Be aware na tamthiliya ya Be Careful With My Heart

Be aware na tamthiliya ya Be Careful With My Heart

Habari zenu, nadhani kuna baadhi yetu wanafatilia ile tamthiliya ya Be Careful with My Heart inayoonyeshwa katika luninga ya Star TV. Sasa mimi pia ni mdau huwa nakaa naangalia na familia akiwemo msichana anaenisaidia kazi za nyumbani.

Sielewi yeye alikua anaichukuliaje ila nadhani anajifananisha na Maya yule. Nina mtoto mdogo wa kike. Nikawa naona anazidisha mapenzi kwa yule mtoto nikaona sio mbaya.

Pili kuna wakati mume wangu hupendelea chai mida ya jioni sasa pale akiagiza chai inakuwa kama tunagombania kwenda kuandaa na yeye. Mimi huwa nanyanyuka nikijua ni wajibu nakuta mwenzangu yuko jikoni tayari.

Mwanzoni hakua kiherehere hivi nikakumbuka mambo ya chief kuipenda kahawa ya Maya nikajipa moyo niache mawazo machafu. Sasa leo ndio nikaona too much yani alipotoka kuoga kajipulizia perfume nyumba nzima inanukia.

Nikakumbuka jinsi Maya alivyojipulizia perfume nyingi ile episode ya jana. Nikamfata chumbani nikamwambia kulikoni mperfume wote huo? Akasema hamna kitu.

Nikamwambia unajipulizia umvutie nani? Akasema sina hayo mawazo. Nikamwambia hayo unayoyaona kwenye tamthiliya ni maigizo. Na hata yangekua kweli yule Sir chief mkewe amekufa.

Sasa usikae busy kutaka kumfurahisha mume wangu mi bado niko hai. Hakujibu kitu nikawaza tu huyu sir chief kazua jambo. Haa!

Competition ni faida kwa consumer.
 
star tv nao wahuni sana sijui imekuaje wameikatisha ile tamthilia
Mheshimiwa Dialo TASAVALI WAMBIE VIJANA WAKO
 
Akili ya shule na ya maisha tofauti, ma prof wangekuwa wanaongoza kwa maisha mazuri, na std 7 wangekuwa ma hg wote.


Kubali, anakuzidi ujanja, kwanza anajua anachokitaka, anajua atakipataje, anajifunza haraka kulingana na mazingira yake, anachagua nini cha kujifunza kumfikisha atakapo.


Wewe kwako ni tamthilia ni burudani tu, yeye kwake ni burudani na shule.


Sema tu alichochagua kujifunza kina conflict of interest na boss wake, so rahisi yeye kupotzwa kwenye game. Ila akichange malengo yake akajikita mfano kwenye biashara, na akajifunza na kujaribu ku-implement kwa kasi hii hii humkuti pamoja na elimu yako.


Some people are born like that, just clever, shuleni wanapigwa msasa tu.

Clever kwa zero yake aliopata form four au kuiga kila akionacho bila kupima faida na hasara?
 
star tv nao wahuni sana sijui imekuaje wameikatisha ile tamthilia
Mheshimiwa Dialo TASAVALI WAMBIE VIJANA WAKO

Wamesema week hii haitokuwepo kutokana na sababu zlzo nje ya uwezo wao eti
 

MamaBeata umenichekeshaje?
Ni true story hii?

Lakini I'm against kumwonyesha housegirl insecurities zako na mume wako. Heshima yako inaondoka. Atakuwa very confident na kujiona kama mke mwenza sasa.

Lakini ni kweli unaweza kubabaishwa na housegirl? Unfortunately Sijawahi kupata housegirl aliyenitisha.

Ndo madhara ya kuwa na urafiki mno na maHousegirl. She is supposed to know from the beginning who is the Alpha Female.

pole.
 
Last edited by a moderator:
Tamthilia ya mwisho kuangalia ilikuwa ni la revancha ya akina aljandro na soledad enzi nikiwa primary school..

Baada ya hapo, mzuka wa tamthilia ukafia mbali after economics dominating my head...

Heri yenu mnaoendelea kufuatilia..
 
Tamthilia ya mwisho kuangalia ilikuwa ni la revancha ya akina aljandro na soledad enzi nikiwa primary school..

Baada ya hapo, mzuka wa tamthilia ukafia mbali after economics dominating my head...

Heri yenu mnaoendelea kufuatilia..

Revancha ulikuwa primary...?

Naomba shikamoo yangu tafadhali.
 
Mi naona mama mwenye nyumba hujiamini kabisa. Mwache house girl apendeze bana-ni haki yake. Kisha si ulimwajiri ampende mwanao na achape kazi? Mbona unaona kufanya hivyo ni kiherehere.

Mi naona kama unakesha kawe ukilinda bahari wakati coco wanavua kama kawaida...

Vita havipiganwi hivyo kwa sababu kila anayependeza ukiona kama ni hatari kwa ndoa yako, mbona wanaofanya kazi na mumeo ni majanga zaidi? Mwache housegirl aexperience maisha aone jinsi maigizo yalivyo maigizo.
 
ha ha ha utani utani unakuta unarudishwa kijijini kaa chonjo

tamthilia ni nzuri sana ila weekend hii wametukatili hawajaionyesha wameniudhi mno yaani maya ananichekesha moja na pozi zake
 
Tamthilia ya mwisho kuangalia ilikuwa ni la revancha ya akina aljandro na soledad enzi nikiwa primary school..

Baada ya hapo, mzuka wa tamthilia ukafia mbali after economics dominating my head...

Heri yenu mnaoendelea kufuatilia..

mary soledad?,kama ndo hiyo mbona ya juzi tu,kumbe wewe ni mdogo sana.
Ilishia vipi maana chanel ten waliikatisha njiani.
 
Clever kwa zero yake aliopata form four au kuiga kila akionacho bila kupima faida na hasara?

aisee usicheze na mabinti anaweza akawa ana zero ila ana one kwenye mengine ndo maana yupo kwako anakusaidia kazi na zero yake....!
 
Hawa star tv wazushi kweli umewafagilia humu halafu leo hawajaionyesha saa zingine wanatuboa kweli hawana msimamo wanaotushikia akili kama mshahara wa serikali.
tamthilia za kimexcan zinazoonyeshwa capital tv ndo huwa wanadeliver.hakuna kuishia njiani wala kukatisha hadi inafika mwisho.
 
Tamthilia ya mwisho kuangalia ilikuwa ni la revancha ya akina aljandro na soledad enzi nikiwa primary school..

Baada ya hapo, mzuka wa tamthilia ukafia mbali after economics dominating my head...

Heri yenu mnaoendelea kufuatilia..

Kazi na dawa bana.
 
Tatizo letu wabongo Tamthilia tunazichukulia kama burudani tu lakini sio maana yake yale wakati mwingine ni mafundisho huwa tunapewa tunapaswa tuchukue mazuri mabaya tuwaachie wenyewe.

Huyu bekitatu anaakili amechukua mazuri ambayo yeye kwa mtazamo wake ndio ameona mazuri na mabaya amewaachia wenyewe.

mbona hakuwaiga wengine ameona style ya maya inamfaa na usipokua makini huyo bekitatu atakuliza shost .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom