania must reject because a better life is possible.Fifty years into Tanzania's attainment of nationhood, it still has the status of whatelectorate through rigged elections
domestic and international observers call a failed state, failing state, or failed asset.
Tanzania's failure to belong to the comity of successful and functional states that
obtained the status of independent nationhood within the same decade is not
attributable to the lack of material and human resources. On the contrary, the
country's economic, social, and political failure has resulted from the non-adherence
to the practice of true federalism and the consequent mismanagement of the nation's
resources by most of its political managers since independence. Such managers have
ranged from military dictators to civilian presidents and governors imposed on the
What to do now?
What is direly needed now is how to get
Tanzania out of the hole of underdevelopment, corruption, and mismanagement.
Now is the time for truly patriotic Tanzanians to join the movement to save Tanzania
from its current state of failure by joining forces with the Voice for the Voiceless Tanzanians (V4V) Group.
Now is the time to liberate Tanzania from the grips of its predators. V4V believes thatTanzanias's failure is avoidable; that Tanzania can be saved. But to stop the politics ofsecurity, and prosperity to all Tanzanians, is being made available to all Tanzanians, through building strong citizens to create wealth and
self-imposed failure, a new crop of leaders with a patriotic outlook and a
transformational vision from those of its predatory leaders must move to the centre
of the country's political space to re-engineer it away from chronic failure and chart
a new course in the direction of success. The V4V is blazing the trail of change and
transformation in Tanzania. V4V values has been designed to bring liberty,
make contributions to modern global civilization.
Hauna haja ya kuendelea,wakati tushakujua wewe ni mnafiki mkubwa,subiri ndoa,yako pia yataletwa na hao wenzako.Sikupenda kuingia tena katika majadiliano haya zaidi ya kusubiri vikao vya Chama.Kwa kuwa kundi hili linaendeleza mjadala na upotoshaji wa pale alipoishia kiongozi wa kundi nimeona si vyema kukaa kimya.Mchange anasema hakuwa wa kwanza kunitafuta mimi as if hii ni hoja ya Msingi sana.Hata Zitto sikuanza kumtafuta mimi ila yeye hasa baaada ya kuenguliwa uchaguzi wa BAVICHA.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yake ya kwanza yakiwemo ya tarehe 29/05/2011 siku iliyofuata baada ya kuenguliwa BAVICHA.Kwanza NI KWELI kundi hili la PM7 lilikuwepo.Ni kweli tulishirikana kaktika mpango huu.Kwanza jina PM7 ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa miongoni mwa majina mengine.E-Mail aliyotuma Mchange hapo juu ni e-mail ambayo nilimtumia Zitto Kabwe na tulikubakliana mimi na yeye isajiliwe taasisi ambayo tutakua tukiendesha harakati bila kujipambanua waziwazi na malengo ya taasisi hiyo.Lengo kuu la Taasisi hii lilikua ni kuanzisha vuguvugu la vijana na kulitumia kama platform ya kisiasa na kijamii ambayo ingekuwa non-partisan baada ya taasisi ya ADO kutokuwa active.Pia ingekuwa taasisi ambayo ingefanya harakati za baraza huru la vijana.Zitto alipokea wazo hili kwa furaha.Hata hivyo lengo la Taasisi lilibadilika na kuwa na malengo ya kisiasa ndani ya chama na wakati huo huo tukitafuta njia ya kubeba kundi la masalia kisiasa.Zitto alikuwa ameshaanza kuzunguika na kundi hili kwenye mikutano ya hadhara mikoani.Mimi ndiye niliye-draft contents zote ambazo hata hivyo Mchange hajathubutu kuziweka zote hapa.Tulitohoa jina la PM kutoka katika taasisi hiyo niliyoipa jina la Youths Patriotic MovementNinayo mawasiliano yangu na Zitto kuhusu kundi hili na alinihimiza wakati huo akiwa Songea kwenye kampeni za udiwani kwenye chaguzi ndogo za udiwani akiwa na akina mwampamba na Shonza.Tulikubaliana kwamba hii taasisi isajiliwe haraka sana iwezekanavyo namnukuuu YPM MUST BE REGISTERED SOON AND GO COUNTRYWIDE mwisho wa kunukuu.Ndugu Zitto,bila shaka anaweza kuthibitisha hiliNikiwa Geita wanachama wa kundi la Masalia walikua wakinipigia simu mara kwa mara na hata Message za kunitaka nirudi Dar haraka hata kwa muda mfupi tu tuweke mipango ya kuanzisha kundi hili pamoja na kufungua bank account.Tarehe 01/05/2012 nilifika Dar es Salaam kikazi. Siku hiyo hiyo tulikutana na Habib mchange,Mtela mwampamba,Juliana shonza na Festo Sanga pale Lunch time hotel.Siku hii ndiyo niliyotambulishwa kwa Festo Sanga. Wote walikua na shauku ya kupata mawazo yangu kwa kuwa zitto alishawadokeza juu ya mkakati huu hasa baada ya kikao cha kamati kuu.Nadhani ilikua ni matokeo ya kikao cha kamati kuu na mambo yaliyotokea humo ambayo sitaki kuyaandika hapa kwa sababu ni siri za vikao.Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua-David Kafulila-Mwigulu Nchemba-Deo Filikunjombe Na baadhi ya wafanyabiasharaPia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili.Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi.Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA,Mchange-Mdude,Shonza-Benazir,Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au DogoRole yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chamaShonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA.Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti,Mwampamba Katibu,Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba.tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika.sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matataniHata hivyo niliandaa bajeti ya Sh.25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao.PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama.Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7.Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati.Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiriActually,niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki,nilikutana na Dr.Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili.Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji.Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu.Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi,yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana.Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese,Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&.Kwa bahati nzuri shonza,Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu.Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo.uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila.ilikua Tarehe 4/07/2012.Tulikutana Tamal Hotel.Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA,tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu.Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane.nilimwambia nitafikiria.Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile.Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto.Tulipanga kukutana siku iliyofuata.Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza.Siku hii mchange hakuwepo Tarehe 7/07/20012 nilikua ndani ya Ofisi ya CHAUMMA.Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati.Mingine sitaiandika hapa kwa sasa.walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway.Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively.Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM.MAliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa.Kafulila anaweza kuthibitisha hili. Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7.Hapa Dr.Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA.Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA.Nilikua nikifahamiana naye hapo kabla.Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa .Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password.Kafulila alitaka nimpe paswd yeye,Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi.Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA.Alitaka tuende kimya kimya.Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE..Nitaendelea....
Mkuu, kunani? Mbona unaji-quote mwenyewe???
Au ndiyo kupitiliza kwa ushabiki na mapenzi ya unachokitetea?
Kulingana na maandiko yako na unavyojibu hoja za JF kuhusiana na mada hii, unaonesha kabisa kwamba wewe ni wa kundi la Bw. Machange and Co.
Inasikitisha sana kuona vijana ambao ndio tegemeo la maendeleo ya taifa wakilumbana kwa hoja mufilisi zisizojenga ndani ya JF.
Kwa maoni yangu, huyo Saanane amewapiga bao la kisigino kwa kitendo chake cha kukiri makosa yake na kuomba msamaha.
Ameonesha uungwana tofauti na ninyi ambao mnadai kufahamu makosa lukuki ya bw. Saanane lakini hamkuyatolea taarifa pahala popote, si ndani ya chama chenu wala kwa vyombo vya usalama, hususan hilo la kukamatwa akitaka kumdhuru Mhe. Zitto.
Mtaandika mengi na utetezi wa kila aina, lakini kwa werevu watajua kwamba ni harakati za mfa maji tu.
hakuna sababu ya kumuita zitto kwenye masuala ya kitoto kama haya, inavyoonyesha saa nane yupo kazini, na hiyo kazi ni kutoka nje kabisa, isipokuwa viongozi wa CDM hawajamuelewa, wanadhani wanamtumia kumchafua zitto, kumbe wanajitumia kukichafua chama.
TAARIFA NILIZOZIPATA ZINASEMA KUWA ''SAA NANE NI MTUMISHI HALALI WA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA AMEBOBEA KATIKA MASUALA YA KUANZISHA MIGOGORO. ALIFANYA HIVYO MARA NYINGI AKIWA INDIA NA SASA ANA KAZI MAALUM CHADEMA''.
kwa maana hiyo nawashauri viongozi wa chadema kumuangalia vizuri mtu wa namna hiyo.
hakuna sababu ya kumuita zitto kwenye masuala ya kitoto kama haya, inavyoonyesha saa nane yupo kazini, na hiyo kazi ni kutoka nje kabisa, isipokuwa viongozi wa CDM hawajamuelewa, wanadhani wanamtumia kumchafua zitto, kumbe wanajitumia kukichafua chama.
TAARIFA NILIZOZIPATA ZINASEMA KUWA ''SAA NANE NI MTUMISHI HALALI WA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA AMEBOBEA KATIKA MASUALA YA KUANZISHA MIGOGORO. ALIFANYA HIVYO MARA NYINGI AKIWA INDIA NA SASA ANA KAZI MAALUM CHADEMA''.
kwa maana hiyo nawashauri viongozi wa chadema kumuangalia vizuri mtu wa namna hiyo.
Sikupenda kuingia tena katika majadiliano haya zaidi ya kusubiri vikao vya Chama.Kwa kuwa kundi hili linaendeleza mjadala na upotoshaji wa pale alipoishia kiongozi wa kundi nimeona si vyema kukaa kimya.Mchange anasema hakuwa wa kwanza kunitafuta mimi as if hii ni hoja ya Msingi sana.Hata Zitto sikuanza kumtafuta mimi ila yeye hasa baaada ya kuenguliwa uchaguzi wa BAVICHA.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yake ya kwanza yakiwemo ya tarehe 29/05/2011 siku iliyofuata baada ya kuenguliwa BAVICHA.
