Bunge la Ujerumani laondoa Vikwazo vya kupata Uraia Pacha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Bunge la Ujerumani limeidhinisha sheria inayorahisisha kanuni za kupata uraia na kuondoa vikwazo kwa watu kuwa na uraia pacha.

Serikali imetoa hoja kuwa mpango huo utasaidia ujumuishwaji wa wahamiaji na kuwavutia wafanyakazi wenye ujuzi kufanya kazi Ujerumani.

Bunge la Ujerumani lilipiga kura 382 dhidi ya 234 kwa ajili ya kuupitisha mpango huo uliowasilishwa na muungano wa vyama vinavyounda serikali inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz. Wabunge 23 hawakupiga kura.

Sheria hiyo mpya itawafanya watu kuwa na sifa ya kuomba uraia wa Ujerumani baada ya miaka mitano au miaka mitatu ikiwa atakidhi viwango maalumu. Watoto waliozaliwa Ujerumani watakuwa raia moja kwa moja ikiwa mzazi mmoja amekuwa mkaazi kwa miaka mitano, tofauti na minane ya hapo awali.

Vikwazo vya kuwa na uraia pacha navyo vitaondolewa. Kabla ya mageuzi haya watu wengi kutoka nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya na Uswisi, walitakiwa kuukana uraia wa nchi zao ili kupata Uraia wa Ujerumani.

Serikali inasema kuwa asilimia 14 ya idadi ya watu ambayo ni zaidi ya watu milioni 12 waishio Ujerumani hawana uraia wa Ujerumani na kwamba milioni 5.3 kati ya hao wameishi nchini humo kwa takribani muongo mmoja.

Mwaka 2022 takribani watu 168,500 walipewa uraia wa Ujerumani idadi hiyo ikiwa ni kubwa zaidi tangu mwaka 2002. Idadi hiyo ilichochewa na ongezeko la raia wa Syria waliopata uraia kwa kuasiliwa katika muongo mmoja uliopita.
 
Kwa Ulaya sawa, ila kwa Africa ni hatari sana, nilikuwa namfuatilia yule Isabela Donsantos wa Angola, mwana Dada ana uraia pacha wa nchi kama 5 hivi, Angola, Hispania, Ureno, Uingereza na Russia kapiga ufisadi Angola na sasa anaishi labda Hispani au Ureno akiwa kama Raia kamili.
 
Back
Top Bottom