Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 21,838
- 38,729
Zamani sana Jijini Milan nchini Italia miaka 16 iliopita kulikuwa na jina la Playmaker mmoja mstaarabu mno, muungwana kutoka Mji wa vipaji wa Sao Paulo ni kama vile Morogoro kwa Tanzania, Ricardo Izecson dos Santos Leite maarufu kama 'Kakà'
Nani asiyemkumbuka fundi huyu ambaye anatua uwanja wa ndege wa Malpensa kwenye kitongoji cha Varese pale Italia na biblia yake, Waitaliano wanamtazama Silvio Berlusconi na Carlo Ancelotti, nyie vipi mnatuletea mtoto laini huyu, ataweza kweli soka la Italia, ataweza kweli kupasua Catenacio na Uchawi mweusi kwenye kujilinda?
Maswali yalikuwa mengi ila Kakà alijibu juu ya nyasi za San Siro, aliwapa majibu wale wahafidhina wa Milano, Fossa de Leoni kundi la mashabiki lilofunguliwa mwaka 1968 japo 2005 lilisambaratika, hawa walivua kofia kwa Mbrazil huyu ambaye hakuwa na mambo mengi kwenye kazi yake, but he kept things ticking
Ancelotti aliamini Kaka anafaa kuungana na Andriy Shevchenko na Philpo Pippo Inzaghi kwenye eneo la mwisho, Carlo aliamini miguu ya Manuel Costa na akili yake haiwezi tena kufanya hata nusu ya ubora wa Kakà, fundi huyo alitengeneza hub pale kati kila kitu kilikuwa moto
Kule nchini kwao Brazil ilimlazimu Kocha wa timu ya taifa ajifungie kwenye office za CBF, kufikiria anamtumiaje Ricardo kwenye mfumo wake, Carlos Alberto Pereirra alikuja na 4-2-2-2 ili awe tu na fundi wa Sao Paulo
Una the Mighty Brazil yenye namba 9 ya Ronaldo De Lima, una namba 10 ya Dinho wa Gaucho kisha una straika mwingine mwenye mnuso wa bundi kama Adriano, kazi ya Kakà ilikuwa ni kuunganisha, kupikia na kuwafanya wawe free kule mbele, ikumbukwe hakuwa mchoyo
Kiungo chake kilikuwa sio cha kupiga pass tu, bali kuhakikisha imefika tena kwa mlengwa, kiungo chake hakikuwa cha kuwachezesha tu mastraika bali kuhakikisha amedigest kila kitu, alikuwa mwepesi kwenye kupunguza mabeki, he had flamboyant skills
Unataka tuseme nini kuhusu ucha Mungu wake? Wakati Pato anaenda Milano aliwahi kuulizwa na De Lima, unamfata Kakà au Mimi, yani unataka maisha ya dini au maisha ya bata😂 De Lima alitaka kumpa jarida la Playboy kijana Pato
.
Hii dunia wamepita watu bwana kwenye soka.