Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ukiangalia kwa undani ni sisi ndio tunawavibisha kichwa hawa Vijana wasio na uwezo wowote wala karama ya Uongozi, nadhani sasa ni wakati wangu muhafaka kupumzika jukwaa hili na nirelax MMU mpaka mwakani, naona ujinnga ujinga tu hapa...........

Hivi Molemo na Tuntemeke wapo lupango?Ingekuwaje hapa kama wangekuwepo.
 
Adha ya vijana kutumika kuchafua watu ndio hii?
Umewahi msikia Ben saanane kwenye mkutano wowote?au M4C yoyote ya kichama?
Unamisikiaga hapa kwenye usaliti,mara TISS n.k hii ndio kazi ya Ben saanane pale chadema........

Hizo ndo siasa..Ukitaka kuwa mwanasiasa lazima ukubali kuplay dirty,ukijilegeza wenzako wanakupiga bao.Nadhani zitto atakuwa ameelewa sasa What is he agaisnt.
 
Kazi ipo sana. Kwa hali hii CDM kuingia Magogoni ni ndoto. Kumbe wasaliti mpo wengi sana? Mchange, Saanane, Zitto wote hamna kitu.

Kwanini msilumbane kwenye mikutano yenu huko tukajua kama mna nia njema na CDM. Napata picha nyinigine, Zitto ni mbaya kuliko wengine wote hapo kwani kila linalozungumzwa lina connection na zito kwanini?

Kuna kitu kimejificha, Slaa na Mbowe hebu fanyeni uchunguzi kukinusuru chama.
 
kwanini mnawatukana viongozi wakuu wa chama kwenye faceboo?au nalo ni saanane kashtaki?

.........

Unapotoa kauli kama hizi,leta na ushahidi hapa jukwaani.Hata mm naweza kusema kwanini umepokea rushwa ya kuja kufanya kazi ya kumchafua Zitto?(sina ushahidi)
 
Nyani Ngabu: Waliotakiwa kuwakanya wamewagawa katika makundi, kuna vijana wanaothaminiwa michango yao na vijana wengine hawana thamani yeyote mbele ya watu hao.

Kama Dr. Mkumbo aliingilia kati yakashindikana unategemea nini. Mimi nadhani watu kama nyinyi( wewe, Mzee mwanakijiji etc) wasio na upande labda mkiitwa mnaweza mkatatua mgogoro huu.

Dr. Mkumbo atawezaje kutatua mgogoro wakati na yeye ndiyo chanzo pia cha mgogoro.

Sina uhakika kama umelisoma bandiko la Exaud Mamuya, pale aliposema,


..... Bwana Zitto ikumbukwe vizuri ya kwamba wewe ndo uliyekuwa UKICHOCHEA MGOGORO WA MADIWANI kwa lengo la kumdhoofisha mh Lema kisiasa na mipango na mikakati yote ilikuwa ikifanywa baina yangu mimi, wewe Dr Kitila Mkumbo pamoja na madiwani waliofukuzwa Chadema.

Dr. Mkumbo=Mh. Zitto
 
Kazi ipo sana. Kwa hali hii CDM kuingia Magogoni ni ndoto. Kumbe wasaliti mpo wengi sana? Mchange, Saanane, Zito wote hamna kitu. Kwanini msilumbane kwenye mikutano yenu huko tukajua kama mna nia njema na CDM. Napata picha nyinigine, Zito ni mbaya kuliko wengine wote hapo kwani kila linalozungumzwa lina connection na zito kwanini? kuna kitu kimejificha, Slaa na Mbowe hebu fanyeni uchunguzi kukinusuru chama
Onesha onnetion mkuu,ZItto anapendwa na vijana wanataka kumtumia yeye hawataki.Ndio maana wanakuja kurumbana hapa
 
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .


Hii kama ni kweli ni sawa na kula nyama ya mtu, haiwezi kuisha hata kwa fukuza fukuza.
 
[h=5]COPIED AND PASTE from facebook:

Grayson M. Nyakarungu


[/h][h=5] ‎@All, hakuna kinachofanyika zaidi ya ccm kufaidi sasa, mtatawanyika na hakuna atakayewakusanya hata kwa miruzi ya zomali, naona vijana mnaojiita makamanda mkitukanana mkidhania ndio siasa, niliwahi kuonya tabia ya kujiweka kwenye utamaduni wa kutukana viongozi wa serikali hovyohovyo bila kujifunza hoja, na tabia hii imekuwa na kuota mizizi, dhambi yetu inageuka na kututafuna wenyewe, Ben Wa Saanane tumekutana wakati wa mchakato wa bavicha hapo ndipo tulipofahamiana na baadae tukawa tunakutana na kujadili namna gani tutajenga mtandao wa kiharakati wa vijana usio wa chama cha siasa, ila yote yalikufa baada ya mimi kwenda mwanza kazini kwangu, mimi na ben hatujawahi kupanga njama asemazo na wala kumjadili kiongozi wa kitaifa, mwajua mnafiki ataumbuka yeye tu..naomba ben uwahishe ombi lako kwa chama ili utoe huo ushahidi usemao, pia wewe ben ulikuwa ukilalama sana eti kila unapomtafuta zito anakuwa busy hamjawahi kukaa kila siku story yako ni kuwa unatarajia kuonana nae, sasa ndugu yangu ben tena nakusihi sana uje na hizo documents zako fanya haraka!!!

