Ukiangalia kwa undani ni sisi ndio tunawavibisha kichwa hawa Vijana wasio na uwezo wowote wala karama ya Uongozi, nadhani sasa ni wakati wangu muhafaka kupumzika jukwaa hili na nirelax MMU mpaka mwakani, naona ujinnga ujinga tu hapa...........
Adha ya vijana kutumika kuchafua watu ndio hii?
Umewahi msikia Ben saanane kwenye mkutano wowote?au M4C yoyote ya kichama?
Unamisikiaga hapa kwenye usaliti,mara TISS n.k hii ndio kazi ya Ben saanane pale chadema........
kwanini mnawatukana viongozi wakuu wa chama kwenye faceboo?au nalo ni saanane kashtaki?
.........
Nyani Ngabu: Waliotakiwa kuwakanya wamewagawa katika makundi, kuna vijana wanaothaminiwa michango yao na vijana wengine hawana thamani yeyote mbele ya watu hao.
Kama Dr. Mkumbo aliingilia kati yakashindikana unategemea nini. Mimi nadhani watu kama nyinyi( wewe, Mzee mwanakijiji etc) wasio na upande labda mkiitwa mnaweza mkatatua mgogoro huu.
..... Bwana Zitto ikumbukwe vizuri ya kwamba wewe ndo uliyekuwa UKICHOCHEA MGOGORO WA MADIWANI kwa lengo la kumdhoofisha mh Lema kisiasa na mipango na mikakati yote ilikuwa ikifanywa baina yangu mimi, wewe Dr Kitila Mkumbo pamoja na madiwani waliofukuzwa Chadema.
Onesha onnetion mkuu,ZItto anapendwa na vijana wanataka kumtumia yeye hawataki.Ndio maana wanakuja kurumbana hapaKazi ipo sana. Kwa hali hii CDM kuingia Magogoni ni ndoto. Kumbe wasaliti mpo wengi sana? Mchange, Saanane, Zito wote hamna kitu. Kwanini msilumbane kwenye mikutano yenu huko tukajua kama mna nia njema na CDM. Napata picha nyinigine, Zito ni mbaya kuliko wengine wote hapo kwani kila linalozungumzwa lina connection na zito kwanini? kuna kitu kimejificha, Slaa na Mbowe hebu fanyeni uchunguzi kukinusuru chama
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.
Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.
Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.
Palipo ukweli, uwongo hujitenga .
hicho ndiyo chama makini kimejaa vijana wasomi kutoka chuo kikuu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mchange anasema Ben ndiye alikuwa kiongozi wa kundi la PM7 na katika hatua za hawali kwa mujibu wa maelezo ya Mchange, anasema Ben ndiye alikuwa anahitisha vikao mbali mbali na kuwaudumia yeye mwenyewe...
Na kwa majibu ya Ben ya jana ana mtaja Mh. Zitto kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa kundi na alidiriki kuwapeleka kwa Mganga wakale kiapo cha kutosaliti kundi lao.....
Nadhani vijana wamefunguka vizuri sana, hapa ni sisi kuchambua hoja zao na mwisho wasiku tutajua nani mkweli na nani muongo.
Hata hivyo chadema ina kazi kubwa sana, kama vijana wenyewe ambao tulikuwa tunawategemea na kufuata nyendo zao ndio hawa basi safari ya ukombozi ni ngumu sana kuliko tulivyo kuwa tukidhania...
hizo ndo siasa..ukitaka kuwa mwanasiasa lazima ukubali kuplay dirty,ukijilegeza wenzako wanakupiga bao.nadhani zito atakuwa ameelewa sasa What is he agaisnt.
Ofcourse, wanatoa maelezo yanayomaanisha kwamba tokea mwanzo ben amekuwa akiendesha mikakati ya kiharamia dhidi ya chama, na wanaonyesha kwamba hawakuwahi kukubaliana nae hata mara moja, na wanaonyesha kwamba walijua alikuwa anatumwa kwa nini hawakumlipua mapema.
mpaka sasa hawa watu mbele yangu wanahatia
Naona unajiliwaza na kujifariji mkuu.
Zitto hopless sana,hebu jaribuni kuzisoma posts za mchange na juliana shonza jinsi wanavojaribu kujinasua nasua kwenye shutuma hizi na kuishia kulalama ya kwamba ben msaliti beni msaliti wa chama,,!!yani kauli zao hazina mashiko kabisa,so so childish
hakuna ambae hajui ya kwamba ben nae kakisaliti chama,,yeye mwenyewe kasema ivo na amekiri ya kwamba alikua anakihujum chama na hao kina zitto wakiwemo,aliwasihi wenzake kuamua kusitisha harakati hizo kwa maslahi ya chama ila wenzake waliendelea kwa sababu zenye manufaa juu yao,shonza na wenzako kuja hapa na kushupalia kumjibu ben saa nane personally bila kujibu shutuma zilizotajwa ni ukanjanja wa hali ya juu sana,,
na inaonesha kabisa na kwa kiasi gani mlivyo na akili za kitoto,tunataka ukweli tuuskie na sio blah blah na kujinasua nasua kwenye madudu mliyoyafanya,,kama siku zote walikua wanafaham zitto na ben saa nane wanahujum chama walikua wapi kuacha kuyafikisha hayo katika vikao vya chama wanalalamika waende kuyazungumza leo??
broken adults..
Mods tunaomba hii iambatanishwe.Naona nyakarungu kafunguka,na anahamu Ben apeleke ushahidi mbele ya chama haraka sanaCOPIED AND PASTE from facebook:
Grayson M. Nyakarungu
‎@All, hakuna kinachofanyika zaidi ya ccm kufaidi sasa, mtatawanyika na hakuna atakayewakusanya hata kwa miruzi ya zomali, naona vijana mnaojiita makamanda mkitukanana mkidhania ndio siasa, niliwahi kuonya tabia ya kujiweka kwenye utamaduni wa kutukana viongozi wa serikali hovyohovyo bila kujifunza hoja, na tabia hii imekuwa na kuota mizizi, dhambi yetu inageuka na kututafuna wenyewe, Ben Wa Saanane tumekutana wakati wa mchakato wa bavicha hapo ndipo tulipofahamiana na baadae tukawa tunakutana na kujadili namna gani tutajenga mtandao wa kiharakati wa vijana usio wa chama cha siasa, ila yote yalikufa baada ya mimi kwenda mwanza kazini kwangu, mimi na ben hatujawahi kupanga njama asemazo na wala kumjadili kiongozi wa kitaifa, mwajua mnafiki ataumbuka yeye tu..naomba ben uwahishe ombi lako kwa chama ili utoe huo ushahidi usemao, pia wewe ben ulikuwa ukilalama sana eti kila unapomtafuta zito anakuwa busy hamjawahi kukaa kila siku story yako ni kuwa unatarajia kuonana nae, sasa ndugu yangu ben tena nakusihi sana uje na hizo documents zako fanya haraka!!!
Ben saanane anakiua chama,Ben ameamua kutafuta mafao ya mwakaWote hapa tunajua Ben alikuwa msaliti kama alivyokiri mwenyewe hapa...
Sasa hawa nao badala ya kujibu hoja juu ya tuhuma zinazowakabil wanakuja na viroja vingine eti Ben ni msaliti, ingali nawao walikuwa kwenye kundi moja na Ben ambao sasa wamebaki huko kama Masalia na wanachofanya sasa ni kujaribu kumchafua Ben ili wao waonekane wasafi tena kwa hoja dhaifu.