Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Umeongea vizuri sana mkuu. Hapo kwenye ranking yaani kama ulikuwa kichwani kwangu! Sema huyo namba sita nina uhakika miaka ya mbeleni huko ataporomoka mpaka 108th president!
Kwa uwezo wa Mungu mkuu utasubiri sana, badala yake ni wewe utakayeendelea kuporomoka katika hako kafamilia kako ambacho hv tunavyoongea wanakupuuza tayari!
 
Halafu siyo kwamba Magufuli hakupenda kukosolewa, bali hakupenda kukosolewa kijingajinga. Alitaka constructive criticism.

Magufuli hakupenda kabisa watu waliotumiwa na mabeberu kumkwamisha makusudi, kitu ambacho mtu yeyote mwenye akili timamu asingekipenda.

Magufuli hakupenda kufuata mikumbo, na hili linamfanya kuwa mmoja wa viongozi bora kabisa wa Afrika. Angalia kwa mfano handling yake ya Covid-19, it was the best.

Magufuli alikuwa mlinzi mzuri wa rasilimali za taifa, asingependwa na mafisadi na ndiyo maana alipambana nao. Hiki kilifanya propaganda hasi dhidi yake kutoka kwa mabeberu na mafisadi wengine ziwe nyingi.

Sote tunapenda uhai, lakini serikali zote duniani huwapoteza watu wanaoonekana tishio. Ipo hivyo hata Ulaya na Marekani, ipo hivyo hata kwa awamu zilizopita hapa Tanzania. Sidhani kama kuna haja ya kumlalamikia sana. Ndiyo system zote duniani zilivyo.

Kwahiyo sioni kama kuna sababu ya kumchukia unless awe aligusa masilahi yako.
 
Halafu kipaumbele cha serikali zote duniani ni kutengeneza ajira kwa raia wake, siyo kuajiri. Na ndiyo maana serikali zote zilizoendelea zinanawirisha sekta binafsi, kitu ambacho Magufuli amekifanya sana kwa kuweka sheria na sera zinazosaidia kunawiri kwa sekta binafsi.
 
01: Magufuli alinunua nyumba ngapi yeye binafsi kati ya nyumba zaidi ya 8,000 alizosimamia uuzwaji wake? Je, sheria haikumruhusu kununua? Je, kama alitenda kosa kisheria, kwanini hakuna yeyote aliyemshitaki?

02: Magufuli amefanya maendeleo maeneo mangapi Tanzania? Je, Chato haipo Tanzania? Rais haruhusiwi kufanya maendeleo sehemu anayotokea?

03: Je, kuna Rais gani wa wakati wetu aliyependwa na wananchi kama Magufuli? Ni Rais gani wa wakati wetu aliyeeleweka kwa wananchi kama Magufuli? Ni Rais gani mwingine wa wakati wetu aliyetegemewa na kupelekewa shida directly na wananchi wa kawaida kama Magufuli?

04: Ni Rais gani wa wakati wetu aliyesimamisha miradi mikubwakubwa kama Magufuli? Ni rais gani amesimamia ujenzi wa miundombinu kama Magufuli? Ni Rais gani wa wakati wetu ameiongoza Tanzania kwa kujitegemea yenyewe kushinda Magufuli?

05: Kuna Rais gani mwingine aliyefanya ziara za ndani ya nchi na kujionea mwenyewe utendaji kazi, siyo kuletewa tu ripoti ofisini, kushinda Rais Magufuli?

06: Je, ni Rais gani wa wakati wetu amekiheshimisha kiti cha Urais na kukirudishia hadhi yake kuzidi Magufuli?

Magufulia ni Rais bora kabisa wa wakati wetu, itatuchukua muda sana kupata Rais mwingine bora na imara kama Magufuli.
Sio tu kuwa itachukua muda mrefu kumpata Rais aina ya Magufuli.
Ni kwamba hatakuja kutokea nchi hii Rais mzalendo wa kweli kama hayati Magufuli. Wenye nguvu hawatakubali hili litokee tena!
 
