Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Shujaa wa kweli wa Watanzania wanaojitambua. Ni aibu kubwa sana kwa Kiongozi wa Tanzania kwenda kujikomba komba huko nje na kutafuta umaarufu na kuwatukuza walio na ngozi nyeupe, ni aibu kubwa sana.

JPM ndiye mwanzilishi wa kujitegemea kwa vitendo kuanzia pesa za uchaguzi mkuu, kujenga mahospitali kila kona, kuwezesha umeme kumfikia kila Mtanzania, na mengineyo mengi.

RIP JPM. Tutakukumbuka daima.
Lugha ya malikia ilikua Tatizo kubwa akajifanya haendi nje!!!!
 
Hapendwi na nani, hebu kesho asubuhi toka hapo kwenye nyumba ya baba alafu sema kwa sauti Magu hapendwi alafu uone kichapo, pumbavu!!!
Wapumbavu ndio watakupiga wenye akili wanajua jamaa was worse ever alikua mbovu aliyejificha kwenye ukali!?? Wajinga hamjui
 
01: Alileta nidhamu serikalini

02: Aliwapigania Watanzania

03: Alipambana na ufisadi

04: Aliongeza uzalendo kwa Watanzania wengi

05: Alijenga miundombinu ya nchi hii
Alileta ukanda
Aliogopa kukosolewa
Alibeba wasukuma (hata waliofoji vyeti) bashite
Alishindwa kuongeza mushahara kwa miaka mitani ( aibu ilioje)
Alishindwa kuajiri kwa miaka mitani
Lugha ndio usiseme
Ni kiongozi wa Tz ambae hotuba zake hazita rejewa kwa ajili ya kauli alizokua akizitoa
Alijificha kwenye ukali kumbe alificha udhaufu wake
Alipika takwimu ili kuhadaa ulimwengu
Alitaka chato iwe exceptional
Aliua uchumi wa nchi na kupora pesa za watu benk
 
Hapendwi na nani? usipompenda wewe mpumuliwa kisogoni na bwana ako ndo watanzania hawampendi? mnapomtukana mitandaoni tumekaa kimya mnahisi nyie ndo wenye nchi sio? kama hapendwi mnahangaika nini kumtukana kila uchao? embu mwambieni mama na wajao waende kinyume na JPM then waone kitachowapata, vyeti vyenu feki na vile hamna cha kufanya mmebakiza kumtukana mitandaoni mnahisi watu wote hawana cha kufanya ta.ahira wewe.
Msukuma umepanic nenda jando aisee
 
JPM
FB_IMG_1616556474832.jpg
 
Tafadhali Anti-Magu mnaposema Hayati hakuwa Rais mzuri mtoe sababu ambazo zitawashawishi Magufulians kwamba kweli mpendwa wao alikuwa sio kiongozi bora, kwamba waone nyie msiomuelewa mna sababu za kutomuelewa, yani wekeni hapa sababu za kueleweka na sio kutoa sababu zisizo na mashiko na ushahidi wowote.

Sisi Magufulians tunaamini kwamba Hayati alikuwa moja kati ya viongozi bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na sababu za kusema hivyo tunazo na ziko wazi kabisa na tunaziongea kila siku, sasa nyie mnaosema hakuwa kiongozi mzuri mtuambie ni kwa vipi hakuwa kiongozi mzuri, usiishie tu kutukana haitasaidia na itatufanya tuamini kwamba mnaomchukia Magu ni chuki binafsi zaidi kuliko uhalisia na ndiyo maana mpo wachache tu na asilimia kubwa mnapatikana Jamii Forums na twitter.
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

6. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Mnaongea bila taarifa sahihi. Nakupa hii ya moto

Mafisadi wajipanga

Jamhuri September 21, 2021 Mafisadi
wajipanga2021-09-21T09:57:59+00:00Gazeti Letu, Habari za Kimataifa, page za ndani

*Ni vigogo wazito serikalini, waanza figisu ujenzi wa reli ya SGR

*Washirikiana na wazabuni wa nje kuhujumu ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’

*Waanzisha kundi wakijiita wazalendo, latajwa ni fedha mbele

*Kenya walipigwa bilioni 18.4 kila kilomita, wailengesha Tanzania

DODOMA
Na Mwandishi Wetu

Sikio la kufa halisikii dawa. Hili ndilo linaloweza kusemwa kutokana na baadhi ya wanasiasa na watendaji serikalini kuanza mpango wa hatari wa kukwamisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR; JAMHURI limebaini.

