Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Katika mengi aliyoandika Mchange kwenye post yake sehemu hii imewavutia wengi
Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Habari za kishushu tulizozinasa zinaonyesha jana kutwa kulikuwa na mawasiliano ya ''aina mbalimbali'' kati ya Zitto na Mchange kuhusu post ya Ben Saanane. Na katika makubaliano yaliyofikiwa ni kuwa Zitto yuko kwenye wakati mgumu na huenda suala la kufukuzwa au yeye kujitoa Chadema likawepo. Hivyo yatengenezwe mazingira ya kuonyesha kuwa Zitto alitaka kuuawa kwa ajali ya gari kama Chacha Wagwe (RIP) ili hata likitokea la kutokea (akaondoka au akafukuzwa) Chadema ibaki na picha mbaya kwa umma ili isambaratike. Bado tunaendelea kuwafuatilia kwa karibu.
 
Jibu hoja je mlienda au kutaka kwenda kuapishwa kwa mganga? Kama saa nane alikuwa ndio kiongozi wenu kwanini muukubali mpango wake? Kama hamkukubaliana nae je ni wapi mlimripoti? Je saa nane ni nani ndani ya cdm mpaka mkubali awe leader wenu.? Hayo ndio maswali ya majibu tunayotaka wacha love story



Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .
 
zitto ni tetemo litakaloleta nyufa ktk chama,huyu ben wa saanane ndo huyu kuna tetesi nilizipata mwezi wa tano kwamba alitumwa kumuwekea sumu zitto,akakamatwa na masalia akaomba msamaha huku akilia na kuwataja waliomtuma,
kweli kazi ipo hapa,mchange umefunguka sana kwa wenye ufahamu kama mimi tunaelewa nini kinaendelea ndani ya chadema
tujiulize ben na mamuya ni wa wapi na wanaowapinga zitto,shonza,mchange,mwampamba ,sanga,gwakisa nao ni wa wapi nadhani majibu yatapatikana kuanzia hapo

Duhh ndio maana Zitto alisema swala la kuuana,Kumbe ni kweli.Nilikua nampuuzia TUNTEMEKE alipokuwa anasema Ben saanane ni jasusi wa kimataifa.Kumbe Lol
SERIKALI IPO WAPI ???kijana huyu ni haramu
 
Neno uzee halipendi sahihisha usemi wako.

Neno kizee hapo ni general term, likimaanisha busara za watu wazima. DR Slaa anaonesha mapungufu katika uongozi. Hili limeigharimu na litaigharimu CHADEMA.
 
Jibu hoja je mlienda au kutaka kwenda kuapishwa kwa mganga? Kama saa nane alikuwa ndio kiongozi wenu kwanini muukubali mpango wake? Kama hamkukubaliana nae je ni wapi mlimripoti? Je saa nane ni nani ndani ya cdm mpaka mkubali awe leader wenu.? Hayo ndio maswali ya majibu tunayotaka wacha love story




Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ''patriotic movement seven'' na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi '' kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote''?...saa nane..''kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo''…mimi..''kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung'unikia kila leo?''..saa nane.. '' hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa''….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?''…saa nane..''Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango''… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7.?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..
 
Broda, ktk hali iliyopo hawawezi kuacha kuwasiliana. Kwa upande wa Zitto lazima apagawe, maana amekuwa na mategemeo ya juu mno na political carrier.
 
Jibu hoja je mlienda au kutaka kwenda kuapishwa kwa mganga? Kama saa nane alikuwa ndio kiongozi wenu kwanini muukubali mpango wake? Kama hamkukubaliana nae je ni wapi mlimripoti? Je saa nane ni nani ndani ya cdm mpaka mkubali awe leader wenu.? Hayo ndio maswali ya majibu tunayotaka wacha love story

Ben saanane aseme ni wapi kwa mganga walikwenda(hii ni serious,aseme walikwenda wapi)
Pili kumbuka hawa wanafanamiana toka uchaguzi wa bavicha,inaonekana walipoona wazo la ben linamadhara kwenye chama wakaamua kulipotezea.(walilindana)
Unapouliza saanane ni nani ndani ya chadema ni kama unajitukana,BEN SAANANE NI TISS WA CHADEMA TENA WA KIKUNDI FLANI HA VIONGOZI.
 
Mkuu chama,
Nimemaliza kunywa kahawa nimemsoma Mchange, na sasa namsoma kamanda Gryson M. Nyakarungu, naye anafunguka zaidi...ngoma bado mbichi.

Mkuu Ritz
Kelele zote hizi kumbe Ben Saanane na Exaud Mamuya njaa ndiyo inawasumbua? Wao ndio walikuwa vinara wa kutaka kupiga chapuo kutoka kwa Zitto; jamaa njaa kali sana halafu @Ben anadai ana biashara zake tangu lini unafiki ukageuka kuwa biashara? Mkuu watauana hawa watu inabidi itumike busara ya hali ya juu sana yule muuaji wa Mwangosi slaa yupo tuli kama vile hajui nini kinachoendelea; kweli tulifanya busara sana kuliachia tapishi lile.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wewe unakionea huruma?Wakati wakuu wa chama ndio wamesuka mpango huu mchafu wa kuchafuana.Zitto alipo anaheka tu na kushangaa timutimu hiii dhidi yake

As if Zitto is an innocent bystander. Gimme a break!
 
Chonde chonde vijana wa CDAHEMA, wahenga walisema kusema yote siyo kuyamaliza. Kuja hapa kusemana na kusingiziana hapa siyo ustaarabu hata kidogo na wala haku-reflect uwezo wenu kitaaluma na nafasi mliyonayo ndani ya Chama. What are you trying to send to CDM followers and members? Think big my friends!
 
