VUVUZELA
JF-Expert Member
- Jun 19, 2010
- 3,103
- 786
Beki wa Vijana ataka uraia wa Italia |
JACKSON ODOYO MTANZANIA anayecheza soka Italia, George Mtemahanji amesema ataomba uraia wa Italia. Mtemahaji, ambaye anachezea Modena FC inayocheza Ligi Daraja la Pili nchini Italia, atakuwa anafuata nyayo za Mtanzania mwingine Patrick Mtiliga, ambaye anachezea Malaga ya Hispania, ambaye aliutosa uraia wa baba yake Mtanzania na kuchukua ule wa Denmark, ambako amechezea mara nne timu ya taifa ya nchi hiyo. Beki huyo aliiambia Mwanaspoti kuwa anataka kutumia mwanya wa Italia kuruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili. Mtemahaji, ambaye kwa sasa yuko katika kambi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chinia ya miaka 23, alisema atalazimika kuomba uraia ili acheze soka huko bila bughudha. Alisema ataomba mwakani uraia huo kwa kuwa ameishi kwa miaka tisa tu nchini Italia, ambako sheria inaruhusu kuomba uraia baada ya kuishi miaka 10 nchini humo. �Sijaomba uraia wa Italia kwa sababu sijafikisha miaka kumi huko, huwezi kupewa uraia kama haujamaliza miaka 10 ndani ya nchi hiyo. "Kwa sasa nina miaka tisa tangu nilipokwenda hivyo ninaimani kwamba mwakani nitachukuwa uraia na wanaruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili,� alisema Mtemahaji, ambaye anaishi na wazazi wake huko Italia. Hata hivyo, kuna serikali ya Tanzania nayo imeandaa mpango wa kuruhusu Watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili. Akizungumzia timu ya taifa ya vijana, Mtemahaji mwenye umri wa miaka 18, alidai hajafurahishwa mazoezi ya timu hiyo. Beki hiyo, alidai mazoezi anayopewa na makocha Jamhuri Kiwelu `Julio' na msaidizi wake Mohamed Ayoub alifundishwa wakati akiwa na umri wa miaka 12 nchini Italia. �Sioni kitu kipya katika mafunzo ya walimu wa timu hii kwa sababu hayo wanayofundisha hivi sasa nilishajifunza nikiwa na miaka 12,� alisema Mtemahaji, ambaye ameonyesha umahiri mkubwa katika kulinda lango na kupanda mbele kusaidia mashambulizi. Mtemahaji alidai anataka mafunzo kama ya huko Ulaya yanayoweka katika mkazo wa namna ya kucheza mpira wa kasi, kutumia akili na nguvu. Source: Mwanaspoti |