Mpango huo unaosukwa kwa umakini mkubwa, una malengo mawili. Kwanza, kujipatia fedha kwa njia yoyote ile na pili ni kuihujumu Serikali ya Awamu ya Sita kuonyesha kuwa haiwezi kusimamia ujenzi wa reli kama ilivyokuwa awali.

Hivi karibuni kumekuwapo taarifa inayosambazwa na watu wanaojiita ‘wazalendo’ ikitoa shutuma za kuhusu mchakato wa ununuzi unaoendelea vipande viwili; ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’, wakitaka utumike utaratibu uliokwamisha ujenzi wa reli tangu enzi za uhuru.

Kuna mgogoro mkubwa unapikwa chini kwa chini na baadhi ya wanasiasa na wataalamu wakitaka vipande viwili vya reli vya kutoka Makutupora hadi Tabora (Lot 3) na Makutupora hadi Isaka (Lot 4) zabuni itangazwe tena, waingize kampuni zao.

Tayari kuna kampuni kadhaa kutoka China ambazo zimewasilisha serikalini nia ya kujenga vipande hivyo na bei wanayotaka kutoza hata kabla zabuni haijatangazwa.
Mbaya zaidi, moja ya kampuni zilizoomba mwaka 2015, iliomba kujenga reli yote kwa gharama ya dola milioni 6.2 kwa kila kilomita, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita.

Kwa urefu wa reli unaojengwa wa kilomita 1,063 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, mkandarasi huyu alitaka alipwe dola za Marekani bilioni 6.59, sawa na Sh trilioni 15.2 za Tanzania.

Ukiacha ughali wa gharama, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa mkandarasi huyu na wengine walikuwa na upungufu mkubwa uliomsukuma hayati Rais Dk. John Magufuli kuwakataa.

“Muhimu Watanzania wakajua hili group (kundi) la wanaojiita wazalendo ni kina nani. Kwa kudokeza tu hili ni group la watu ambao wanatetea masilahi binafsi, hasa kwa sababu tayari walishakula huko nyuma na wanataka ‘ku-retire imprest’,” anasema Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na kuongeza:

“Huu ni mlolongo wa matukio. Mwaka 2016 serikali ilipoanza hatua za ujenzi, kampuni pekee iliyojitokeza kuunga mkono serikali ilikuwa Kampuni ya Yapi Merkezi. Katika hatua za awali zilijitokeza kampuni 40, lakini wakati wa kurudisha zabuni kampuni 39 kutoka China zote zilijitoa. Cha kusikitisha hata benki moja ya China iliyokuwa imeahidi kutoa fedha, ilikataa ikitoa sababu zisizokubalika.

“Kwanza, benki hiyo ilisema Tanzania imeamua kujenga reli kufuata ‘standards’ (viwango) za kimataifa, yaani kwa kufuata AREMA Standard. Wao hawakulifurahia hili kwa sababu walitaka kufuata standard za Kichina, ikiwa na maana vitu vyote viwe vya Kichina. Kama kuna mtu haelewi tunachozungumza, waulize majirani zetu Kenya. Walifanyiwa mchezo huu.

“Pili, hawakutaka Tanzania ijenge reli kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kisasa, yaani ‘European Level 2 (digital)’, ambayo ndiyo inayotumiwa duniani kote. Walitaka kutuletea teknolojia ya zamani (analogy) kama ya Kenya.

“Tatu, hawakutaka kutumia upembuzi yakinifu wa kwetu. Walitaka wafanye upembuzi wao mpya, na watwambie wanatujengea kwa bei gani. Walitaka makandarasi wote watoke kwao, ‘consultant’ wa mradi wa kwao, ‘design’ Mchina, ‘insurer’ wao na pengine mwishoni kuwa na masharti ya kuendesha wao kama walivyowafanyia majirani zetu. Na hili halikukubalika, na halikubaliki serikalini Tanzania.

