Mkuu Ritz siasa aka politics is all about power struggle ambazo huongozwa na personal decision zinazolenga kunufaisha jumuia nzima. Kwenye siasa hakuna fursa ya kujifariji maana maamuzi yakifanyika yanakuwa yamefanyika, Mwenyekiti Kikwete huita hili "ajali ya kisiasa"
Kwa kutambua hilo neno la Mwenyekiti Kikwete,itakuwa ni ajabu ya musa kwa wanazi na mashabiki wa siasa kama 50thebe kujifariji kufuatia maamuzi ya kisiasa yaliyofanya ana wanasiasa waigizaji. Maana haiwezekani ku-reverse maamuzi hayo bali kuishi nayo na kuyafanyia maamuzi mengine muhimu ili kuyatangua.
Istoshe mkuu Ritz, ukilinganisha siasa za ndani ya CCM na siasa za ndani ya Chadema, kwa mtazamo wangu naona siasa za ndani ya chadema zinayo siha bora zaidi kuliko zile za ndani ya CCM, sababu kubwa ni moja, wanasiasa wa ndani ya chadema wanasema kero zao hadharani, mwenye ushahidi wake anautoa bila kujali UTHABITI wa ushahidi alionao ili kutoa fursa kwa mashabiki na "mahakimu wa matukio" kutoa maoni ama hukumu zao. Tofauti na CCM hii ya kizazi kipya, kila neno linakanushwa ama litatolewa ufafanuzi unaopwaya huku ukweli ukizingwa na wingu la "suala halina maslahi kwa taifa". Hapo tu ndio CCM inapopoteza umakini na nasaba ya kuwa Chama Cha Wanyonge ambao wanaamini kila kitu-kizuri ama kibaya- kina maslahi kwao kujali ukubwa ama udogo wake.