KERO Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari JF,

Ni wiki na zaidi sasa maji yamekuwa yakitoka machafu hivi na wakati mwingine huwa machafu zaidi na yenye harufu mbaya.

Niliuliza kwa mjumbe maana ni jirani yangu kama anakutana na tatizo hilo nikitaka kufahamu huenda ni mimi tu, naye akasema yapo hivyo na kwake pia (maji yalikatika usiku pekee kwa kama siku tatu mfululizo pia ambapo kwake nako alipata shida hii, sasa hivi hili limekoma) na kwamba ni DAWASA wanafanya marekebisho ya mabomba.

Lakini hali hii haijakoma toka nimuulize inakaribia wiki, na kumbuka mpaka naenda kumuuliza ni masiku yamepita maji yanatoka machafu hivi kama mnavyoona kwenye picha.

Hii sio sawa na ni hatari kwa afya zetu, vipi kama maji haya yanachanganyika na maji ya chooni, maana siku nyingine yanakuwa na harufu nzito, kama sasa hivi hii harufu inanipa mashaka huenda yamechanganyika na maji uchafu, jambo ambalo linaweza kuleta magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu, kuhara nk.

Haya ni maji niliofungulia kwenye sinki la kunawia mikono, yametoka moja kwa moja kwenye bomba, hayajaongezwa kitu chochote
20240224_085629.jpg


Hiki choo sio kichafu ndugu zangu, ni cheupe kote, na hapo nimeflashi mara mbilo, maji yakitulia vumbi linatulia chini kama hivyo. Kama ningeacha yatulie kwenye sinki la mikono yangekuwa kama hayo. Na yanatoa hafuru mbaya. Haya si magonja tunatafutiwa ndugu zangu?

DAWASA mtupe ufafanuzi kwenye hili na mje kurekebisha mlipoharibu. Ni maeneo ya Mbezi Beach kwa Zena.
20240224_085422.jpg
 
Wengine uku Mbezi Luis mabomba yanakoroma tu mpaka leo hamna maji
 
Hali inazidi kuwa mbaya. Jana nimerudi home na mijasho ila kuona maji yalivyo machafu bafuni, nikaona bora nipigwe na feni tu nipoe.
 
Ni machafu, ukioga badala ya kutakasika unachafuka pamoja na harufu mbaya. Kulikoni DAWASA??? Tuombe uwe uchafu unaotokana na matope baada ya kuzibua bomba ila isiwe uchafu wa chooni.
 
Back
Top Bottom