“Nne, hawakupenda kubadilishwa kwa mipango yao ya kushirikiana na mafisadi wachache kufuja fedha za walipa kodi waliopanga kufanya na watu wao ambao ndio wanaohaha kila mahala kuihujumu serikali iliyopo madarakani. Mipango haikuwa yenye heri kwa taifa. Kwanza, reli iliyokuwa ijengwe Tanzania ilikuwa kama ile ya Kenya ambayo ni ‘Second hand railway with old technology’, ambayo duniani haitumiki tena,” anasema mtoa habari wetu.

Mtaalamu huyo anatofautisha reli waliyotaka kujenga makandarasi hao na hii iliyojengwa sasa na Yapi Merkezi kwa kusema: “Kwanza, reli yetu ina uwezo mkubwa sana, kwa maana ya kubeba mzigo mkubwa ekseli 35. Reli nyingi zilizojengwa Afrika zina ekseli 25. Ni reli ambazo haziwezi kuchukua mizigo mizito, hasa kwa mtindo wa ‘double stack’.

“Ukitaka kubadilisha reli ya ekseli 25 kwenda ekseli 35, hii pekee itaongeza bajeti kati ya asilimia 15-17.5 ya jumla ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Pili, reli inayojengwa Tanzania inatumia teknolojia ya kisasa ‘digital’ (European Train Control System Level) ikilinganishwa na analojia inayotembea kasi ya kilomita 80 kwa saa hapo kwa jirani zetu. Kubadilisha mfumo kutoka ‘analogy’ kwenda ‘digital’ unahitaji kutumia asilimia 7 hadi 7.5 ya jumla ya bajeti ya ujenzi wa reli ya kisasa. Na ujue kwamba unapozungumzia teknolojia kwenye reli, unazungumzia mawasiliano (signaling na telecommunications).

“Tatu, reli inayojengwa Tanzania inafanyiwa kitu kinachoitwa ‘continue welding’. Maungio ya reli yamechomelewa kwa teknolojia ya hali ya juu sana. Kubadilisha reli kuipeleka kwenye ‘continue welding’ bajeti inaongezeka kwa asilimia tano ya bajeti ya ujenzi wa reli.

“Nne, reli inayojengwa Tanzania ni ‘electrified line’ (ya umeme). Reli itatumia umeme badala ya dizeli, lakini pia itaweza kupitisha treni za dizeli ukilinganisha na walizotaka kujenga za injini za dizeli pekee.

“Mambo mawili muhimu; kwanza, treni ya umeme ni rahisi mara tatu kuliko treni ya dizeli. Ukitaka kubadilisha treni ya dizeli uweke miundombinu ya umeme inabidi utumie asilimia 25 ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Tano, reli inayoijenga Tanzania ina kasi ya kilomita 160 kwa saa ikilinganishwa na hiyo waliyotaka kutujengea ya kilomita 80 kwa saa waliyojenga Kenya. Kubadilisha kasi ya kilomita 80 kwa saa kwenda kilomita 160 kwa saa, itahitaji kutumia bajeti isiyo chini ya asilimia 15 ya gharama zilizotumika kujenga reli yote,” anasema.

Anaongeza kuwa iwapo Kenya wangependa kujenga reli sawa na ya Tanzania katika hiyo gharama ya dola za Marekani milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita, ilibidi waongeze asilimia 70 ya bei hiyo na kuwa dola milioni 10.5, sawa na Sh bilioni 24.15 kwa kilomita au asilimia 70 ya gharama zote za kujenga reli.

Hii ina maana kuwa Tanzania imejenga reli hii kwa gharama ndogo ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka. Kwa wastani hii reli ya umeme ya ‘Standard Gauge’, Tanzania inajenga kilomita moja kwa dola milioni 4.1, sawa na Sh bilioni 9.43.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa ujenzi wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro; ambacho ni kilomita 300, kwa maana ya kilomita 205 za njia kuu na kilomita 95 za njia ya kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 1.22 ikijumuisha na VAT. Ukigawa kilomita 300 kwa kiasi hicho cha fedha, unapata wastani wa dola milioni 4.07 kwa kila kilomita, ikiwamo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Kipande cha pili cha Morogoro mpaka Makutupora ya Singida chenye urefu wa kilomita 422, zikiwa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishania, kinajengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.924. Ukigawanya kwa kilomita 422 ni sawa na dola milioni 4.6 kwa kilomita moja ikijumuisha VAT.