JPM2021. honestly baada ya Kufariki ndo nikagundua kua nilkua Namkubali...Jiwe Kweri kweri..
JamiiForums-11641031.jpg
 
Umeandika vyema. Hakika huyu alikuwa kipenzi cha watu na ninathubutu kusema MAGUFULI ndiye kiongozi bora Tanzania kuwahi kushuhudia na yote aliyoyatenda ameyatenda katika kipindi cha miaka sita tu! Tofauti na wengine,Sasa fikiria angemaliza miaka yake 10 Tanzania ingekuwa wapi sasa?.Binafsi ninaona fahari kuishi katika zama za Magufuli Mungu akinijalia umri mrefu nitawasimulia vizazi vijavyo kuhusu mtu huyu! Hakika tumeona ukuu wa Mungu kupitia mtu huyu!

Itoshe tu kusema Bwana ametoa Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
katenda yepi mapya?? binafsi ni kiongozi wa hovyo kabisa kuwahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru!
 
Naanza na no 3
Sikatai miradi kupelekwa Chato kimkakati ila napinga kwanini miradi mingi iliyopelekwa Kule Ina bajeti kubwa kuzidi uhalisia wa eneo
Kingine mingi ya miradi hiyo haikukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali wala haikupitishwa na bunge
Kingine kandarasi ya miradi hiyo haikuwekwa wazi Kama sheria inavyotaka kua tenda itangazwe na Wazabuni wajitokeze wagombee tenda kisheria ila maajabu ikapewa kandarasi Mayanga Construction ambayo Kwa tetesi inadai ni kampuni iliyokua na mkono wa Jiwe!

Hilo swala unalichukuliaje?

Hapo hujaongea Mayanga construction, ununuzi wa ndege kwa cash bila kuidhinishwa na Bunge na miradi mingine mingi.... alikuwa mpigaji tu.
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo


1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Kiongozi mwenye ushawishi. Hayati JPM alikuwa na karama ya ushawishi mbele ya jamii, alikuwa na uwezo wa kusema jambo fulani na jamii nzima ikakubaliana naye kwa asilimia kubwa, kiukweli kabisa hata leo hii JPM akiamka na akasema watanzania wachanje basi believe me dawa za kuchanja hazitatosha, hii ni kutokana na imani kubwa aliyojiwekea mbele ya jamii kwakuwa watanzania waliamini kwamba JPM ana upendo wa dhati kwa wananchi wake na hawezi kuwarubuni kwa namna yoyote ile.

6. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

7. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.

Magufuli alikua ni kiongozi mmoja very trick alicheza na akili duni za wengi kutawala kidicteta so alifanikiwa sana kuwageuza watanzania wengi kuwa magufulisim.

Kasoro kubwa katika utawala ni pale unapo wanyima haki au uhuru wale unao watawala kutoa maoni yao au kushauri waonavyoona na wao pia.
Na wanapojaribu kusema unawatangazia si wazalendo na unajibu hoja zao kwa mtutu wa bunduki au kuwapoteza .
Ni mwenye afya mbaya ya akili tu husifia maendeleo ya materials na kuwa kipofu ktk maendeleo ya watu na uhuru wa kutoa maoni yako.

Katika vipindi vyote vya utawala wa nchi hii ni kipindi pekee cha Magufuli tulishuhudia watu kupigwa risasi kama swala porini maiti kuokotwa majini zikiwa ndani ya sandarusi watu kupotea wakiwa nchini mwao kama vile wameyayuka na balafu. Kutekwa na hayo yote yanafanya na kikundi kilichopewa jina la WASIOJULIKANA kwa muda wa miaka mitano kundi hili lilihifadhiwa na ASIEJULIKANA
viongozi waandamizi kutukanwa na kukashifiwa hadharani na kusimamishwa kazi baadae kusifiwa na kurudishwa kazini. Ulikua ni utawala wa ajabu pamoja na KUPIGA HATUA KATIKA UJENZI WA MIUNDO MBINU KWA MUDA MFUPI.