[/h]
 
hicho ndiyo chama makini kimejaa vijana wasomi kutoka chuo kikuu.


almighty god gave you the life to live,instead of living your life,you are living the life of others,,

poor boy,hujielewi,huelewi future yako,huelewi matarajio yako,,

unaishi kwa sababu tuh una pumzi na unaitumia kupumua,who taught you to dispise your self??
 
Kwa mujibu wa maelezo ya Mchange anasema Ben ndiye alikuwa kiongozi wa kundi la PM7 na katika hatua za hawali kwa mujibu wa maelezo ya Mchange, anasema Ben ndiye alikuwa anahitisha vikao mbali mbali na kuwaudumia yeye mwenyewe...

Na kwa majibu ya Ben ya jana ana mtaja Mh. Zitto kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa kundi na alidiriki kuwapeleka kwa Mganga wakale kiapo cha kutosaliti kundi lao.....

Nadhani vijana wamefunguka vizuri sana, hapa ni sisi kuchambua hoja zao na mwisho wasiku tutajua nani mkweli na nani muongo.

Hata hivyo chadema ina kazi kubwa sana, kama vijana wenyewe ambao tulikuwa tunawategemea na kufuata nyendo zao ndio hawa basi safari ya ukombozi ni ngumu sana kuliko tulivyo kuwa tukidhania...

Hapana bado kuna wengine wanatakiwa wafunguke mkuu,idadi yao bado na kila mmoja ana lake jambo la kusema hatuwezi kuchambua haya mambo wakati kuna watu tunasubiri wafunguke humu akiwemo huyo na Zitto.Tulia kwanza mkuu usiwe na haraka hii muvi ni kali inazidi ile ya Escape From Sobibo!!!!!!
 
hizo ndo siasa..ukitaka kuwa mwanasiasa lazima ukubali kuplay dirty,ukijilegeza wenzako wanakupiga bao.nadhani zito atakuwa ameelewa sasa What is he agaisnt.

Yeah Zitto ameshajua kuwa anawindwa kwa kila namna na hawa vigogo wa chadema.Lakini ni bora chama kipone hawa wanaotunga uongo wafe
 
Ofcourse, wanatoa maelezo yanayomaanisha kwamba tokea mwanzo ben amekuwa akiendesha mikakati ya kiharamia dhidi ya chama, na wanaonyesha kwamba hawakuwahi kukubaliana nae hata mara moja, na wanaonyesha kwamba walijua alikuwa anatumwa kwa nini hawakumlipua mapema.

mpaka sasa hawa watu mbele yangu wanahatia

kwangu mimi hawa wote ni wasaliti wakubwa kwa chama chao pamoja na kwa watanzania walioweka matumaini yao kwa CDM km mkombozi kwa kucheza ngoma ya upande wa pili naya hatari ya kukibomoa chama chao wenyewe
 
Mchange,
Maji yashamwagika hayazoleki tena! Kwa uzi wako huu unathibitisha (kwa kujua au la) tuhuma za uzi wa Mamuya awali. Kwa sababu watu wote aliwaotaja Mamuya mmejitokeza (kwa bahati hata Tuntemeke kaja kwa jina lake halisi la Gwakisa) na kufanya exactly mlichokuwa mnatuhumiwa.

Kama mnataka siasa jichunguzeni upya. Na hasa kama mnataka kufanya siasa mkiwa wana-CHADEMA nadhani ukweli uko wazi tu kuwa ninyi mmeshiriki usaliti dhidi ya CHADEMA kwa namna zaidi ya moja.

Ukweli unauma lakini ndio dawa pekee, vijana mnaaibisha! Tubuni na jirekebisheni haraka na mjifunze kutokana na makosa na uovu mliokuwa mnaitendea CHADEMA. Period.
 
Naona unajiliwaza na kujifariji mkuu.

Mkuu Ritz siasa aka politics is all about power struggle ambazo huongozwa na personal decision zinazolenga kunufaisha jumuia nzima. Kwenye siasa hakuna fursa ya kujifariji maana maamuzi yakifanyika yanakuwa yamefanyika, Mwenyekiti Kikwete huita hili "ajali ya kisiasa"

Kwa kutambua hilo neno la Mwenyekiti Kikwete,itakuwa ni ajabu ya musa kwa wanazi na mashabiki wa siasa kama 50thebe kujifariji kufuatia maamuzi ya kisiasa yaliyofanya ana wanasiasa waigizaji. Maana haiwezekani ku-reverse maamuzi hayo bali kuishi nayo na kuyafanyia maamuzi mengine muhimu ili kuyatangua.