Ikumbukwe kipande hiki cha reli kimepita milimani kwa zaidi ya kilomita 120, ikiwamo na kuchoronga mahandaki (tunnels) zaidi ya kilomita 2.7.

Kipande cha tano cha Mwanza mpaka Isaka chenye urefu wa kilomita 341 kikiwa ni njia kuu kilomita 249 na kilomita 92 zikiwa njia za kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.33. Ukigawa kwa kilomita 341 inakuwa dola bilioni 3.9 kwa kila kilomita moja, gharama hii ikijumuisha VAT.

“Sasa angalia kituko cha upembuzi yakinifu uliofanywa Novemba 2015 na kampuni inayoomba sasa kujenga vipande vilivyobaki kwa kutumia wanasiasa na wataalamu wachumia tumbo. Hawa walitaka wapewe mradi wote wa reli kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma. Kila kilomita moja walitaka kuijenga kwa dola milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita moja,” anasema mtoa taarifa na kuongeza:

“Na hiyo reli ambayo ingejengwa ni kama ya Kenya. Na kama ingejengwa tukataka ‘ku- upgrade’ ifanane na ya sasa ya kwetu, serikali ingetakiwa kutumia gharama zaidi ya asilimia 70. Maana yake nini? Ukiongeza asilimia 70 ya dola milioni 6.2 kwa kilomita moja, maana yake tungejenga kilomita moja kwa dola milioni 10.5 ili tupate reli ya ‘standard’ inayojengwa na Yapi Merkezi.

“Nini maana ya gharama hizo nilizozitaja? Maana yake ni kuwa gharama inategemea na eneo (terrain) ukipita kwenye milima na kuchoronga mahandaki, gharama ni tofauti na ujenzi wa sehemu nyingine. Hao hao waliotaka kutujengea reli ya kizamani kwa kilomita moja kwa dola milioni 6.2, leo ndio wanaopigiwa debe na wanataka kuwaamanisha Watanzania kuwa ni wazalendo. Walikwisha kusaini mkataba mwaka 2015 ambao Rais Magufuli alisema hautambui,” amesema.

JAMHURI limefahamishwa kuwa nchi nyingi Afrika zimeliwa katika ujenzi wa reli kwa kutumia gharama ya kati ya dola milioni 5.1, sawa na Sh bilioni 11.73 hadi dola milioni 8.0, sawa na Sh bilioni 18.4 kwa kilomita bila asilimia 18 ya VAT.

“Sasa kelele zimeanza wanataka tuwape hawa kazi hii. Sisi tunasema hapana. Tumsaidie Rais Samia [Suluhu Hassan] nchi yetu isiingizwe majaribuni. Utaratibu uliotumika kupata wazabuni kwa ‘Lot 2’ na ‘Lot 5’ ndiyo utumike kupata wa ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’. Kinacholengwa kufanywa hakina masilahi kwa taifa letu,” amesema mtoa habari mwingine.

Duniani ujenzi kama uliofanywa na Tanzania kwa takwimu za mwaka 2015, wastani wa ujenzi wa kilomita moja ya reli ni dola milioni 3.5, sawa na Sh bilioni 8.05 bila kodi ya VAT.
Kwa mabadiliko yaliyotokea ya bei za vifaa ikijumuisha na kupanda kwa bei ya chuma, bei ya mafuta, bei ya saruji na vifaa vingine inakadiriwa sasa kuwa wastani wa kujenga reli ya umeme kilomita moja inagharimu dola milioni 4.0, sawa na Sh bilioni 9.2.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa kelele zinazoendelea zinatokana na kuzipigia debe kampuni tatu za Kichina ambazo zimewasilisha serikalini maombi ya kujenga kipande cha 3 na cha 4 kwa wastani wa bei ya dola milioni 5.5, sawa na Sh bilioni 12.65 kwa kilomita. Gharama hii iko juu kwa zaidi ya dola milioni 1.5, sawa na Sh bilioni 3.45 ikilinganishwa na gharama za sasa za ujenzi zinazotumika.

