Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

dah..hili la sumu kama ni kweli.aliempa sumu ili amuue zito atakua ndio alietoa pesa kuhakikisha huyo ben anawanasa hao kina machage kwa lunch za sijui serena hotel.na hii nadhani ni baada ya harakati za kumuua kushindikana.ukikonect doti hapa na issue ya kutaka kuengineer accident kwa kulegeza nut za tairi la gari la zito,unabaki na swali.WHO WILL BENEFIT FROM ZITO KILLING?.


Hapo kwenye red jibu ni slaa!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..



SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

Nilipo RED.
umekosea kwa kiarabu tunasema Alamat munafiqina thalatha kwa maana alama za Mfaniki ni
tatu.
 
[h=5]COPIED AND PASTE from facebook:

Grayson M. Nyakarungu


[/h][h=5] ‎@All, hakuna kinachofanyika zaidi ya ccm kufaidi sasa Ben Wa Saanane tumekutana wakati wa mchakato wa bavicha hapo ndipo tulipofahamiana. mimi na ben hatujawahi kupanga njama asemazo na wala kumjadili kiongozi wa kitaifa, mwajua mnafiki ataumbuka yeye tu..naomba ben uwahishe ombi lako kwa chama ili utoe huo ushahidi usemao, pia wewe ben ulikuwa ukilalama sana eti kila unapomtafuta zito anakuwa busy hamjawahi kukaa kila siku story yako ni kuwa unatarajia kuonana nae, sasa ndugu yangu ben tena nakusihi sana uje na hizo documents zako fanya haraka!!!

[/h]

...Duh huyu Ben wa Saanane ni noumer,ni heri usiwe na rafiki kabisa kuliko kuwa na rafiki mnafiki kama huyu, sio kwenye siasa tu bali ata kwenye maisha ya kawaida...
 
Ni ugomvi wa kugombea madaraka au mmetomb...ana mademu?
 
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7.?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..



Ni rahisi sana Kujua mnafiki ni na Mchawi wa CHADEMA ni nani baina yenu.

Kuna Observations kadhaa ambazo kama uko makini unawajibika kujibu.

1. Ulichukuwa hatua gani ili tuone kama wewe siyo mnafiki wa kundi fulani CHADEMA e.g Zitto kudeal na Mnafiki Saanane. NI kwa sababu umedhibitisha kuhusina na Saanane mwanzo hadi mwisho lakini hukuchukua hatua yoyote. Isipokuwa unakuja kumwaga umbea hapa JF ambao unakuhukumu moja kwa moja unahusika na mpango huo.

2. Saanane alidhibitisha kuhusika na njama hizo, na nafsi yake imemusuta na kaona anafanya kitu ambacho siyo sahihi na kamwaga issue yote hapa. Wewe unakuja na umbea zaidi, ungeonekana wa maana kama ungekubali kuhusika then ukaomba radhi then ukaendelea kueleza kilichotokea. Wewe unaonekana umekuja kumsafiisha Zitto, ambaye by hooks and crooks hasafiishiki tena. Na tumemstukia.

3. Ulijuaje kwamba Zitto kupata ajali siku ya Mwl. Nyerere zilikuwa ni njama za Watu kutaka kumuua na si ajali tu. Unatupa muelekeo wako na wachawi/washirikina wenzako akina Zitto. Yaani wote kundi moja, Kazi moja, Malengo yaleyale tu.

4. Sasa kama ndivyo sivyo alivyoeleza Saanane, wewe unasema alitumwa na viongozi fulani ndani ya CHADEMA, lakini maelezo yako yanaonyesha nia ya Saanane kukutana na Zitto kukamilisha malengo ya Zitto, sasa inakuwaje huyohuyo ambaye katumwa na watu wengine lakini anakuja kufanya kazi ya mtu mwingine tena.


NB. Mnakiharibu CHADEMA nyie washirikina, wapenda madaraka e.g Urais, Wanafiki, na mashetani wakubwa nyie. Mlaaaniwe nyinyi na vizazi vyenu vyote kuendelea kuwarudisha nyuma watanzania.

Pathetic!!!???
 
ZITTO anatamani kuingia JF kujibu kashfa, wenye busara wanamzuia wanamwambia chama kitasambaratika.

ZITTO anawaambia vijana wananihsaribia na wameshanichafua, wenye busara wanamwambia vumilia kwani ukubwa ni dawa.

ZITTO anawaambia taswira yangu kwa jamii nisipojibu itakuwa imechafuka, wanamwambia hawa vijana wataomba radhi kwenye vikao na in public.

ZITTO anawaambia lakini jamii itakuwa imeshaamini kuwa waliyosema ni kweli, anaambiwa kwa mustakbali wa ' chama chetu' tunakuomba ukubali hiyo price.

ZITTO anasema ngoja nifikirie zaidi ila moyo unauma.

Nini kitaendelea baada ya hapo:

1) Jee Ben ataomba radhi kwa ZITTO kwa kumchafua?

2) Jee BEN na kundi lake watatemwa CDM?

3) Nini kitatokea ikiwa jibu ni ndiyo au hapana, tuendelee kusubiri.