Duhh ndio maana Zitto alisema swala la kuuana,Kumbe ni kweli.Nilikua nampuuzia TUNTEMEKE alipokuwa anasema Ben saanane ni jasusi wa kimataifa.Kumbe Lol
SERIKALI IPO WAPI ???kijana huyu ni haramu
Product ya wapi hiyo Libya au Cuba?
 
Yaani we acha tu mkuu, tulishajua tumepata mkombozi, sasa kama mambo yenyewe ndo haya kweli kuna ukombozi hapo? Pamaoja na hayo yote moyo wangu huwa haumwamini Zitto, inaweza kuwa kweli anahusika kwa kiasi kikubwa kukidudumiza chama chetu makini.

Wewe unakionea huruma?Wakati wakuu wa chama ndio wamesuka mpango huu mchafu wa kuchafuana.Zitto alipo anaheka tu na kushangaa timutimu hiii dhidi yake
 
Mkuu Matola ahsante kwa matusi yako nikikujibu nitakula ban acha tu nikuvumilie vipi lakini za masiku? Naona unaingia jamvini kwa kwa gari la kuazima kwema?

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu jamaa uwa anasema yeye ni mfadhili wa Chadema sijui anafadhili kundi gani kwenye haya makundi au na yeye alikuwa anafadhiliwa.
 
Last edited by a moderator:
lakini mkuu mleta mada, nadhani nimekusoma mahala ukisema nawe umewahi kumrekodi huyo bw. Saanane. Soma hapa maandishi yako "… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa saanane kuwa alikuwa na kazi maalum."

ninachanganyikiwa kidogo na ninapata shida kuamini kama haya uliyoyaandika yana ukweli kama yanakinzana kiasi hiki. Angalia pia maandishi niliyoyawekea wekundu.

Saanane alipata kuandika humu jf kwamba alipata kuwa msaliti kwa viongozi na chama chake na akatubu. Na wewe je ambaye ulipata kuushuhudia usaliti ndani ya chama chako ukipendacho na ukawa na ushahidi wa mazungumzo yenu lakini hukuchukua hatua zozote dhidi ya usaliti huo hadi leo hii unaleta mashtaka katika baraza la jf, uitweje?

Mimi nadhani ni mbinu mfu ya kujikosha na kujitetea. Nadhani hili ni doa sugu, halisafishiki.
Kajipange upya kutafuta rehema ya chama chenu kutokana na madudu haya mkuu.



umeongea kwa mantiki ya hali ya juu sana mkuu,,

huyo mchange ni mfa maji tuh na daima hatoacha kutapa tapa
 
zitto ni tetemo litakaloleta nyufa ktk chama,huyu ben wa saanane ndo huyu kuna tetesi nilizipata mwezi wa tano kwamba alitumwa kumuwekea sumu zitto,akakamatwa na masalia akaomba msamaha huku akilia na kuwataja waliomtuma,
kweli kazi ipo hapa,mchange umefunguka sana kwa wenye ufahamu kama mimi tunaelewa nini kinaendelea ndani ya chadema
tujiulize ben na mamuya ni wa wapi na wanaowapinga zitto,shonza,mchange,mwampamba ,sanga,gwakisa nao ni wa wapi nadhani majibu yatapatikana kuanzia hapo

dah..hili la sumu kama ni kweli.aliempa sumu ili amuue zito atakua ndio alietoa pesa kuhakikisha huyo ben anawanasa hao kina machage kwa lunch za sijui serena hotel.na hii nadhani ni baada ya harakati za kumuua kushindikana.ukikonect doti hapa na issue ya kutaka kuengineer accident kwa kulegeza nut za tairi la gari la zito,unabaki na swali.WHO WILL BENEFIT FROM ZITO KILLING?.
 
Mkuu jamaa uwa anasema yeye ni mfadhili wa Chadema sijui anafadhili kundi gani kwenye haya makundi au na yeye alikuwa anafadhiliwa.

Mkuu Ritz
Ulisikia wapi mfadhili anapanda daladala? Matola kiatu kimempauka yeye mwenyewe anafadhiliwa malazi atafadhili chama? Ni matumizi mabaya ya kiswahili Matola ni walewale waganga njaa

Chama
Gongo la mboto DSM
 
ZITTO anatamani kuingia JF kujibu kashfa, wenye busara wanamzuia wanamwambia chama kitasambaratika.

ZITTO anawaambia vijana wananihsaribia na wameshanichafua, wenye busara wanamwambia vumilia kwani ukubwa ni dawa.

ZITTO anawaambia taswira yangu kwa jamii nisipojibu itakuwa imechafuka, wanamwambia hawa vijana wataomba radhi kwenye vikao na in public.

ZITTO anawaambia lakini jamii itakuwa imeshaamini kuwa waliyosema ni kweli, anaambiwa kwa mustakbali wa ' chama chetu' tunakuomba ukubali hiyo price.

ZITTO anasema ngoja nifikirie zaidi ila moyo unauma.

Nini kitaendelea baada ya hapo:

1) Jee Ben ataomba radhi kwa ZITTO kwa kumchafua?

2) Jee BEN na kundi lake watatemwa CDM?

3) Nini kitatokea ikiwa jibu ni ndiyo au hapana, tuendelee kusubiri.
 
mchange, unaonekana jinsi ambavyo unaweza kuburuzwa na watu na kwa hili unaweza kuwa kibaraka wa kiongozi yoyote, wewe unasema ulimshtukia, mara nilipingana naye lakini bado ukaendelea kuwa ktk kikundi hicho hicho unachoamini kilikuwa kinaongozwa na mtu uliyejuwa katumwa...... tukuweke wapi?
 
Back
Top Bottom