Uchaguzi 2020 BAWACHA amkeni, uwezo wa kumfanya Tundu Lissu awe Rais wa Tanzania uko mikononi mwenu kwa sasa

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
963
1,927
Hatari Wana JF,

Baada ya takribani siku kumi za amshaamsha ya mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu kuigongesha CCM na mgombea wake kwenye majukukwa ya kampeni, ni dhahiri kuwa Magufuli na CCM yake waweza kuwa chama cha upinzani kwa Mara ya Kwanza katika historia ya taifa hili, 'assuming' Tume ya uchaguzi ni huru.

Mwitikio wa sera anazonadi ndugu Tundu Lissu na Chama chake miongoni mwa wananchi ni mkubwa sana na mijadala ya uwezo na maono yake makubwa kwa taifa la Tanzania vinazidi kushika Kasi.

Pamoja na ukweli kuwa ndugu Tundu Lissu anamhenyesha vilivyo Magufuli na CCM yake kwenye kampeni za majukwaani, lakini Kuna kundi hili kubwa la kina mama katika rika zao zote zile zenye umri wa kupiga kura.

Akinamama wa nchi hii mimi binafsi sijui saikolojia yao ikoje. Ila mara nyingi wakati wa kampeni hujazwa hofu na CCM kuwa iwapo watachagua vyama upinzani, basi vita itatokea na wao wataachwa wakiteseka na watoto.

Hofu hii hukipatia CCM kura nyingi kutoka kundi hili ambalo likiwekwa sawa likajiamini, Tanzania ya Tundu Lissu tunaweza kuiona.

Kwa maana hiyo ni rai yangu kwa Baraza la Wanawake wa Chadema liamuake sasa, sumu ya hofu imeshaanza kusambazwa kwa Kasi kubwa.

Ndiyo maana kukawa na BAWACHA, mambo yenu akinamama mnayajuwa wenyewe, msaidieni Tundu Lissu sasa mapema iwezekanvyo, msisubiri dakika za majeruhi, jeshi kubwa muanze sasa.

Heri mimi sijasema.
 
Mkuu CCM ina wanachama wengi vijijini.

Ambako CHADEMA ili kuitaji wanachama wengi zaidi wanatumia lugha zenye mlango wa matusi na dharau kitu ambacho wamama na wazee wanabaki kushika vichwa.

Lakini kwa jambo hilohilo ambalo MJINI SI MATUSI NI SEHEMU YA SIASA.

Kwa sasa upinzani hauhitaji dola na kamwe LISU hawezi kuwa Rais hata vyama vyote vikiungana.

ILA!
Kumuondoa NDULICCM inahitaji nguvu ambazo hazina tamaa ya RUZUKU NDANI YAKE. (UMOJA)
 
Mkuu CCM ina wanachama wengi vijijini.

Ambako CHADEMA ili kuitaji wanachama wengi zaidi wanatumia lugha zenye mlango wa matusi na dharau kitu ambacho wamama na wazee wanabaki kushika vichwa...
Mi sijaona matusi katika kampeni za Chadema!

Kampeni za CCM ndizo zinachezesha wasanii hadharani wakiigiza mambo ya ngono mbele ya watoto wetu.
 
BAWACHA NI KIKUNDI CHA MACHECK BABIES WA MJINI, HAWATAKUBALI KUFANYA KAZI KAMA ANAZOFANYA MAMA KABAKA KULE CCM, BWAWACHA KUFIKA VIJININI KWAO NI NDOTO WAKO MJINI TU, BAHATI MBAYA MIJINI HAKUNA WAPIGA KURA WANAOJITAMBUA, WENGI WANAHUDHURIA MIKUTANO NA KURA HAWAPIGI. TUNDU LISSU KUSHINDA SIYO RAHISI JAPO ANGEPENDA KUWA IKULU BY NOVEMBER
 
Bawacha sio taasisi bali kijiwe cha kina mama wa kichaga wakiongozwa na halima. A.K.A bi Kidude.

Kawe maji yako shingoni, je akiondoka nani wa kuokoa jahazi
Sawa its much better kuwa hivyo ulivyowaita lakini wanapigania haki. CCM ni "genge la wanyang'anyi", ni dhambi kubwa kwa mtu wa imani kuwa na ties na CCM, ni sawa na Sheikh au Mchungaji kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kahaba.