“Kaka hapa kinachofanyika ni watu wanataka wagawane hizo Sh bilioni 3.45. Tukiwakubalia nchi itapoteza zaidi ya Sh trilioni 2. Hizi fedha zitaingia mifukoni mwa watu na kwa kweli haikubaliki. Tujenge reli kwa utaratibu wa zamani ambao tumeanza nao. Huu mchakato wa zabuni ukianza sasa, kwanza, hautakamilika, lakini hata ukikamilika ni miaka mitatu ijayo. Tutapoteza mwelekeo. Tuendelee kama tulivyokuwa tumalize hii reli, wanaopigania matumbo yao tuachane nao,” amesema mtoa habari mwingine.

JAMHURI limezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, aliyekiri kuyasikia hayo maelezo wanayotaka mchakato uanzishwe wa kutangaza vipande vya 3 na 4 vya reli naye akasema: “Sisi tupo kumsaidia Mheshimiwa Rais. Tunaamini kwa masilahi mapana ya nchi hii, reli hii ujenzi wake ulianza na unaendelea vizuri.

“Kuna utaratibu wa kisheria wa ‘single sourcing’ ikiwa anayetoa zabuni anazifahamu gharama halisi za mradi. Naamini utaratibu huu ni mzuri na utatupunguzia kelele. Rejea yaliyotokea mwaka 2016. Kelele zilikuwa nyingi kuliko sasa na tuliendelea kwa masilahi mapana ya taifa letu. Matunda bora kabisa ya ujenzi yanaonekana.”

Kadogosa anasema anasubiri mchakato wa kumpata mzabuni unaondelea serikalini ukamilike ‘Kazi Iendelee’.
JAMHURI linafahamu kuwa kuna kundi la watu wanaoamini kuwa baada ya kufariki dunia Rais John Magufuli, kwa sasa wanaweza kupenyeza masilahi yao binafsi katika miradi ya kitaifa na kujipatia fedha nyingi. Gazeti hili litaendelea kufuatilia sakata la mradi huu kuhakikisha nchi haiingizwi katika gharama zisizostahili na wajanja wachache.

Mwisho.....
 
Mwamba alikuwa na misimamo, vision na mwenye kupenda mambo yatokee haraka haraka, hakuwa mbabaishaji na hakufanya mambo kwa ajili ya kufurahisha mtu bali alifanya mambo aliyoamini yanamanufaa kwa taifa hata kama wengine walipinga yeye hakujali.

Kuna vitu watu waliamini haviwezekani kwa sasa ila kwa huyu mwamba viliwezekana tena kwa kasi ya ajabu, mfano kuhamia Dodoma, ujenzi wa bwala la Nyerere ujenzi wa daraja la Busisi, kununua ndege 11 kwa miaka mitano.

Mwamba alikuwa akihutubia lazima ukute watu kwenye vibanda umiza waafuatilia hotuba, bodaboda njiani wamefungua redio wanafuatilia kujua leo mwamba anakuja na lipi jipya. Hotuba zake zilijaa matumaini na faraja, hakupenda kutukatisha tamaa watu wake, ilifika mahali tulijiona watanzania ni kama watu wa ulaya tu maana alituaminisha sisi ni matajiri na akasema anataka wazungu wawe wanakuja kununua mitumba kwetu. Daah! ama kweli kizuri hakidumu.
 
Asante kwa taarifa ila lot 4 ilishapata mkandarasi ambaye ni mchina, alishinda zabuni tangu Magu akiwa madarakani kinachotakiwa ni usimamizi kuhakikisha wanajenga kwa standards tunazotaka sisi, lot 3 inasemekana Yerpi Merkezi amepewa.
 
Huyu ndiye Magufuli, mwamba wa Afrika.
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

6. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amefariki zaidi ya miongo miwili( miaka 20) bado anakumbukwa hadi leo hii. Miezi 6 kitu gani ?
 
Asante kwa taarifa ila lot 4 ilishapata mkandarasi ambaye ni mchina, alishinda zabuni tangu Magu akiwa madarakani kinachotakiwa ni usimamizi kuhakikisha wanajenga kwa standards tunazotaka sisi, lot 3 inasemekana Yerpi Merkezi amepewa.
Ubaya wa kifo cha JPM ni kukosa mtu wa kuzuia ufisadi wa JK nchi hii
 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amefariki zaidi ya miongo miwili( miaka 20) bado anakumbukwa hadi leo hii. Miezi 6 kitu gani ?
Natumai umejijibu kwamba viongozi walioacha alama ni ngumu kuwasahau, kama ilivyokuwa ngumu kumsahau Nyerere pia itakuwa ngumu kumsahau Magufuli kwa mambo aliyoyafanya, wenye chuki mvumilie tu hamna jinsi mana miradi aliyoianzisha itadumu kwa karne nyingi na ndiyo itakayofanya akumbukwe daima.