Pia ni mara ya kwanza kuona Raisi pamoja na bunge kuzua mzozo na CAG kisa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katamka hadharan hali halisi ya upotevu wa pesa za serikali ktk bajet ya Raisi na Udhaifu wa bunge kusimamia serikali.

Ni mara ya kwanza ktk tawala zote za nchi hii kuona au kushuudia wafanya kazi wa taasisi za serikali na taasisi za umma ndani ya miaka mitano wakidhulimiwa haki yao ya kupandishwa madaraja na kuongezewa mshahara nao kwa ummoja wao wakaufyata pasiwe maandamano wala migomo ya madai ya kupandishiwa mashahara wakiohofia misha yao wasije wakachukuliwa na WATU WASIO JULIKANA.
 
Hapo hujaongea Mayanga construction, ununuzi wa ndege kwa cash bila kuidhinishwa na Bunge na miradi mingine mingi.... alikuwa mpigaji tu.
jamaa alikua fundi wa kufix mambo Ili aonekane innocent Kwa wajinga wajinga wasiofuatilia mambo,zile propaganda kuabudiwa kwenye media zilimsaidia Sana kuwateka nyumbu na ndio njia aliyoitumia Hittler enzi za unazi!
 
jamaa alikua fundi wa kufix mambo Ili aonekane innocent Kwa wajinga wajinga wasiofuatilia mambo,zile propaganda kuabudiwa kwenye media zilimsaidia Sana kuwateka nyumbu na ndio njia aliyoitumia Hittler enzi za unazi!
Kabisa, eti anatembea na hela anagawa kwa wanyonge. Mara yuko kanisani anaomba aombewe na kujinyeyekeza, alikuwa ni mjanja sana na alijua kundi la kujiweka nao karibu... Wajinga Wajinga.
 
jamaa alikua fundi wa kufix mambo Ili aonekane innocent Kwa wajinga wajinga wasiofuatilia mambo,zile propaganda kuabudiwa kwenye media zilimsaidia Sana kuwateka nyumbu na ndio njia aliyoitumia Hittler enzi za unazi!
Nnachowapendea Anti-Magu huwa mnakubali kwamba Magu alikuwa kipenzi cha Watz.
 
jamaa alikua fundi wa kufix mambo Ili aonekane innocent Kwa wajinga wajinga wasiofuatilia mambo,zile propaganda kuabudiwa kwenye media zilimsaidia Sana kuwateka nyumbu na ndio njia aliyoitumia Hittler enzi za unazi!
Watu walimuita Yesu mjanja mjanja, itakuwa Magufuli?
Ukweli tunaujua sisi tuliomuelewa.
 
Nnachowapendea Anti-Magu huwa mnakubali kwamba Magu alikuwa kipenzi cha Watz.
Binadamu kupendwa na kuchukiwa ni kawaida, na sio kwamba Magufuli alikua
Mbaya tu mema hakua nayo la hasha,ila Mimi binafsi Kuna mambo ambayo hua napenda kutazama Kwa jicho la tatu na kumpima kiongozi kiuweledi
Kwa mfano alipotumia nguvu kubwa kudeal na mambo madogo madogo kama kuwafanyia ukatili wapinzani wake,
Mimi kipimo cha mtu aliyekomaa kiuongozi ni pale anapo kubali mapungufu yake na kutafanyia kazi kitaaluma
Ila Jiwe alikua Sadist njia ya kuwanyamazisha wapinzania Kwa kutumia nguvu ilinifanya nijitoe mapema kua mfuasi wake!
 