Ataambiwa hata viongozi wenzako kina slaa wamechafuliwa sana lakini hawajajibu kwa kuwa ukubwa jalala je! yeye hataki kuwa jalala???? Rais gani wa hivyoooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cardinal Pengo, nakuomba waite vijana wako wamalize ugomvi wao!
 
Juliana Shonza napenda utuambie watanzania kuwa 1. kwa nini ulishiriki kwenye kikundi hichi? 2.Je mlikua mna matarajio gani ndani ya kikundi hichi? 3. kwa nini haukuwa tayari kuanika haya kabla ya nyie kupishana na Saa nane??

........
@Daudi Mchambuzi kwanini usianzishe thread nyingine? hii ni ya Ben 0' clock iliyoletwa na Mchange na Juliana Shonza ametajwa huko, nakushauri wewe changia km mada zinavyokwenda maana haujaingizwa au kutajwa wala mm sijaingizwa, hao ni BAVICHA na CDM.

Watanzania tunatamani kuingia na kutoa ushuhuda wetu lakini sio wakati wake PATA PICHA
hata kwenye FB wanatajana kwa majina huku JF mnafichana tu kwa ID (Ingia FB ya huyo Shonza ukamuulizie hukohuko)
 
SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..........

Saa nane sio Muislam mkuu...
 
Mchange,zitto kabwe,nyie ni wanafiki katika chama chetu,Chadema mliikuta na mtaiacha,na mjue hamna wafuasi wanaowaunga mkono\.

Watanzania wana elimu kubwa sana,wanajua kila kitu,na endeleeni na ushirikina wenu we na Zitto,sisi tunamwamini Mungu! Its shame to Zitto to say ameaga kigoma na atakagusa kwao watapukutika kama panya,kiongozi anayeamini ktk ushirikina si kiongozi.
 
imeanza,juzi na Mamuya, jana kaja Saanane, leo Mchange, kesho sijui nani, mbona inaonekana kama ndiyo sijui hiyo PM7 hiko kazini, ni mkakati wa vijana uliopangwa ukapangika, mwisho wote mnakusanyika mnaomba radhi mmoja anainuka kidedea, siasa kweli ni uwongo uliokomaa
 
Kunasehemu umeona zitto amejulishwa kuhusu hicho kikundi??au hiho kikundi kilikuwa kinajipanga kukutana na zitto wamwambie adhima yao?
jaribu kushiriksha akili yako na nywele zao..........

sidhani kama kuna haja ya kubishana hapa JF kwa sababu kutakua na kikao cha chama mtaeleza yote myokua mnayafanya na mliyotarajia kuyafanya kabla hamjaingia kwenye huu msuguano.
 
Mkuu Ritz
Kelele zote hizi kumbe Ben Saanane na Exaud Mamuya njaa ndiyo inawasumbua? Wao ndio walikuwa vinara wa kutaka kupiga chapuo kutoka kwa Zitto; jamaa njaa kali sana halafu @Ben anadai ana biashara zake tangu lini unafiki ukageuka kuwa biashara? Mkuu watauana hawa watu inabidi itumike busara ya hali ya juu sana yule muuaji wa Mwangosi slaa yupo tuli kama vile hajui nini kinachoendelea; kweli tulifanya busara sana kuliachia tapishi lile.

Chama
Gongo la mboto DSM.......

Kuna mtu kaongelea mahaba yenu ya kutajana hapa naona aliniwahi manake naona wakuu mnafuatana tu ni mahaba ya dhati mnayo.
 
YESU NA MARIAAAA!!!!Huyu mtu hatari .Ben saanane,Unaomba kupiga story then unageuza kikao halali na unalipa Bili ya msosi wote bila kujali hapa ni BLue pearl,Lunchtime n.k

sasa wewe umeprove vipi maneno ya mchange mkuu?
 
ben hawezi kumuingiza mtu yeyote king kati ya hao anaowataja yeye mwenyewe anajua ,anachofanya ni kutoa report ya uwongo kwa wale waliomtuma ili aonekane amefanikiwa kutimiza lengo.kitu ambacho si kweli.ukweli utajulikana tu.

A woman with no commercial value! Hili ndio tatizo la kuokota madada kona bar na kuwasimika kuwa viongozi.
 
Naona ni mambo ya kumwaga ugali na mboga, jamani mnafaidisha nani kwa bifu hizi? nyumba yako ikivuja unatafuta jinsi ya kuziba tundu hilo, siyo kutoboa tundu zaidi, busara nafikiri mnaotuhumiana mngekaa na kutatua mzozo huu.
 
ben hawezi kumuingiza mtu yeyote king kati ya hao anaowataja yeye mwenyewe anajua ,anachofanya ni kutoa report ya uwongo kwa wale waliomtuma ili aonekane amefanikiwa kutimiza lengo.kitu ambacho si kweli.ukweli utajulikana tu.



Post sita zote upu.pu!

Junior Member

verified.png
Array


Join Date : 19th December 2012
Posts : 6
Rep Power : 302
Likes Received6
Likes Given2
 
Back
Top Bottom