Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Mheshimiwa Zito, Hawa ndio waharibifu wa chama chetu! Hivi wewe unaukoma hapo Chadema, hizo tuhuma juu yako mbona hawathibitishi, kazi ni majungu nakueneza chuki binafsi tu......

Zitto ni zaidi yao ndio maana tuhuma zao hawazidhibitishi ni maneno tu,ambayo hata mimi naweza kuyatunga
 
Mkuu Kimbunga,
Hivi Wassira alijuaje kuwa mwaka 2015 Chadema itasambaratika.

Chadema wataingia kwenye uchaguzi mwaka 2015 na majeruhi makubwa.

Kuna mgogoro mkubwa unakuja kwenye uchaguzi mkuu wa Chadema.

Hivi wewe Ritz nani hautaki Urais? Nani hajui kwamba ukishakuwa Rais unakuwa Urais hauna ubia? Niliwaambia CDM wanakimbilia jumba jeupe wanadhani milango iko wazi lakini watafika pale nje wakiwa mmoja mmoja na milango inafungwa.
 
Last edited by a moderator:
Wana JF naomba kwa mwenye ufahamu anijibu swali langu, Hivi huyu Ben Saanane ameungama kwa nani CHADEMA,Mamuya,Dr Slaa,Mbowe au Lema? sioni chanzo au utaratibu aliotumia kujisafisha.
 
Zitto huwa hataki ushauri kutoka kwa mtu, huwa anakurupuka km ngiri aliyetoka usingizini. Hapa ameshikwa pabaya, atajitetea kwa lipi?.

Hoja za ZITTO zilitaka kuangusha serikal ya CCM. Leo unataka tuamini yeye hafai anafaa BEN? Ni wabaguzi na wapenda vyeo tu watakaokubali hizi kashfa dhidi ya ZITTO.
 
Tatizo ni kile kiapo naona bado kinafanya kazi na kumbe wengi mlishiriki ........
 
Ben Saanane analazimisha kujuana na Zitto patamu sana hapo!

Chama
Gongo la mboto DSM

Mimi tangu juzi niliposoma ile Thread ya kwanza iliyomtetea sana Ben na kuonyesha ni namna gani ambavyo yeye ni mzuri eti kwa sababu ametoa siri,nilicomment humu ndani kwamba huyo mtu anayeitwa Ben huyo,ni tatizo,mimi simjui lakini nataka niwaambie CHADEMA kama wananisikia ama wanaiona hii comment yangu sasa hivi wamtimue Ben mara moja wakae pembeni wakati bado wanaendelea na wengine,nashukuru Mungu kwamba Mchange amekuja na majibu ambayo mimi tayari nilikuwa nimeyabashiri,kwa hiyo huyu mtoto Ben huyu,aki ya mama yangu mzazi ni tatizo kubwa na CDM wasipoka vizuri anaweza akawakoroga,weka kwanza pembeni wakati mambo mengine yanaendelea.
 
Sio siri wewe jamaa umenichekeshaaa kinoma nomaaa.yaani hadi majirani wamesikia.
Lakini ukweli ndio huo sipendi ligi bali nafichua unafiki wa viongozi flani wa chadema kutumia vijana flani wa nyumbani kwao kuchafua chama na viongozi kama zitto

halafu na wewe unanekana mhusika kwenye kundi hili la wasaliti na mda si mrefu na wewe utamwaga ladhi tu kama hawa wenzio akina saa nane, mchange na wengine mnaojipambanua hapa bila kujijua
 
hahahahaahah.....inamaana starring anakufa halafu movie inaendelea?

Kama ulikuwepo starring zamani wameshazika tunasubiri mzimu urudi kumaliza mchezo

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Zitto huwa hataki ushauri kutoka kwa mtu, huwa anakurupuka km ngiri aliyetoka usingizini. Hapa ameshikwa pabaya, atajitetea kwa lipi?.

Zitto ni mwiba kwako na hao watu wako.
 
zitto hamjui ben saanane.

Katika watu wawili ambao mmoja anadai ananijua na tumekutana na mwingine anasema simjui wala hatujakutana..., inawezekana vipi third party awe na uhakika wa kutokujuana kwa hawa watu wawili ?
 
Hoja za ZITTO zilitaka kuangusha serikal ya CCM. Leo unataka tuamini yeye hafai anafaa BEN? Ni wabaguzi na wapenda vyeo tu watakaokubali hizi kashfa dhidi ya ZITTO.

Mkuu ukisoma vizuri moja ya Comment zangu kwenye ule uzi wa Mchange utaona namna ambavyo nimeeleza kwamba ile Thread ya kwanza kabisa juzi iliyokuwa humu kabla ya kufungwa jana ilianzishwa kwa makusudi kabisa ya kumchafua Zitto,lakini sasa ninavyoona wamekosea katika mipango yao ndio maana unaona wameanza kuumbuana wao kwa wao,wewe nakwambia subiri kuna data nimepenyezewa ambazo zitaletwa humu na wale wengine waliotajwa,nina hakika kuna baadhi yao watamua kujinyonga,maskini ya mungu ingawa wengine hatuwajui kwa sura lakini utawasikia tu.
 
Hoja za ZITTO zilitaka kuangusha serikal ya CCM. Leo unataka tuamini yeye hafai anafaa BEN? Ni wabaguzi na wapenda vyeo tu watakaokubali hizi kashfa dhidi ya ZITTO.

unataka kuniaminisha kuwa mtu mwaminifu hawezi kugeuka kuwa msaliti? Ni swali la kivushi tu usijetoka povu ndugu
 
Back
Top Bottom