Nyerere aliacha alama nyingi kama mabwawa ya kuzalisha umeme na reli na ndiyo maana hasahauliki na Magufuli naye ni hivyo hivyo, hawa viongozi wengine baada ya Nyerere na kabla ya Magu hakuna alama za kipekee walizoacha na ndiyo maana inakuwa rahisi kuwasahau lakini sio Nyerere na Magu, ni ngumu sana.

Viongozi waliofuata baada ya Nyerere walipimwa kulingana na uongozi uliotukuka wa Mwalimu na baadaye wakaonekana hawatoshi mpk pale tulipompata aliyetosha viatu vya Nyerere, sasa kilichobaki ni hawa wanaofuata baada ya JPM kupimwa kulingana na uongozi uliotukuka wa Magu.
 
Ubaya wa kifo cha JPM ni kukosa mtu wa kuzuia ufisadi wa JK nchi hii
Kweli kabisa mkuu, tunaona mipango ya wazi wazi ikisukwa kila kukicha japo hawataweza kwani mtanzania wa leo sio wa jana, na kama watalazimisha iwe kama walivyozoea basi lazima kitanuka mana mbegu ya ujasiri aliyoiacha Magu kwa watanzania imeshaota mizizi.
 
Ndoto za alinacha hizo
 
Shujaa wa kweli wa Watanzania wanaojitambua. Ni aibu kubwa sana kwa Kiongozi wa Tanzania kwenda kujikomba komba huko nje na kutafuta umaarufu na kuwatukuza walio na ngozi nyeupe, ni aibu kubwa sana.

JPM ndiye mwanzilishi wa kujitegemea kwa vitendo kuanzia pesa za uchaguzi mkuu, kujenga mahospitali kila kona, kuwezesha umeme kumfikia kila Mtanzania, na mengineyo mengi.

RIP JPM. Tutakukumbuka daima.
Shida yenu nyie watu wa magufuli ndo hiyo tu, UJINGA! NI WAJINGA MNO! Mmeharibiwa akili na sasa mnekuwa km wafu fulani hiviiii....hamuwazi sawasawa. Aliyeenda kujikomba nani?!! Hv chuki hizo, majungu na wivu mlizoachiwa na Shujaa wenu wa kizamani (in msigwa's voice) zitaisha lini?

Kiongozi wenu alikuwa na mazuri yake lakini alikuwa na mapungufu yake pia. Moja ya mapungufu yake ilikuwa kutanguliza maguvu mbele, akili nyuma. Mengine ni UDINI NA UKANDA.

Amini nakwambia, kama una imani ya dini, Mungu ana maana yake kubwa katika kumtanguliza mh Magufuli......ana maana kubwa sana, ndo maana binafsi nawacheki tu na kucheka mnavyokufuru kila leo humu mnapojatibu kuziondoa frustrations zenu kwa kuwatwisha watu mizigo isiyo yao, eti wamemuua!! Mungu gani huyo wa kupenda kikundi kidogo na kuchukia taifa zima hili? Mi naamini analipenda taifa zaidi kuliko kikundi kidogo cha watu na ndo maana akafanya alilofanya; ana mamlaka makuu, angeweza kuzuia tu km angeona kuna haja ya kufanya hivyo! Acheni ujinga, viongozi wengine wataongoza kwa maono yao siyo lazima yawe km ya magufuli; watachukua mazuri na yale ya hovyo na kishamba watawaachia wafuasi wake mhangaike nayo!!
 
'Anapendwa' na uneducated class because they can't see past his propaganda and cooked statistics.
Kisiasa hao ndiyo wengi kuliko matajiri hao ndiyo muhimu kwenye sanduku la kuliko matajiri.

****************
Mtoa mada The best 007 baada ya wiki toa majibu kutokana na comments.

Humu humu kuna majibu ya NDIYO au HAPANA.
 
Back
Top Bottom