It's a disgrace to the nation, kuendelea kuchagua CCM ni sawa na kuwalaani watoto wa taifa hili wanaokuja. Majamaa kwa miaka zaidi ya hamsini yameshindwa kuboresha maisha ya wananchi mpaka leo kuna watanzania wengi sana suala la milo mitatu kamili ni tabu, tiba wanapata kwa tabu,maji ndio usiseme, usafiri hovyo kabisa.

Halafu mnapata ujasiri wa kusema wanaleta maendeleo. Tubuni mbadilike enyi wafuasi wa CHAMA CHA MASHETANI(CCM)..."Laana ya taifa"
 
Mi sijaona matusi katika kampeni za Chadema!
Kampeni za CCM ndizo zinachezesha wasanii hadharani wakiigiza mambo ya ngono mbele ya watoto wetu.
Binafsi sijaona wasanii kwenye kampeni za CCM.

ILA NIMEONA AHADI ZAO ZA KILA SIKU TANGU UHURU sehemu moja kila awamu MAJI MAJI MAJI.
 
CHADEMA wanapaswa kuwa na mbinu nyingi ili kuweza kushinda uchaguzi.
Binafsi sijaona umuhimu wowote wa viongozi wote wa kitaifa kuambatana na mgombea uraisi.

Cha muhimu chama kilipaswa kuunda team mbalimbali kwa kuspot vichwa vizuri katika kushambulia jukwaa wapeleke mashambulizi pande zote za nchi.
Ni mambo ya ajabu sana kutegemea mbinu moja tu kupata ushindi.

Excuse isiwe eti uhaba wa fedha kwa nn hamkujipanga mapema zaidi before uchaguzi? kwa maoni yangu n bora mngeweka wagombea katika baadhi ya maeneo yanayoonekana watu wana mwamko wa mageuzi hii ingesaidia kuokoa fedha na kupanga safu nzuri kwa ajili ya kampeni ya kufa na kupona.

Mwisho watumieni vizuri watu wanaoupenda upinzani kwa dhati mfano watu km akina Malisa G kuliko kuwakumbatia waganga njaa ambao hawachelewi kuunga mkono juhudi.
 
Pia watafute wenye ujuzi ili kuboresha Chadema Media TV. Kwa sasa ni kama ina administrator ambaye kaishia darasa la nne na hana ujuzi wowote wa Information Technology.
Anayemonitor ile tv inaonekana yuko slow sana. Chadema tuko vijana wachangamfu sana na wenye fani mbali mbali. Msituangushe aisee.
 
CHADEMA wanapaswa kuwa na mbinu nyingi ili kuweza kushinda uchaguzi.
Binafsi sijaona umuhimu wowote wa viongozi wote wa kitaifa kuambatana na mgombea uraisi.

Cha muhimu chama kilipaswa kuunda team mbalimbali kwa kuspot vichwa vizuri katika kushambulia jukwaa wapeleke mashambulizi pande zote za nchi.
Ni mambo ya ajabu sana kutegemea mbinu moja tu kupata ushindi.

Excuse isiwe eti uhaba wa fedha kwa nn hamkujipanga mapema zaidi before uchaguzi? kwa maoni yangu n bora mngeweka wagombea katika baadhi ya maeneo yanayoonekana watu wana mwamko wa mageuzi hii ingesaidia kuokoa fedha na kupanga safu nzuri kwa ajili ya kampeni ya kufa na kupona.

Mwisho watumieni vizuri watu wanaoupenda upinzani kwa dhati mfano watu km akina Malisa G kuliko kuwakumbatia waganga njaa ambao hawachelewi kuunga mkono juhudi.
Mzee acha kuchanganya mambo ule ni uzinduzi wa kikanda lazima viongozi washiriki baada ya hapo tunaenda mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyumba.
 
Mzee acha kuchanganya mambo ule ni uzinduzi wa kikanda lazima viongozi washiriki baada ya hapo tunaenda mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyumba.
Ndo shida yenu UJUAJI mwingi.
Kuna kitu kibaya nmeandika hapo?
Mkubali mkatae bila kufanya kazi kama TEAM WORK ni ngumu sana kupata matokeo chanya.
 
"Assumingi tume ya uchaguzi ni huru "

Lissu kuwa raisi ni ndoto za abunuasi

Hata wananchi wampigie kura, lissu hawezi kuwa raisi

Mbona kila kitu kinajionesha

Chadema kuchukukua nchi hii sijui itakuwa baada ya miaka 10000
 
Back
Top Bottom