Mpaka sasa nadhani hawa Anti-Magu washanyoosha mikono yao japo kimya kimya, hili jambo liko wazi kabisa kwamba hayati ametumia muda mfupi zaidi kufanya mambo makubwa yaliyowashinda maraisi wote waliowahi kuongoza nchi hii.
Iko wazi tangu uhuru nchi haijawahi kujenga reli, bwawa la umeme, flyover, Roads za kisasa kama Kimara-Kibaha highway, meli, ndege nyingi n.k n.k, hayo yote yamefanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano tu na sio miaka 50.
Zamani nilikuwa naamini kwamba miaka 10 haitoshi kwa rais kufanya mambo makubwa kumbe inawezekana kabisa mana chuma kilitumia miaka mitano tu kubadili taswira, na ndiyo maana tulitaka aongoze mpk atakapokufa na kweli mwenyezi Mungu alitusikia hayati aliongoza mpk kifo chake mana hakuna binadamu angeweza kutuongoza nchi hii ilhali Magufuli yupo hai.