Beki wa Vijana ataka uraia wa Italia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beki wa Vijana ataka uraia wa Italia

Discussion in 'Sports' started by VUVUZELA, Aug 3, 2011.

1. VUVUZELA

VUVUZELA JF-Expert Member

#1
Aug 3, 2011
Joined: Jun 19, 2010
Messages: 3,106
Likes Received: 11
Trophy Points: 135
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"]Beki wa Vijana ataka uraia wa Italia[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #FFFFFF, align: left"]JACKSON ODOYO
MTANZANIA anayecheza soka Italia, George Mtemahanji amesema ataomba uraia wa Italia. Mtemahaji, ambaye anachezea Modena FC inayocheza Ligi Daraja la Pili nchini Italia, atakuwa anafuata nyayo za Mtanzania mwingine Patrick Mtiliga, ambaye anachezea Malaga ya Hispania, ambaye aliutosa uraia wa baba yake Mtanzania na kuchukua ule wa Denmark, ambako amechezea mara nne timu ya taifa ya nchi hiyo.

Beki huyo aliiambia Mwanaspoti kuwa anataka kutumia mwanya wa Italia kuruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili.

Mtemahaji, ambaye kwa sasa yuko katika kambi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chinia ya miaka 23, alisema atalazimika kuomba uraia ili acheze soka huko bila bughudha.

Alisema ataomba mwakani uraia huo kwa kuwa ameishi kwa miaka tisa tu nchini Italia, ambako sheria inaruhusu kuomba uraia baada ya kuishi miaka 10 nchini humo.

�Sijaomba uraia wa Italia kwa sababu sijafikisha miaka kumi huko, huwezi kupewa uraia kama haujamaliza miaka 10 ndani ya nchi hiyo.

"Kwa sasa nina miaka tisa tangu nilipokwenda hivyo ninaimani kwamba mwakani nitachukuwa uraia na wanaruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili,� alisema Mtemahaji, ambaye anaishi na wazazi wake huko Italia.

Hata hivyo, kuna serikali ya Tanzania nayo imeandaa mpango wa kuruhusu Watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili.

Akizungumzia timu ya taifa ya vijana, Mtemahaji mwenye umri wa miaka 18, alidai hajafurahishwa mazoezi ya timu hiyo.

Beki hiyo, alidai mazoezi anayopewa na makocha Jamhuri Kiwelu `Julio' na msaidizi wake Mohamed Ayoub alifundishwa wakati akiwa na umri wa miaka 12 nchini Italia.

�Sioni kitu kipya katika mafunzo ya walimu wa timu hii kwa sababu hayo wanayofundisha hivi sasa nilishajifunza nikiwa na miaka 12,� alisema Mtemahaji, ambaye ameonyesha umahiri mkubwa katika kulinda lango na kupanda mbele kusaidia mashambulizi.

Mtemahaji alidai anataka mafunzo kama ya huko Ulaya yanayoweka katika mkazo wa namna ya kucheza mpira wa kasi, kutumia akili na nguvu.

Source: Mwanaspoti
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: readstory"][/TD]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[/TABLE]

2. VUVUZELA

VUVUZELA JF-Expert Member

#2
Aug 3, 2011
Joined: Jun 19, 2010
Messages: 3,106
Likes Received: 11
Trophy Points: 135
Basi Tanzania makocha hatuna

3. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#3
Aug 3, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Kama ni hivyo, kuwepo na kozi za ukocha hapa nchini kama hazipo basi tupeleke wakufunzi nje wakajifunze ukocha!

4. Yo Yo

Yo Yo JF-Expert Member

#4
Aug 3, 2011
Joined: May 31, 2008
Messages: 11,247
Likes Received: 73
Trophy Points: 0
Modena FC ipi anayochezea Mtemahaji? katika squad list ya wachezaji woote hayumo.

5. Lambardi

Lambardi JF-Expert Member

#5
Aug 3, 2011
Joined: Feb 7, 2008
Messages: 10,306
Likes Received: 5,596
Trophy Points: 280
nami sijamuona hata nimetafuta sana kwenye hiyo club sijamuona hata jina lake halipo kwenye net uki search

6. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#6
Aug 3, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Kama soka la Tanzania limetofautiana miaka 12 tu toka kwa soka la Italy...bas hatuko pabaya ha ha haaa!

