RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Hatari Wana JF,
Baada ya takribani siku kumi za amshaamsha ya mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu kuigongesha CCM na mgombea wake kwenye majukukwa ya kampeni, ni dhahiri kuwa Magufuli na CCM yake waweza kuwa chama cha upinzani kwa Mara ya Kwanza katika historia ya taifa hili, 'assuming' Tume ya uchaguzi ni huru.
Mwitikio wa sera anazonadi ndugu Tundu Lissu na Chama chake miongoni mwa wananchi ni mkubwa sana na mijadala ya uwezo na maono yake makubwa kwa taifa la Tanzania vinazidi kushika Kasi.
Pamoja na ukweli kuwa ndugu Tundu Lissu anamhenyesha vilivyo Magufuli na CCM yake kwenye kampeni za majukwaani, lakini Kuna kundi hili kubwa la kina mama katika rika zao zote zile zenye umri wa kupiga kura.
Akinamama wa nchi hii mimi binafsi sijui saikolojia yao ikoje. Ila mara nyingi wakati wa kampeni hujazwa hofu na CCM kuwa iwapo watachagua vyama upinzani, basi vita itatokea na wao wataachwa wakiteseka na watoto.
Hofu hii hukipatia CCM kura nyingi kutoka kundi hili ambalo likiwekwa sawa likajiamini, Tanzania ya Tundu Lissu tunaweza kuiona.
Kwa maana hiyo ni rai yangu kwa Baraza la Wanawake wa Chadema liamuake sasa, sumu ya hofu imeshaanza kusambazwa kwa Kasi kubwa.
Ndiyo maana kukawa na BAWACHA, mambo yenu akinamama mnayajuwa wenyewe, msaidieni Tundu Lissu sasa mapema iwezekanvyo, msisubiri dakika za majeruhi, jeshi kubwa muanze sasa.
Heri mimi sijasema.