Kwanza NI KWELI kundi hili la PM7 lilikuwepo.Ni kweli tulishirikana kaktika mpango huu.Kwanza jina PM7 ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa miongoni mwa majina mengine.E-Mail aliyotuma Mchange hapo juu ni e-mail ambayo nilimtumia Zitto Kabwe na tulikubakliana mimi na yeye isajiliwe taasisi ambayo tutakua tukiendesha harakati bila kujipambanua waziwazi na malengo ya taasisi hiyo.Lengo kuu la Taasisi hii lilikua ni kuanzisha vuguvugu la vijana na kulitumia kama platform ya kisiasa na kijamii ambayo ingekuwa non-partisan baada ya taasisi ya ADO kutokuwa active.Pia ingekuwa taasisi ambayo ingefanya harakati za baraza huru la vijana.Zitto alipokea wazo hili kwa furaha.Hata hivyo lengo la Taasisi lilibadilika na kuwa na malengo ya kisiasa ndani ya chama na wakati huo huo tukitafuta njia ya kubeba kundi la masalia kisiasa.Zitto alikuwa ameshaanza kuzunguika na kundi hili kwenye mikutano ya hadhara mikoani.Mimi ndiye niliye-draft contents zote ambazo hata hivyo Mchange hajathubutu kuziweka zote hapa.Tulitohoa jina la PM kutoka katika taasisi hiyo niliyoipa jina la Youths Patriotic Movement
Ninayo mawasiliano yangu na Zitto kuhusu kundi hili na alinihimiza wakati huo akiwa Songea kwenye kampeni za udiwani kwenye chaguzi ndogo za udiwani akiwa na akina mwampamba na Shonza.Tulikubaliana kwamba hii taasisi isajiliwe haraka sana iwezekanavyo namnukuuu YPM MUST BE REGISTERED SOON AND GO COUNTRYWIDE mwisho wa kunukuu.Ndugu Zitto,bila shaka anaweza kuthibitisha hili
Nikiwa Geita wanachama wa kundi la Masalia walikua wakinipigia simu mara kwa mara na hata Message za kunitaka nirudi Dar haraka hata kwa muda mfupi tu tuweke mipango ya kuanzisha kundi hili pamoja na kufungua bank account.Tarehe 01/05/2012 nilifika Dar es Salaam kikazi. Siku hiyo hiyo tulikutana na Habib mchange,Mtela mwampamba,Juliana shonza na Festo Sanga pale Lunch time hotel.Siku hii ndiyo niliyotambulishwa kwa Festo Sanga. Wote walikua na shauku ya kupata mawazo yangu kwa kuwa zitto alishawadokeza juu ya mkakati huu hasa baada ya kikao cha kamati kuu.Nadhani ilikua ni matokeo ya kikao cha kamati kuu na mambo yaliyotokea humo ambayo sitaki kuyaandika hapa kwa sababu ni siri za vikao.
Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua
-David Kafulila
-Mwigulu Nchemba
-Deo Filikunjombe
Na baadhi ya wafanyabiashara
draft niliyoandika ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wale ambao walikua potential donors.
Pia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili.Zitto alisafiri siku hiyo bila kutuambia na tulilalmika sana sana.Baada ya hapo alikua akiwasiliana na mtu mmoja mmoja.Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi.Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA,Mchange-Mdude,Shonza-Benazir,Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au Dogo
Role yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha.Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chama.
Shonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA.Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti,Mwampamba Katibu,Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba.tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika.sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matatani
Hata hivyo baadae nilikubali na niliandaa bajeti ya Sh.25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.
Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao.PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama.Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7.Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati.Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri
Actually,niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki,nilikutana na Dr.Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili.Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji.Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu.Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi,yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana.Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese,Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&.Kwa bahati nzuri shonza,Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu.Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo.uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili
Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila.ilikua Tarehe 4/07/2012.Tulikutana Tamal Hotel.Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA,tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu.Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane.nilimwambia nitafikiria.Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile.Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto.Tulipanga kukutana siku iliyofuata.Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza.Siku hii mchange hakuwepo
Tarehe 7/07/20012 nilikua ndani ya Ofisi ya CHAUMMA.Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati.Mingine sitaiandika hapa kwa sasa.walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway.Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively.Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM.MAliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa.Kafulila anaweza kuthibitisha hili.
Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7.Hapa Dr.Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA.Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA.Nilikua nikifahamiana naye hapo kabla.Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi.Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa .Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password.Kafulila alitaka nimpe paswd yeye,Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi.Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA.Alitaka tuende kimya kimya.Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE..Nitaendelea....
mkuu kwenye blue na taswira is one and the same rat