7. M

Masuke JF-Expert Member

#7
Aug 3, 2011
Joined: Feb 28, 2008
Messages: 4,606
Likes Received: 108
Trophy Points: 160
Campionato di vertice anche per gli Allievi Regionali di Mister Gianluca Cavazzuti, sempre tra le prime quattro posizioni della graduatoria ed importante serbatoio per gli Allievi Nazionali. Numerosi ragazzi, nel corso della stagione, si sono meritati più di una convocazione con gli Allievi di Mister Treggia ed hanno acquisito la giusta esperienza per affrontare nel prossimo anno, da protagonisti, il campionato nazionale di categoria. Diversi i record dei ragazzi di Mister Cavazzuti: la vittoria esterna con più gol (1-5 sul campo del Russi), il maggior numero di vittorie stagionali (17), maggior numero di pareggi (12), maggior numero di vittorie esterne (7) e minor numero di sconfitte esterne (3). Nella squadra più prolifica del Settore Giovanile, con 63 gol fatti, 17 su 19 giocatori di movimento sono andati a segno almeno una volta: Stefano Pecora (11 reti), Andrea Bernardo e Pietro Pannullo (9), Facundo Stik e Roberto Ansaloni (5), Andrea Guicciardi, Angelo Piscopo e George Mtemahanji (3), Federico Martinelli, Tommaso Iazzetta, Filippo Manno, Francesco Foresta e Said Mamouni (2), Andrea Di Stasio, Francesco Bosco, Francesco Munaro, Samuele Marchetti e Matteo Montorsi con una rete.

Huyo hapo kwenye red na source yake hii hapa.

Modena Football Club 1912 - Sito Ufficiale - Official Site

8. VUVUZELA

VUVUZELA JF-Expert Member

#8
Aug 3, 2011
Joined: Jun 19, 2010
Messages: 3,106
Likes Received: 11
Trophy Points: 135
Ahsante kwa kutufahamisha. Kwa hiyo hii club iko Serie B?

9. Belo

Belo JF-Expert Member

#9
Aug 3, 2011
Joined: Jun 11, 2007
Messages: 11,262
Likes Received: 4,236
Trophy Points: 280
Huyu dogo nae mzushi nakumbuka alikuwa anahojiwa na Clouds FM akasema hawezi kuukana uraia wa Tanzania

10. M

Masuke JF-Expert Member

#10
Aug 3, 2011
Joined: Feb 28, 2008
Messages: 4,606
Likes Received: 108
Trophy Points: 160

Mkuu hiyo Lugha utata mkuu, mimi nimeona jina tu inaweza kuwa ni Serie B halafu timu ya watoto.

11. M

Masuke JF-Expert Member

#11
Aug 3, 2011
Joined: Feb 28, 2008
Messages: 4,606
Likes Received: 108
Trophy Points: 160

Mkuu hiyo Lugha utata mtupu, mimi nimeona jina lake tu inaweza kuwa ni Serie B halafu timu ya watoto.

12. Chimunguru

Chimunguru JF-Expert Member

#12
Aug 3, 2011
Joined: May 3, 2009
Messages: 9,843
Likes Received: 270
Trophy Points: 180

mkuu haukani uraia wa bongo coz italy inaruhusu uraia wa nchi mbili.

13. VUVUZELA

VUVUZELA JF-Expert Member

#13
Aug 3, 2011
Joined: Jun 19, 2010
Messages: 3,106
Likes Received: 11
Trophy Points: 135
Sasa akibainika amechukua uraia wa Italy basi si itabidi aukane uraia wa kibongo la sivyo itakuwa soo akija bongo kutokana na sheria zetu?

14. georgebest

georgebest Member

#14
Mar 5, 2012
Joined: Feb 28, 2012
Messages: 23
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Kitu kinachonichekesha kua hayo maneno mimi sijasema kabisa, yule mwandishi wa habari alinihoji baada ya mazoezi pale karume na mimi nikasema maneno mengine kabisa, nimeshangaa kuona kama kwenye gazeti ameandika vingime!!! Mimi niente mtanzania na naipenda inchi yangu suoni shida ya kubadilisha uraia!!!!

15. zomba

zomba JF-Expert Member

#15
Mar 5, 2012
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Wewe nae hufahamu alichoongea? kasema Italia wanaruhu Uraia wa nchi mbili, sasa hapo hana sababu ya kuukana Utanzania, labda Utanzania umkane yeye.

16. georgebest

georgebest Member

#16
Mar 5, 2012
Joined: Feb 28, 2012
Messages: 23
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Asante ribosome kua umenielewa, kitu strage ni kua odoyo ameandika alichoelewa yeye sio nilichosema mimi. Mimi narudia tena naipenda sana inchi yangu siwezi kuikataa lakini serekali inabidi ijue kua niente important kuweka possibility ya kuchukua Uraia wa inchi zingine.

17. Maundumula

Maundumula JF-Expert Member

#17
Mar 9, 2012
Joined: Nov 4, 2010
Messages: 7,055
Likes Received: 74
Trophy Points: 145
Akibadili atakuwa amefanya la maana hapa bongo hamna mpira kabisa

Loading...