GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Makamu mwenyekiti wa chadema mh Tundu Lissu akiongea na diaspora wa Tanzania waishio Marekani kwenye suala la uraia pacha amegusia kuhusu maisha ya watoto wake wawili wanaosoma vyuo vikuu vya Marekani
Mosi, Tundu Lissu anasema watoto wake wawili walizaliwa Marekani katika hospitali ya George Town University miaka ishirini na moja iliyopita na hivyo wana haki za kugombea Urais wa Marekani na watoto wake hawahitaji visa kama yeye na mkewe kuingia Marekani kwani watoto ni Raia wa Marekani
Tundu Lissu amesema kwa sasa watoto wake mmoja anasoma George Town University Atalanta Marekani na mwngine anasoma Kenneth State University Marieta Georgia Marekani
Pili, Tundu Lissu amesisitiza watoto wake hawana haki yoyote ya kurithi mali zake za Tanzania kwa mujibu wa sheria za Tanzania hususani suala la ardhi kutokana ni Raia wa Marekani
Tatu,Tundu Lissu amesisitiza ni lazima suala la uraia likafikiliwa upya kwani watanzania wapo wengi wenye elimu bora lakini wanashindwa kusaidia nyumbani kutokana na sheria za Tanzania zinazominya uraia pacha
Nne, Tundu Lissu amesisitiza pia kuwa watoto hawakuwa na maamuzi ya kuzaliwa Marekani bali ni maamuzi ya wazazi, Lakini kwa sheria za Tanzania masuala ya wazazi yanawaathiri watoto ambao hawakuwa na maamuzi wazaliwe nchi gani.