Magari ya kuzoa takataka na yenyewe ni takataka, yanafanya nini barabarani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu salama?

gari taka.jpg

Hivi umeshawahi kukutana na gari la kuzoa taka lenye hali nzuri? Magari yote ambayo nimewahi kukutana nayo yanakuwa yameisha, yana hali mbaya, kutu kila pahala, yametoka, na yanajikokota kwelikweli kutoka eneo moja kwenda eneo jingine!

Kwanini magari haya yanaruhusiwa kufanya kazi katika hali hiyo? Yaani ni kama upo na bomu, hata ukajigonga tu bahati mbaya likakuchana na msala! Uwajibikaji kwenye suala zima za uzoaji taka ni 0 sifuri, utafikiri hakuna watu wanaosimamia eneo hilo.

Ni kwamba wanaopewa tenda hawapewi standard ya vifaa wanavyotakiwa kutumia kukamilisha kazi hiyo, hapo hujaongelea mazingira na vifaa wanavyotumia wazoaji taka wenyewe, huu utakuwa mjadala wa wakati mwingine.

Kwanini magari haya yanaruhusiwa kufanya kazi?
 
hizi gari ni za wakubwa huko trafiki ndo manake haziguswi mkuu!!!
 
Kazi kwelikweli, hizi skrepa hazitakiwi kuwa barabarani kabisa
Hizo ni gari pekee ambazo askari wa traffic barabarani hawezi zisimamisha wala kuomba rushwa

Hao ndio wanaume wa mjini wenye mji au jiji hata mpita njia akiona limepaki linapakia hupita mbio huku kabana pua
Wababe wengine ni wale wabeba mavi ya chooni traffic hasimamishi kukiwa na foleni ataenda kuvuta foleni lipite walipo haraka
 
Ahhh Mkuu, usiwashushe kiivyo bwana
Huo ni ukweli mchungu mkuu, watu wanapoanza kufanya hiyo kazi kwa mara ya kwanza, huwa ni smart kabisa, ila akisha jiingiza kwenye hiyo kazi, jumla anakuwa chokoraa( kula mabaki ya viporo vya jalalani, soda zilizotupwa na n.k)
 
Taka si zinazolewa lakini? Shida nini? Magari yenyewe Isuzu za miaka 40 max speed ni 20 km/hr hazina shari labuda steering au breki zizingue
 
Hayo magari ni mali binafsi za maofisa usalama barabarani, hayawezi kukamatwa japo hayafai
Sio kweli ya kwao ni yale magari ya breakdown mabovu kuanzia breakdown zile land-rover za zamani hadi malori ma breakdown na mengi ni ya Askari hasa wazee wastaafu wa polisi hasa waliokuwa kitengo cha Traffic
 
Taka si zinazolewa lakini? Shida nini? Magari yenyewe Isuzu za miaka 40 max speed ni 20 km/hr hazina shari labuda steering au breki zizingue
Hazitakiwi kuwa barabarani, zinaweza kuleta majanga majanga kibao, hazina viwango tena vya kuendelea kutembea barabarani
 
Back
Top Bottom