mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda akiwa mkoani singida Makonda Januari 25, 2024 amesema kuwa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuna mgawanyiko unaochochewa na uwepo wa makundi mawili ambayo yote yanataka kumuweka Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa
Kundi la kwanza ni lile linalomuhusisha Mwenyekiti aliyepo madarakani Freeman Mbowe na kundi la pili linaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu.
Makonda ameongeza kuwa hata Lissu anajua hakuna chama chochote kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya CCM, ndio maana ameamua kuishi nje ya nchi na kuja Tanzania kimatukio, uchaguzi ukiwadia anakuja, matokeo yakitoka anarudi kwake. Haijulikani makazi yake yapo Tanzania au nje ya nchi.
''Kwenye kuongoza nchi anajua pia hawezi na ndio maana ameamua kuishi huko na kuja Tanzania kimatukio. Akisikia uchaguzi anakuja, matokeo yakitoka anarudi kwake. Sasa sijajua makazi yake yapo wapi kwamba yapo Tanzania halafu kule ni ofisi au kule ni ofisi makazi ni Tanzania!"