Binadamu kupendwa na kuchukiwa ni kawaida, na sio kwamba Magufuli alikua
Mbaya tu mema hakua nayo la hasha,ila Mimi binafsi Kuna mambo ambayo hua napenda kutazama Kwa jicho la tatu na kumpima kiongozi kiuweledi
Kwa mfano alipotumia nguvu kubwa kudeal na mambo madogo madogo kama kuwafanyia ukatili wapinzani wake,
Mimi kipimo cha mtu aliyekomaa kiuongozi ni pale anapo kubali mapungufu yake na kutafanyia kazi kitaaluma
Ila Jiwe alikua Sadist njia ya kuwanyamazisha wapinzania Kwa kutumia nguvu ilinifanya nijitoe mapema kua mfuasi wake!
Angalia sifa ya Magu namba 2 nmeelezea kwamba alikuwa ni kiongozi mkweli daima, aliona upinzani kama ni watu waongo, wanafki na wenye tamaa ya pesa na ndiyo maana alitaka kuwaondoa wapinzani wote bungeni ili abaki na wabunge ambao atawaweza mana Magu ukishakuwa chini yake kazi unayo, sasa hawa wapinzani wa kibongo ni wachumia tumbo, Magu alipoingia tu madarakani aliwaambia washushe mshahara nchi iende wakagoma akashusha yeye peke yake.

So Magu alikuwa hapendi unafki unafiki na ndiyo maana hakutaka upinzani kabisa, upinzani wa Afrika unachelewesha maendeleo ya hili bara, utakuta nchi inahitaji kujenga stiglers gorge lakini upinzani unagoma, ukija kuchunguza kumbe wamelipwa vipesa na watu ili mradi usifanyike nchi iwe inaingiza majenereta kwa wingi.
 
Angalia sifa ya Magu namba 2 nmeelezea kwamba alikuwa ni kiongozi mkweli daima, aliona upinzani kama ni watu waongo, wanafki na wenye tamaa ya pesa na ndiyo maana alitaka kuwaondoa wapinzani wote bungeni ili abaki na wabunge ambao atawaweza mana Magu ukishakuwa chini yake kazi unayo, sasa hawa wapinzani wa kibongo ni wachumia tumbo, Magu alipoingia tu madarakani aliwaambia washushe mshahara nchi iende wakagoma akashusha yeye peke yake.

So Magu alikuwa hapendi unafki unafiki na ndiyo maana hakutaka upinzani kabisa, upinzani wa Afrika unachelewesha maendeleo ya hili bara, utakuta nchi inahitaji kujenga stiglers gorge lakini upinzani unagoma, ukija kuchunguza kumbe wamelipwa vipesa na watu ili mradi usifanyike nchi iwe inaingiza majenereta kwa wingi.
Hivi umeandika haya ukiwa timamu kabisa au umelewa?
Yaani miaka 60 Toka uhuru wapinzani ndio walikua kikwazo?

Wewe na Jiwe akili zenu za ajabu Sana Aisee unatia aibu Kwa hiyo comment yaani am sure hata MATAGA pori watakuja kukupinga Kwa nguvu zote,
Haya Sasa zile ajenda zake za kuweka Bunge la kijani zilitimia unaona kinachotokea?

Mlisema hii nchi wapinzania ndio tatizo ndani ya kipindi kifupi tu Cha bunge la kijani kuhodhi bunge wao wenyewe wameshakiri nchi bila upinzani ni sawa na kutia maji kwenye Tenga

Aliyewaamisha kua upinzani unachelewesha maendeleo baada tu ya uchafuzi wa uchaguzi akaanza kuona aibu kubwa baada hata wale raia waliomuunga mkono nafsi kuwasuta waakanza vunja Hadi katiba kulazimisha kambi rasmi ya upinzani ndio wale wabunge Covid 19 kina Mdee
Tunaowaona wakitafuna Kodi zetu Kwa Ujinga wa mpuuzi Jiwe!

Ona hata aibu shame on you kuleta hoja dhaifu!
 
Back
Top Bottom