Istoshe mkuu Ritz, ukilinganisha siasa za ndani ya CCM na siasa za ndani ya Chadema, kwa mtazamo wangu naona siasa za ndani ya chadema zinayo siha bora zaidi kuliko zile za ndani ya CCM, sababu kubwa ni moja, wanasiasa wa ndani ya chadema wanasema kero zao hadharani, mwenye ushahidi wake anautoa bila kujali UTHABITI wa ushahidi alionao ili kutoa fursa kwa mashabiki na "mahakimu wa matukio" kutoa maoni ama hukumu zao. Tofauti na CCM hii ya kizazi kipya, kila neno linakanushwa ama litatolewa ufafanuzi unaopwaya huku ukweli ukizingwa na wingu la "suala halina maslahi kwa taifa". Hapo tu ndio CCM inapopoteza umakini na nasaba ya kuwa Chama Cha Wanyonge ambao wanaamini kila kitu-kizuri ama kibaya- kina maslahi kwao kujali ukubwa ama udogo wake.
 
Zitto hopless sana,hebu jaribuni kuzisoma posts za mchange na juliana shonza jinsi wanavojaribu kujinasua nasua kwenye shutuma hizi na kuishia kulalama ya kwamba ben msaliti beni msaliti wa chama,,!!yani kauli zao hazina mashiko kabisa,so so childish

hakuna ambae hajui ya kwamba ben nae kakisaliti chama,,yeye mwenyewe kasema ivo na amekiri ya kwamba alikua anakihujum chama na hao kina zitto wakiwemo,aliwasihi wenzake kuamua kusitisha harakati hizo kwa maslahi ya chama ila wenzake waliendelea kwa sababu zenye manufaa juu yao,shonza na wenzako kuja hapa na kushupalia kumjibu ben saa nane personally bila kujibu shutuma zilizotajwa ni ukanjanja wa hali ya juu sana,,

na inaonesha kabisa na kwa kiasi gani mlivyo na akili za kitoto,tunataka ukweli tuuskie na sio blah blah na kujinasua nasua kwenye madudu mliyoyafanya,,kama siku zote walikua wanafaham zitto na ben saa nane wanahujum chama walikua wapi kuacha kuyafikisha hayo katika vikao vya chama wanalalamika waende kuyazungumza leo??

broken adults..

Wote hapa tunajua Ben alikuwa msaliti kama alivyokiri mwenyewe hapa...
Sasa hawa nao badala ya kujibu hoja juu ya tuhuma zinazowakabil wanakuja na viroja vingine eti Ben ni msaliti, ingali nawao walikuwa kwenye kundi moja na Ben ambao sasa wamebaki huko kama Masalia na wanachofanya sasa ni kujaribu kumchafua Ben ili wao waonekane wasafi tena kwa hoja dhaifu.
 
COPIED AND PASTE from facebook:

Grayson M. Nyakarungu




‎@All, hakuna kinachofanyika zaidi ya ccm kufaidi sasa, mtatawanyika na hakuna atakayewakusanya hata kwa miruzi ya zomali, naona vijana mnaojiita makamanda mkitukanana mkidhania ndio siasa, niliwahi kuonya tabia ya kujiweka kwenye utamaduni wa kutukana viongozi wa serikali hovyohovyo bila kujifunza hoja, na tabia hii imekuwa na kuota mizizi, dhambi yetu inageuka na kututafuna wenyewe, Ben Wa Saanane tumekutana wakati wa mchakato wa bavicha hapo ndipo tulipofahamiana na baadae tukawa tunakutana na kujadili namna gani tutajenga mtandao wa kiharakati wa vijana usio wa chama cha siasa, ila yote yalikufa baada ya mimi kwenda mwanza kazini kwangu, mimi na ben hatujawahi kupanga njama asemazo na wala kumjadili kiongozi wa kitaifa, mwajua mnafiki ataumbuka yeye tu..naomba ben uwahishe ombi lako kwa chama ili utoe huo ushahidi usemao, pia wewe ben ulikuwa ukilalama sana eti kila unapomtafuta zito anakuwa busy hamjawahi kukaa kila siku story yako ni kuwa unatarajia kuonana nae, sasa ndugu yangu ben tena nakusihi sana uje na hizo documents zako fanya haraka!!!

Mods tunaomba hii iambatanishwe.Naona nyakarungu kafunguka,na anahamu Ben apeleke ushahidi mbele ya chama haraka sana
 
Wote hapa tunajua Ben alikuwa msaliti kama alivyokiri mwenyewe hapa...
Sasa hawa nao badala ya kujibu hoja juu ya tuhuma zinazowakabil wanakuja na viroja vingine eti Ben ni msaliti, ingali nawao walikuwa kwenye kundi moja na Ben ambao sasa wamebaki huko kama Masalia na wanachofanya sasa ni kujaribu kumchafua Ben ili wao waonekane wasafi tena kwa hoja dhaifu.
Ben saanane anakiua chama,Ben ameamua kutafuta mafao ya mwaka
 
Nafarijika kuona na kutambua uwepo wa Dr. Slaa ktk uzi huu pia. Naamini kuna kitu chema mwisho wa tafrani hii!
 
Back
Top Bottom